Membe akalia bilioni 200 za Zanzibar

Membe akalia bilioni 200 za Zanzibar

halafu neno MEMBE-laanatu llah limekujaje kwenye lalamiko lao?wasitake kuuchafua uislam kwa uroho wao wa madaraka na fedha.Nani amewapa RUKHSA kumtaja ALLAH bila nidhamu?wasilete personal attack zao,serikali visiwani na bara inaongozwa na ccm,kwanini hawazungumzi mambo haya kwenye vikao vya chama kama serkalini hakuna ufumbuzi?sidhani kama MEMBE anakalia pesa zao,hizo ni za Muungano na kama zimekuja kwaajili ya znz zitaenda tu.
 
Kwanza habari za mzalendo ni majungu.

cc. JokaKuu Jasusi FJM Nonda Mchambuzi Mzee Mwanakijiji

Asante mkuu ilikua niandike haya haya. jamaa kweli ni wavivu wa kufikiri na kudhihirisha hilo ni pale wasikiapo Jussa, Moyo na wale wakereketwa wao wakisema jambo wao huamini papo hapo na kamwe hawatumii akili zao kuyatafakari. Kweli wajinga ndio waliwao. poleni zenu enendeni baharini mkavue kibua mpunguze njaa yenu
 
Membe hawezi kwa makusudi kukataa kusign kama hana maelekezo mengineyo
Sikuona umuhimu wowote wa habari kama hii kuwa public....labda kama walioileta wanayao ya sirini kuhusu muungano
 
Leo watu wetu wamefukuzwa zantel wangapi? Rushwa imeifanya kampuni ya zantel kufilisika na itakufa kama inavyokufa nchi ya znz, wallah nakupeni kwa ufupi, kampuni ya zantel ilikuwa na ubia wa WARABU, WAHINDI NA SERIKALI YA ZNZ, WAHINDI WAKATAKA KUIPELEKA ZANTEL TANGANYIKA, WAARABU NA SERIKALI YA ZNZ WAKAKATAA, WAHINDI WAKASEMA TUPIGENI KURA YA MAONI ATAKAESHINDA NDIO ATAFUATWA, WAHINDI WAKAJUWA TUTASHINDWA, BASI WALILOLIFANYA WAHINDI WAKAWAFATA WALE BODI MEMBERS WA SERIKALI YA ZNZ WAKAWAPA RUSHWA KUBWA TU ILI WAUNGE MKONO ZANTEL KUHAMIA DAR, MWISHO WA SIKU KUPIGWA KURA MWARABU ANASEMA NO, WAHINDI NA SERIKALI YA ZNZ WAKASEMA YES, HATIMA YAKE ZANTEL HIYO DAR, NA DAR WANAOIMALIZA ZANZTEL NI TIGO, AIRTEL, VODACOM, WANAWAHONGA WAFANYAKAZI WA KIBONGO KUIYUWA MITAMBO KWA MAKUSUDI ILI KAMPUNI IFE NA ITAKUFA KWA TAARIFA YENU, TUMELALAAAAAA, WATU WANAKWENDA MBELE, UKISEMA UNAITWA CUF, MUWAMSHO, AKILI HATUNA, WALA MIPANGO, SISI TUPO KWENYE SIASA TU, WATU WANAJENGA NCHI ZAO SISI TUPO NA FITNA, HASADA, WAJINGWA WAKUBWA.

Ningependa kucomments hili la zantel na hayo mengine sina comments
Zantel kuhamia bara ilikua ni sababu za kimkakati na kibiashara zaidi kwani soko la ZNZ lilikua limekaribia ukomo wake.
Hii hutokea kwa operator duniani kote ndio maana hata etisalat dubai wanafocus kwny kukuza na kuanzisha masoko mapya. Kwa ujumla unavyokua na mtandao mpana zaidi na wateja wengi zaidi una nafasi bora ya kuwin market na kuongeza faida.
Kwa mikakati ya Zantel baada ya kuhamia bara ilikua mizuri sna na endelevu ila menejiment wanaendesha biashara kiundugu/kujuana na kidini dini huku wakisahau biashara ni professional na hivyo kukiuka miiko.Ni kawaida Zantel kuanzisha huduma mpya mfano m-commerce, wireless internet ambazo zinabamba sana sokoni ila washindani wanakuja kuwazidi kete mfano m-pesa,tigo pesa nk. WHY ni upuuzi wa management yao.

