Membe adaiwa kusaidia kampuni ya wanandugu (MEIS) kuchota bilioni 54

Kwahiyo mmekubali mnajaribu kimchavua MEMBE kupitia gazeti lenu la MTANZANIA kisa kujistukia kwamba, au kwa hisia zakinyume na maumbile umlizonazo ,eti yeye MEMBE anawachafua kupitia RAIA MWEMA? Je kama yeye MEMBE ausiki na vijishutma vyenu thidi yake kipitia RAIA MWEMA, umtajikaza kiume angalau sekunde kazaa na kumtaka radhi,na we JUHA tu kwamba unajidhalilisha bure

Duh, I smell desperation here! You have completely lost it! Mimi naangalia pande zote za mraba. Watu hapa mmelalamika kwamba Membe anachafuliwa na MTANZANIA - hayo hayakuwa maneno yangu. Lakini ukiuliza mbona inajulikana kwamba na yeye Membe anachafua wenzake, unachopata ni matusi na kejeli. Logical conclusion is that Membe's hands are dirty.
 
U rais bado upo mbali jamani!. Tunajua nia zenu. Pande zote Vuteni subra tekelezeni ilani na sera za vyama vyenu kwanza. Mtakuja kuvuta shuka kumesha kuchwa!
 
Duh, I smell desperation here! You have completely lost it! Mimi naangalia pande zote za mraba. Watu hapa mmelalamika kwamba Membe anachafuliwa na MTANZANIA - hayo hayakuwa maneno yangu. Lakini ukiuliza mbona inajulikana kwamba na yeye Membe anachafua wenzake, unachopata ni matusi na kejeli. Logical conclusion is that Membe's hands are dirty.
Then again you could be right, desparation it is, yet again why are you so bent on proving MEMBE as a villan? I could be more desparate than arafat,Mandela, osama bin laden or the next man ,but you are obsesesed with villifying MEMBE, if thats the case,one can only see you as a nugget short of a happy meal,then again i might just be desperate, you think?
 
KAMPUNI ya Mohamed Enterprises (MeTL), kupitia Mahakama Kuu, imekwamisha malipo ya dola milioni 34 za Marekani (Sh bilioni 54.4)bil- ambazo zilikuwa zichukuliwe na kampuni ya MEIS Industries katika mazingira yenye utata.

Kampuni ya MEIS Industries inamilikiwa na wanandugu watatu ambao ni Islam Ally Saleh, Merey Ally Saleh na Saleh Ally Saleh.

MEIS ilikuwa imeamriwa ichukue fedha hizo mali ya Serikali ya Libya, ilhali kukiwa na kesi ya msingi namba 110/2010 iliyofunguliwa na MeTL dhidi ya Serikali hiyo. Kumekuwapo msukumo mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia wa kutaka MEIS ilipwe mabilioni hayo, ilhali ikiwa haina haki hiyo kisheria.

Duru za kimahakama zinaonyesha kuwa MeTL walifungua kesi hiyo na kupeleka samansi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyo chini ya Waziri Bernard Membe, ili kupitia kwake, afikishiwe Balozi wa Libya nchini. Hata hivyo, Wizara ya Membe katika namna ya kushangaza ilipokea samansi hiyo, lakini ikakataa kuiwasilisha kwa Balozi wa Libya.

Imebainika kuwa, wakati kesi ya MeTL ikiwa inaendelea siku chache badaye MEIS Industries ilifungua kesi namba 124/2010 dhidi ya Serikali ya Libya ikitaka ilipwe dola milioni 20 za Marekani na gharama za usumbufu za dola milioni 14.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilitoa ushirikiano kwa kuhakikisha samansi inapelekwa kwa Balozi wa Libya nchini, tofauti na ilivyokuwa imeikatalia kampuni ya MeTL inayowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Dk. Masumbuko Lamwai.

Kesi hiyo ilisikilizwa upande mmoja wa walalamikaji na hukumu ikatolewa na Mahakama Kuu kwa kuamuru Benki ya TIB iilipe MEIS dola milioni 34 za Marekani.

Katika namna ya kustaajabisha, Balozi wa Libya hapa nchini akijua wazi kwamba kuna kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Serikali ya Libya, hakuweka wakili wa kuitetea Serikali, na matokeo yake ndiyo yaliyowezesha kesi isikilizwe upande mmoja na kutolewa hukumu.

Duru za uchunguzi zimebaini kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilikuwa bega kwa bega na MEIS Industries pamoja na Balozi wa Libya nchini kuhakikisha kesi hiyo inaendeshwa na kufikia tamati kama ilivyotokea.

