Membe - Chadema walikuja kwangu wakiwa na njaa

Membe anachekesha sana, kwa hiyo anataka kusema kuwa wakati wote chakula kinapikwa kingi nyumbani kwake kusubiri wageni kama akina Lema? au ilikuwaje kikaandaliwa chakula cha kuwatosha kama kulikuwa hakuna mawasiliano kabla? Mtu anakana vipi taarifa zilizorushwa kwenye tv?
 
Hivi kabisa na akili zenu CDM mlitegemea Membe ajiunge na nyie kweli mliingia choo cha kike
 
Maelezo ya Membe ni ya kutapa tapa. Huyu bwana anafikiri Wanzania wa leo ni wajinga na ni watu wa kupelekwa pelekwa tu na porojo. Inawezekanaje hao vijana waone au kuonyeshwa kwa Membe na kuamua kwenda kwake kienyeji bila kualikwa? Yeye membe alikuwa amendaa chakula chake na familia yake. Inawezekanaje vijana wote wale wakaingia kwake ghafla na kupata chakula ambacho tayari kilikuwa kimeandaliwa na wao wakala na kushiba. Kwa haraka haraka inaonekana Membe anajikosha kwa Wana-CCM wenzake. Yeye bila shaka aliwaalika wale vijana na sasa anaona njia ya kujinasua ni kupiga porojo ambazo kutokana na ukilaza wa Magamba, atafanikiwa! Kwanza arudishe fedha za rushwa ya mafuta na gesi alizo-zikimbiza huko nje.


Naomba niulize maswali machache tu.
1.Anasema alikuwa anakula akamwambia mlinzi awakaribishe alipoambiwa vijana wa Chadema,
je,alijua hao vijana ni kina nani?

2.Hicho chakula alikuwa amekiandaa akijua kuwa wanakuja?

3.Mbona kwenye taarifa ya siku ile ITV alionekana akiwapokea nje
akawakaribisha ndani,au analiaga nje?

4.Hao waandishi wa habari walitoka wapi?

5.Hata mimi nikijitambulisha kama kijana wa chadema atanikaribisha chakula cha mchana?
 
Membe akiendelea kukanusha nitatoa CD nisambaze bure msome,make tulimrecord by G.lema...akihutubia Manzense bakhresa wiki jana.
 
Kwani umeambiwa huwa hawali?viomgozi wenu waliwakaribisha wenyewe lakini leo wanageuka,
lakini si vema kumsema mtu kwa ajili ya chakula,
kwani yeye hajawahi kukaribishwa/kula kwa watu?
Huo ni ujinga uliopitiliza ukimueleza mtu mwenye akili timamu lazima akushangae.
Kaishiwa hoja za kisiasa, sasa amebakiwa na maneno ya chumbani na mkewe, tena hata mkewe anaweza akamshangaa pia...
 
We kweli hujui utamu wa ubunge, lazima ajipendekeze ili arudishiwe ubunge. Lakini ndio ajiangalie tu, tabia ya mtoto wa kiume kujipendekeza ni mbaya.

Nakushangaa na wewe dume zima unajipendekeza kwa Nape kuja kuandika ujinga huku!
 
Back
Top Bottom