Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Wanajamvi Bernard Membe alikuwa atoe ufafanuzi juu ya meli za Iran kusajiliwa Zanzibar na kupeperusha bendera ya Jamhuri ya Tanzania. Naomba kujuzwa kasema nini mpaka sasa.
Bernard Kamilius Membe
Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa ku...zingatia uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja. Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!