MEIS Industries inamilikiwa na watu wanaotajwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na baadhi ya maofisa waandamizi kabisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Imebainika kuwa TIB baada ya kuamriwa ilipe kiasi hicho cha fedha, ilikataa kulipa kwa maelezo kwamba haikuwa na ruksa ya kuzitoa.

Kutokana na msuguano huo, MeTL walilazimika kuweka zuio mahakamani ili TIB wasiilipe MEIS Industries.
Aidha,
utata wa namna fedha hizo zinavyotaka kuchukuliwa umejitokeza pia kwenye mchakato wa kisheria ambapo wakili Joseph Thadayo ndiye mwanasheria wa MEIS, ndiye wakili wa Membe na amekuwa pia akilipwa na TIB kwa kazi za kisheria anazowafanyia. “Hapa kuna maswali mengi ya kuuliza juu ya uhusiano wa MEIS, Membe na Thadayo,” kimesema chanzo chetu cha habari.

Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa MeTL inataka ilipwe
fedha hizo kinyemela, imebainika kuwa MeTL ndiyo inayojitahidi kuzuia malipo hayo ambayo MEIS wanahaha kuhakikisha wanalipwa.

Wakati Membe na Balozi wa Libya wakinukuliwa wakisema Massoud Mohamed Nasr, hatambuliki,
MTANZANIA imefanikiwa kupata waraka unaoonyesha kuwa Nasr ndiye anayetambuliwa kwa nyaraka rasmi za Serikali ya Libya kukusanya madeni ambayo Serikali hiyo imekuwa ikiidai Serikali ya Tanzania tangu Februari 12, 1983. Uhalali wa Massoud upo hata kwenye nyaraka ambazo zipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nasr alishalipwa dola milioni nne za Marekani kama kamisheni kwa kazi hiyo, jambo ambalo Ubalozi wa Libya hapa nchini unalifahamu, na hivyo kuondoa dhana kwamba hatambuliki. Dk. Lamwai amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimpa tahadhari juu ya kutowajibika kwake katika suala la kesi iliyofunguliwa na MeTL.

Amemwandikia pia Balozi wa Libya juu ya uamuzi wake wa kutotaka kufanya mipango ya kuitetea Serikali yake katika kesi namba 124/2010.

Katika kesi nyingine namba 110/2010 walalamikaji MeTL wamewasilisha mahakamani pingamizi dhidi ya wakili Kamara na kampuni ya The Crest Professional Attorneys kwamba hawana sifa ya kuiwakilisha MEIS Industries, kwa vile mwaka 2009 walitoa ushauri wa kisheria kwa suala hilo hilo lililo mahakamani.

Shauri hilo halijatolewa uamuzi na Mahakama. Katika kesi namba 124/2010, MeTL pia imewasilisha pingamizi kama hilo kwa Kamara na kampuni hiyo na Jaji amemtaka Kamara asiwajibike kwa shauri kati ya MeTL na MEIS Industries.

Katika hatua nyingine kampuni ya MeTL imelalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti kumhusisha Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji kwenye sakata hili. Ofisi ya Mwanasheria wa MeTL, imesema Mohamed si Mkurugenzi wala mwanahisa katika MeTL, bali mhusika ni Ghulam Dewji ambaye ni baba yake.

“Mohamed kuwa na uhusiano na Ghulam kwa sababu ni baba yake haina maana kwamba ni Mkurugenzi au mwana hisa wa MeTL, tena habari zinazoandikwa zinamhusu Ghulam, lakini kwanini iwekwe picha ya Mohamed? Huu ni mpango wa kuchafuana.

“Hatutaki suala hili liingiliwe kisiasa, kirafiki au kidiplomasia, Mahakama iachwe iwe huru kuamua, vyombo vya habari visitumiwe kupotosha ukweli,” imesema taarifa ya mwanasheria wa MeTL.

source:Mtanzania

Hii yote ni kutafuta pesa za kampeni 2015 au?

Kama Libya mambo yashaharibika, then there is always IRAN au mshasahau ya 2005?
 
