mlagha
Bahati nzuri miminimeshiriki press Conference hii. Mhe. Membealitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Wizara ambayoyamekuwa yakiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari isivyo.
Masuala hayo ni pamoja na taarifa kuhusu uwasilishwaji wa Ripoti ya Tanzaniakuhusu Mpango wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
Katika suala hili Mhe. Membe alitoa ufafanuzi kuwa, ni kweli Mhe. Rais hatowezakuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tanzania katika Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchina Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababamwezi Julai, 2012 kwa kuwa Timu ya Umoja wa Afrika chini ya APRM inayopitiaripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi hiyo. Hivyo Tanzania itawasilisharipoti yake Januari 2013baada ya timu hiyo kuipitia na si kwa sababu Tanzaniainadaiwa Dola za Marekani laki nane (800,000) kama mchango wake kwa mpango huo.
APRM ni chombo kilichoanzishwa na Serikali za Afrika na kwa hapa Tanzaniakinaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje, ni chombo cha hiari kwa nchi za Afrikakujitathmini zenyewe kiutawala bora, si kweli kuwa Rais atashindwa kuwasilishaRipoti ya Tanzania AU kwa sababu hatujalipa deni, bali ni kwa sababu timuinayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi yake hivyo tunatarajiakuwasilisha ripoti yetu mwezi Januari 2013 wakati wa kikao kingine cha Wakuu wanchi wa AU, alisema Mhe. Membe.
Kuhusu suala la fedha zilizotoweka Wizarani, Mhe. Membe alieleza kuwa hakuna fedha zilizopotea isipokuwaWizara imewasimamisha kazi Watumishi watano waliofanya mchakato wa kuhamishakiasi cha shilingi bilioni 3.5 kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya ziaraza Mhe. Rais za Addis Ababa, Geneva,
na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuliyaani Katibu Mkuu ambaye hakuwepo wakati mchakato huo unafanyika.
Aliongeza kuwa, Watumishi hao wamesimamishwa kazi ili kupishauchunguziunaofanywa na kamati iliyoundwa ili kujiridhisha kama taratibu zakifedha zilifuatwa au kukiukwa katika mchakato huo mzima.
Tarehe 1 Machi, 2012 wakati mimi sipo Wizarani wala Naibu Waziri, Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu kuna mchakato wa kuhamisha fedha kiasi chashilingi bilioni 3.5 ulifanywa kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya safariza Mhe. Rais za Geneva, Addis Ababa,
..na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli.Timu inayojumuisha watu kutoka TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Wizara na Ofisi yaMkaguzi Mkuu wa Serikali imeundwa ili kuchunguza suala hilo ili kujua kamataratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa na uchunguzi ukikamilika tutawekahadharani hakuna cha kuficha, alisema Mhe. Membe.
Vile vile, Mhe. Membe alipinga uvumi unaoenezwa kuwa amekitabiria ushindiChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kusema kuwa yeye si mtabiri nakwamba yeye ni mwanachama halisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa maneno na kwamatendo.
Mhe. Membe aliongeza kuwa alichokifanya ni ukarimu kwakuwakaribisha Vijana wa CHADEMAjimboni kwake Mtama mkoani Lindi na kushiriki nao chakula nyumbani kwake.
Ukarimu hauna udini, rangi wala itikadi, vijana wa CHADEMA walikuja nikawakaribisha kwa chakula nyumbani, na leonataka niwape somo kidogo, upinzani sio uadui, nchi inayoona upinzani ni uaduihaiko salama wala haitaendelea,alisisitiza Mhe. Membe.