Si kwel technical walikua wanahujum mitambo bali network ilikua imesimama 99% tatizo la hiyo kamapuni ni kutokufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi. Kitendawili kinabakia MENEJIMENTI ILIKUA INAFANYA HIVYO KWA MANUFAA YA NANI?
 
Mkuu Nguruvi3 umeandika vyema kabisa kuhusu masuala yaliyoibuliwa. Kuhusu kukalia fedha, Mimi napata taabu kuelewa huyu aliyeandika huko mzalendo. net anakusudia nini hasa. Nijuavyo masuala ya mikopo au misaada ya aina hii yanashughulikiwa na wizara ya fedha/ hazina (masuala ya muungano) na yale ya zanzibar kuna ya uchumi na fedha. Sijaelewa vizuri Membe ameingiaje hapa labda afafanue. Hata kama Membe kama waziri wa mambo ya nje angekasimiwa mamlaka ya kusaini kwa niaba ya hazina sioni sababu na mantiki ya kuzikalia kwani pesa hizo hazitolewi mkononi. Nina wasiwasi, huenda huyu mtu ana chuki binafsi na hawa viongozi wa wizara ya mambo ya nje kwani mbali ya Membe amemvaa naibu waziri Mahadhi kwa mambo ya uzinzi. Leo nimeamini, ni kweli busara ya baadhi ya watu huonekana wanapokuwa kimya. Basi maadam mwenzetu huyu hakukaa kimya ndo hivyo tena.
 
Hoja kama hizi mimi huwa nashindwa kujua undani wake make hazina upande wa pili uanweza kumhukumu mtu ukamuonea bure.

Itakuchukuwa muda sana kuelewa kwa sababu ya Muono na Mtazamo wako. Hii ni taarifa fanyia kazi kama Critical Thinker. Ila ukimsoma betweeni lines utagundua ana Logic na Truth in him/her
 
Mkuu Nguruvi3 umeandika vyema kabisa kuhusu masuala yaliyoibuliwa. Kuhusu kukalia fedha, Mimi napata taabu kuelewa huyu aliyeandika huko mzalendo. net anakusudia nini hasa. Nijuavyo masuala ya mikopo au misaada ya aina hii yanashughulikiwa na wizara ya fedha/ hazina (masuala ya muungano) na yale ya zanzibar kuna ya uchumi na fedha. Sijaelewa vizuri Membe ameingiaje hapa labda afafanue. Hata kama Membe kama waziri wa mambo ya nje angekasimiwa mamlaka ya kusaini kwa niaba ya hazina sioni sababu na mantiki ya kuzikalia kwani pesa hizo hazitolewi mkononi. Nina wasiwasi, huenda huyu mtu ana chuki binafsi na hawa viongozi wa wizara ya mambo ya nje kwani mbali ya Membe amemvaa naibu waziri Mahadhi kwa mambo ya uzinzi. Leo nimeamini, ni kweli busara ya baadhi ya watu huonekana wanapokuwa kimya. Basi maadam mwenzetu huyu hakukaa kimya ndo hivyo tena.

Utaratibu wa Kupata Fedha Zanzibar na Wizara ya Fedha kuingia unaanzia mara fedha inapokuwa imeingia Hazina. Membe anahusika kwa maana ya kukubali hiyo Activity ambayo kwa ajili yake fedha imeombwa. Unaposaini kukubali hiyo shughuli maana yake ni Pamoja na kiasi cha kutekeleza Kazi yenyewe. Ndo mikataba mingi ya Kiserikali ilivyo. Hapo sio Cheque eti amekataa kusaini. Akikataa kusaini maana yake hataki Hiyo shughuli ifanyike. Huo ndio Utaratibu
 
Kwanza habari za mzalendo ni majungu.
Pili, elimu ya mzalendo.net ni majunguTatu, elimu ya wznz kusoma na kutafuta ukweli ni ndogo.
Naonyesha uongo wa huyu bwana.