Mara membe anachafuliwa,mara ritz1 anamchafua january makamba,mara asha rose migiro anaandaliwa.duu,tutasikia mengi hadi kufikia 2015,Mungu atupe uzima! chadema jiandaeni kuchukua nchi,huku magamba wananyukana nyie nendeni kwa wananchi kuwaelezea sera zenu...by the time wanamalizana,watamkuta mwana sie wao,hvyo wataishia kueleka jiwe!
hii movie mbona kali! Nilikuwa sijaisikia
 
sin hakika kama haya madai ni ya kweli au lah, ila kinachonitia wasiwasi ni gazeti ambalo limeripoti habari hii. sote tunajua kuwa gazeti la mtanzania linamilikiwa na Rostam na kazi yao kubwa ni kumsafisha Lowasa na kuwachafua watu wanaoonekana kuwa ni tishio kwake. Membe ni mmoja kati ya watu wanaonekana ni tishio kwa Lowasa since anatajwa kuwa na nia ya kugombea urais mwaka 2015. Sisemi kama ni habari za uongo ila nadhani uchunguzi wa kina unahitajika juu ya swala hili.
nawasilisha

Tuhoji ukweli wa mambo kwani hakuna siri kuwa membe alijihusisha sana na gadafi na aliwahi kupinga kutambuliwa kwa serikali mpya ya libya sasa tusianze kupinga kuna mantiki kwenye taarifa hiyo
 
Usafi wake upi huo? Wa kutumia nafasi yake kukusanya pesa kutoka maofisa wa ngazi za juu wa mataifa ya nje kujenga kitita chake cha kugombea uraisi 2015? Membe hawezi kulalamika eti gazeti la MTANZANIA lina mchafua wakati na yeye yupo bize kuchafua wenzake kupitia magazeti kama RAIA MWEMA.

Ndio maana mawakala wake wamezuguka nchi nzima kutembeza mshiko wa laki tatu kila mjumbe wa mm hee naye ameanza kujitokeza kwa nguvu sana siku za hivi karibuni kumbe jeuri ya fedha za haramu
 
Hii JF bwanaa kweli nimeamini ina vichwa TAKUKURU na vichwa panzi wengine wapitie huu uzi pia itawasaidia.
 
Hatimaye MEMBE amekiri kuwa ana uhusiano wa karibu na ile kampuni ya MEISS ambayo anataka iende jimbon kwake ikajenge kiwanda cha saruji.

Membe amesema kuwa kampuni hiyo ana uhusiano nayo kwa kua ni rafiki zake.....

My take:
Sakata hili liliibuka last weekend ambapo gazeti la Mtanzania liliripoti na inaendelea hukohuko kwenye gazeti la mwanamagamba(mtanzania)

SOMA:

KAMPUNI ya Mohamed Enterprises (MeTL), kupitia Mahakama Kuu, imekwamisha malipo ya dola milioni 34 za Marekani (Sh bilioni 54.4)bil- ambazo zilikuwa zichukuliwe na kampuni ya MEIS Industries katika mazingira yenye utata.

Kampuni ya MEIS Industries inamilikiwa na wanandugu watatu ambao ni Islam Ally Saleh, Merey Ally Saleh na Saleh Ally Saleh.

MEIS ilikuwa imeamriwa ichukue fedha hizo mali ya Serikali ya Libya, ilhali kukiwa na kesi ya msingi namba 110/2010 iliyofunguliwa na MeTL dhidi ya Serikali hiyo. Kumekuwapo msukumo mkubwa wa kisiasa na kidiplomasia wa kutaka MEIS ilipwe mabilioni hayo, ilhali ikiwa haina haki hiyo kisheria.

Duru za kimahakama zinaonyesha kuwa MeTL walifungua kesi hiyo na kupeleka samansi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyo chini ya Waziri Bernard Membe, ili kupitia kwake, afikishiwe Balozi wa Libya nchini. Hata hivyo, Wizara ya Membe katika namna ya kushangaza ilipokea samansi hiyo, lakini ikakataa kuiwasilisha kwa Balozi wa Libya.

Imebainika kuwa, wakati kesi ya MeTL ikiwa inaendelea siku chache badaye MEIS Industries ilifungua kesi namba 124/2010 dhidi ya Serikali ya Libya ikitaka ilipwe dola milioni 20 za Marekani na gharama za usumbufu za dola milioni 14.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilitoa ushirikiano kwa kuhakikisha samansi inapelekwa kwa Balozi wa Libya nchini, tofauti na ilivyokuwa imeikatalia kampuni ya MeTL inayowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Dk. Masumbuko Lamwai.

Kesi hiyo ilisikilizwa upande mmoja wa walalamikaji na hukumu ikatolewa na Mahakama Kuu kwa kuamuru Benki ya TIB iilipe MEIS dola milioni 34 za Marekani.

Katika namna ya kustaajabisha, Balozi wa Libya hapa nchini akijua wazi kwamba kuna kesi katika Mahakama Kuu dhidi ya Serikali ya Libya, hakuweka wakili wa kuitetea Serikali, na matokeo yake ndiyo yaliyowezesha kesi isikilizwe upande mmoja na kutolewa hukumu.

