Bwana Kiwuyo
Member
- Oct 6, 2013
- 8
- 3
Jamii Forums ni moja ya vyanzo vya habari au tetesi zinazoendelea nchini iwe ni za ukweli au za uwongo.Ila kwa asilimia kubwa habari za Jamii Forums ni za kimihemko zaidi na kuvunjiana heshima au kuharibiana malengo na maisha ya kisiasa,uchumi au kijamii.
Sisi marafiki zake Membe tumesoma mjadala unaohusu sakata la Iptl lililoibuliwa na Kafulila ndani ya Bunge la Bajeti miezi kadhaa nyuma humu Jamii Forums tangu lilipoanza hadi lilipofikia sasa.Wanatajwa wafanyabiashara,majaji na wanasiasa kuhusika na sakata hili linaloigharimu nchi na serikali kwasasa.
Baadhi ya waliotajwa yupo pia Jack Gotham!Hatujajua ni misingi ipi au ushahidi upi ambao umetumika kumtaja Jack Gotham na kumuunganisha Membe katika sakata hili.Haina maana ukiwa rafiki na mtu basi uhusishwe na kila baya analofanya.Membe asihusishwe na Iptl kwasababu tuna imani kubwa kwamba hakuna ushahidi either direct au indirect unaomgusa katika Iptl.
Membe ni kati ya makada wa Ccm ambao hawaungi mkono pesa za Iptl(escrow)kuchotwa BOT.Membe hana historia yoyote mbaya ya kuhusika au kujihusisha na ufisadi wa aina yoyote ile ndani na nje ya nchi.Na pia Membe hawezi kuambatana na fisadi au mla rushwa.
Kama kweli Jack Gotham anahusika kwa namna moja au nyingine katika Iptl Saga basi tuna imani Membe ambaye sisi ni rafiki yetu atachukua hatua za nini afanye ili kuhakikisha haki inapatikana kwa kutoa ushirikiano wa namna moja au nyingine ili wahusika wa Iptl Saga wawajibishwe na huo ndio uzalendo ambao Membe anao.
Tunatoa wito kuwa watanzania msiaminishwe lolote kuwa Membe anahusika kwenye sakata la Iptl na asihusishwe na yeyote aliyeshiriki katika sakata la Iptl.Ahsanteni sana!
Imetolewa na Friends Of Hon.Membe.