1.Membe amewanyima wazanzibar Visa kuhuduhuria vikao vya kimataifa kwa kuwanyima VISA
Wazanzibar visa ya nchi nyingine haitolewi na wizara ya mambo ya nje ya Tanzania.
Kama unakwenda US visa inatolewa na ubalozi wa US kama itakavyokuwa kwa visa ya UK, China n.k.
Kauli hii ni ya uongo na ni wajinga tu, narudi wajinga tu watakaokubali.Ni kauli ya kupuuza sana.
Membe hawezi kutoa visa ya Marekani. Wznz wanaafiki, uwezo wa kupambanua pumba na mchele mhh

2. Wanasema mambo ya nje yaondolewe katika muungano.
Hapa ni kuwa wanataka muungano lakini hawataki mambo ya nje yawe ya muungano.
Halafu anasema znz imeonyonywa na Tanganyika kwa miaka 48 wakati huo huo anataka muungano isipokuwa mambo ya nje.

Wazanzibar kataeni mambo ya nje yasiwe ya muungano, na msiishie hapo kataeni ulinzi na mambo ya ndani pia yasiwe ya muungao. Mkikubali kupewa ulinzi basi mjue na mambo ya nje yatakuwa ya muungano.
Hakuna nusu glasi.
Ulinzi na usalama hamzungumzii kwasababu mnajua ni suala la gharama, ndio utamaduni wa wenzetu, kubebwa rahaaaa mustarehe!

3. Hizi habari za Membe kukalia bilioni 200 zimekuja mwezi mmoja tu na ndio maana BLW wamejawa na ghadhabu na jazba

Huu ni uongo, hawana jazba wala ghadhabu wanafoka tu kwasababu wapo znz wakipanda meli kimyaa!
Juzi walikuwa Dodoma hakuna aliyenyanyua mdomo kusema leo ghadhabu inatoka wapi.
Ukumbi wa bunge la katiba unaandaliwa na wao wameomba idadi iongozwe, ghadhabu za muungano zitoke wapi!

4. Ushirikiano wa kimataifa umeingizwa baada ya sakata la OIC
Hapa ndipo utashangaa kuona wznz wanakubaliana na hili.
Hakuna anayekwenda maktaba kufanya hata kautafiti kasikohitaji fedha

Sakata la OIC limetokea miaka ya 1990 Mwinyi akiwa rais wa JMT.
Katika historia ya nchi hii kwa miaka 48 znz haijawahi kuwa na waziri wa mambo ya nje pekee.
Narudia pekee kwa maana kuwa hatujawahi kuwa na mawaziri wawili.

Kwahiyo suala la mambo ya nje lilikuwepo kuanzia mwaka 1964 kwasababu nilizosema.
Sijui hawa wenzetu uongo wanautoa wapi yarabi. Hata hili la miaka 20 linahitaji elimu kweli?

cc. JokaKuu Jasusi FJM Nonda Mchambuzi Mzee Mwanakijiji

Kama kawaida yako Bwa, Muabudu Nyerere....

Tafuta watoto wa chekechea uwafundishe hiyo elimu yako ya Muungano. Sisi hutupati na tunajua ni kinaendelea. Siku za Muungano zinahesabika.
 
Nafikiri (kama habari hi ni ya kweli) Membe ame act kizalendo kabisa, hizo pesa kama zinataka sihihi ya waziri wa mambo ya nchi za nje maanake hata mlipaji atakua Tanzania na sio zanzibar, kumbuka tukio la meli iliokamatwa na tani za Bangi/Bange kule Italy, jumuia ya kimataifa inasema meli ilikua ya Tanzania, hapa Bongo tunajua ile meli ni ya zanzibar, meli nyingi za Zanzibar zimeisha thibitishwa kua ni mbovu sana na gatari kwa usafiri wa majini, ikigwa penalt kwa kosa hilo kimataifa, mlipaji hua Tanzania na sio zanzibar hata kama zanzibar ndio walioiidhinisha kuwepo, big up Bernard Membe kwa hilo, wamezoea kubebwa kial siku hawa!
 