Duru za uchunguzi zimebaini kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilikuwa bega kwa bega na MEIS Industries pamoja na Balozi wa Libya nchini kuhakikisha kesi hiyo inaendeshwa na kufikia tamati kama ilivyotokea.

MEIS Industries inamilikiwa na watu wanaotajwa kuwa na uhusiano wa karibu mno na baadhi ya maofisa waandamizi kabisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Imebainika kuwa TIB baada ya kuamriwa ilipe kiasi hicho cha fedha, ilikataa kulipa kwa maelezo kwamba haikuwa na ruksa ya kuzitoa.

Kutokana na msuguano huo, MeTL walilazimika kuweka zuio mahakamani ili TIB wasiilipe MEIS Industries. Aidha, utata wa namna fedha hizo zinavyotaka kuchukuliwa umejitokeza pia kwenye mchakato wa kisheria ambapo wakili Joseph Thadayo ndiye mwanasheria wa MEIS, ndiye wakili wa Membe na amekuwa pia akilipwa na TIB kwa kazi za kisheria anazowafanyia. "Hapa kuna maswali mengi ya kuuliza juu ya uhusiano wa MEIS, Membe na Thadayo," kimesema chanzo chetu cha habari.

Wakati baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kuwa MeTL inataka ilipwe fedha hizo kinyemela, imebainika kuwa MeTL ndiyo inayojitahidi kuzuia malipo hayo ambayo MEIS wanahaha kuhakikisha wanalipwa.

Wakati Membe na Balozi wa Libya wakinukuliwa wakisema Massoud Mohamed Nasr, hatambuliki, MTANZANIA imefanikiwa kupata waraka unaoonyesha kuwa Nasr ndiye anayetambuliwa kwa nyaraka rasmi za Serikali ya Libya kukusanya madeni ambayo Serikali hiyo imekuwa ikiidai Serikali ya Tanzania tangu Februari 12, 1983. Uhalali wa Massoud upo hata kwenye nyaraka ambazo zipo katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nasr alishalipwa dola milioni nne za Marekani kama kamisheni kwa kazi hiyo, jambo ambalo Ubalozi wa Libya hapa nchini unalifahamu, na hivyo kuondoa dhana kwamba hatambuliki. Dk. Lamwai amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimpa tahadhari juu ya kutowajibika kwake katika suala la kesi iliyofunguliwa na MeTL.

Amemwandikia pia Balozi wa Libya juu ya uamuzi wake wa kutotaka kufanya mipango ya kuitetea Serikali yake katika kesi namba 124/2010.

Katika kesi nyingine namba 110/2010 walalamikaji MeTL wamewasilisha mahakamani pingamizi dhidi ya wakili Kamara na kampuni ya The Crest Professional Attorneys kwamba hawana sifa ya kuiwakilisha MEIS Industries, kwa vile mwaka 2009 walitoa ushauri wa kisheria kwa suala hilo hilo lililo mahakamani.

Shauri hilo halijatolewa uamuzi na Mahakama. Katika kesi namba 124/2010, MeTL pia imewasilisha pingamizi kama hilo kwa Kamara na kampuni hiyo na Jaji amemtaka Kamara asiwajibike kwa shauri kati ya MeTL na MEIS Industries.

Katika hatua nyingine kampuni ya MeTL imelalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti kumhusisha Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji kwenye sakata hili. Ofisi ya Mwanasheria wa MeTL, imesema Mohamed si Mkurugenzi wala mwanahisa katika MeTL, bali mhusika ni Ghulam Dewji ambaye ni baba yake.

"Mohamed kuwa na uhusiano na Ghulam kwa sababu ni baba yake haina maana kwamba ni Mkurugenzi au mwana hisa wa MeTL, tena habari zinazoandikwa zinamhusu Ghulam, lakini kwanini iwekwe picha ya Mohamed? Huu ni mpango wa kuchafuana.

"Hatutaki suala hili liingiliwe kisiasa, kirafiki au kidiplomasia, Mahakama iachwe iwe huru kuamua, vyombo vya habari visitumiwe kupotosha ukweli," imesema taarifa ya mwanasheria wa MeTL.

Source: Mtanzania
poa tu - mbwa kula mbwa ndiyo mtindo wa kisasa ndani ya chama chetu.

ni mwendo wa kuviziana kwa kwenda mbele - ikifika muda wake #team-membe nao watafukua tu makaburi ya 1.5tr, mv Bagamoyo, mabilioni ya kesi ya samaki, mabilioni yailiyolipwa kukomboa bombardier iliyokuwa imeshikiliwa, nk, nk, nk, nk.
 
Back
Top Bottom