Membe arejeshewa kadi yake ya CCM

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, leo amekabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Shaka Hamdu Shaka, makabidhiano hayo yamefanyika Chiponda mkoani Lindi..

Awali Membe alifukuzwa uanachama na chama chake na kisha kujiunga na chama cha ACT Wazalendo na aligombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. ambapo kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, mnamo Machi 31 mwaka huu kilitangaza kumsamehe na kumrudishia uanachama wake baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha.

Membe amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na wanachama wengine zaidi ya 1,000 wa vyama vya upinzani waliorejesha kadi katika mkutano huo.
20220529150548_776875756_7018202698457962002_640_365_85_webp(2).jpg
 
Jamaa alimkimbia mwendazake, sasa hivi karudisha majeshi ...karudi huku akiwa kibogoyo..meno yote kwishaaa...wameyang'oa.

Ukiwa ndani ya CCM huwezi kuipinga, ukiwa na mawazo tofauti wanaku fix..dhambi hii ilianzia kwa Mh. Kolimba pale Dodoma kuhojiwa (RIP).

Kwa hiyo tusimlaumu sana huyu Mzee, anaungana na wenzake akina Sumaye, Lowassa.

Kwa katiba hii CCM ina nguvu mno maana kupambana na CCM ni kupambana na dola.

Pia nawapa pole wale wazee walitaka ku beep baada ya mwendazake kuondoka, majibu majibu yao washayapata.
 
CCM si wamesema na wao wanatoa card za kidigitali, au wamesahau uongo wao?
 
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, leo amekabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Shaka Hamdu Shaka, makabidhiano hayo yamefanyika Chiponda mkoani Lindi..

Awali Membe alifukuzwa uanachama na chama chake na kisha kujiunga na chama cha ACT Wazalendo na aligombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. ambapo kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, mnamo Machi 31 mwaka huu kilitangaza kumsamehe na kumrudishia uanachama wake baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha.

Membe amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na wanachama wengine zaidi ya 1,000 wa vyama vya upinzani waliorejesha kadi katika mkutano huo.
mtego wa panya kwa bi tozo wa royal tour
 
Jamaa alimkimbia mwendazake, sasa hivi karudisha majeshi ...karudi huku akiwa kibogoyo..meno yote kwishaaa...wameyang'oa.

Ukiwa ndani ya CCM huwezi kuipinga, ukiwa na mawazo tofauti wanaku fix..dhambi hii ilianzia kwa Mh. Kolimba pale Dodoma kuhojiwa (RIP).

Kwa hiyo tusimlaumu sana huyu Mzee, anaungana na wenzake akina Sumaye, Lowassa.

Kwa katiba hii CCM ina nguvu mno maana kupambana na CCM ni kupambana na dola.

Pia nawapa pole wale wazee walitaka ku beep baada ya mwendazake kuondoka, majibu majibu yao washayapata.
Usisahau alikatwa mkia ukabaki kama wa mbuzi
 
Ni vema na ni haki yake.

Lkn siasa za upinzani zimemuacha uchi Membe na zimetuwezesha kujua kuwa kumbe alibebwa na mfumo tu. Hana lolote na Wala siyo chochote.

Membe ni hawezi kujenga hoja kabisa. Hana mvuto na anaongea kike.
Tatizo kubwa ni ulafi wa madaraka, hawa jamaa walijiona wao ndio special kuweza kuongoza taifa hili. Am just curious Tanzania tunaweza kuwa na dynasties zinazotoa viongozi zaidi ya sehemu zingine
 
Kuna wachambuzi wanadai ni kawaida duniani kote. Wanatolea mfano Kenya, DRC na USA,
 
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, leo amekabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Shaka Hamdu Shaka, makabidhiano hayo yamefanyika Chiponda mkoani Lindi..

Awali Membe alifukuzwa uanachama na chama chake na kisha kujiunga na chama cha ACT Wazalendo na aligombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. ambapo kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, mnamo Machi 31 mwaka huu kilitangaza kumsamehe na kumrudishia uanachama wake baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha.

Membe amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na wanachama wengine zaidi ya 1,000 wa vyama vya upinzani waliorejesha kadi katika mkutano huo.

Membe Arejeshewa kadi yake ya CCM kilichobakia sasa ni kumpatia ubunge wa viti maalum then Apewe uwaziri.​

Nimesema uongozi ndugu zangu?​

Similar Discussions

Back
Top Bottom