Hao machogo wanatuibia hata umeme wanaotuuzia ,walishitukiwa wanaugida halafu bonge la bili,ila sasa mita imewekwa kule Zenji ,waliposikia Pemba kuna mafuta wakapeleka umeme(ingawa gharama zimetolewa na SMZ) ,Ila kwa muda mrefu sana walikuwa wagumu.
 
Kama kawaida yako Bwa, Muabudu Nyerere....

Tafuta watoto wa chekechea uwafundishe hiyo elimu yako ya Muungano. Sisi hutupati na tunajua ni kinaendelea. Siku za Muungano zinahesabika.
Tena ningependa huo muungano uishe hata leo.

Tunachokataa hapa ni elimu ya ujinga. Hivi wznz kweli wanaamini kuwa waziri Membe ndiye anatoa visa za kusafiria nchi za nje?

Pili, wznz wanaamini kuwa walikuwa na waziri wa mambo ya nje hadi miaka ya 9o wakati wa sakata la OIC.

Wznz ndugu zangu tatizo ni lenu si muungano, fikirieni kuhusu elimu. Kama mnaweza kudanganywa kitoto na kukaa mnajadili ujinga wa namna hiyo, tatizo ni kubwa.

Wasome kabisa wapo katika mtandao wanadanganya mchana bila haya wala soni.
Huyu Salim ni mmoja wa key opinion leader kule znz, sasa fikiria mvua samaki yu hali gani.

Ushirikiano wa Kimataifa uliingizwa kwenye Muungano baada ya Zanzibar kutaka kujiunga OIC? Nani alikuwa Waziri wa mambo ya nje (Kimataifa) wa Zanzaibar wakati inajiunga na OIC, na uwaziri wake ulikoma lini? Hivi vituko vitaisha lini?

Wazanzibari wanalalamika sana kuhusu kunyonya na kutaka waachwe wapumue, lakini inashangaza hakuna mtu anayetamka wazi wazi Muungano uvunjwe, kwanini? Kwa nini hawawapigi marufuku wabunge wao wasipande boti kuja kwa 'wanyonyaji?
Ha ha ha! FJM wao hawataki muungano, lakini pia hawataki kusimama wenyewe. Woga wakubwa sana hawa!

Kila siku wanataka mkataba, hivi kuna mkataba gani na znz utakaoisaidia Tanganyika.
Mkataba wanaoutaka ni wa kusadiwa, huo si mkataba huo ni msaada.
Sasa wanaposaidiwa na kupiga mayowe hovyo unakuwa si msaada ni ukupe.

Badala ya kuungana kupinga muungano unaowanyonya wameungana kupata wajumbe wengi wa kuja Dodoma katika bunge la katiba. Wameshindwa kukataa hatua za mwanzo za rasimu wamebaki na kelele kila uchao.

Inachekesha msomi kweli kweli anadai kulikuwa na waziri wa mambo ya nje ya znz.
Yote hiyo ni kutaka kuwatia hasira wznz kwamba OIC ndio sababu ya kuondolewa waziri wao (Ghost minister).
Huyo anayefanya hivyo anajua kuwa katika wznz 10 lazima atawapata 9.

Wanasema Membe anatoa visa za nje na amewabania wznz waishiriki katika mikuatano.
Wapo watu wanaamini kabisa uzuzu huu. Aliyeandika anajua kuwa katika wznz 10 ataondoka na 10.
Siamini kama wznz hawajui visa ina utaratibu gani na hao mzalendo.net hawana hata aibu kuweka kituko hicho mtandaoni. Ni dhalili wznz mchague nini cha kusema na kuweka mitandaoni. Mnaonekana wa ajabu sana

Hivi kwanini Membe azuie bilioni 200 na asiende kudai bilioni za umeme wa bure.
Bilioni 200 ni pesa kidogo sana Tanganyika huko kwao ni pato la mwaka mzima kwahiyo wanahisi wameibiwa.
Na hakuna sababu za Membe kuzuia hilo, sasa kama wanataka kujikomboa wakatae muungano.

Hii habari ya kutaka mkataba wa kulindiwa kisiwa aa1 tunasema tukiwapa ulinzi you must pay the price.
Mkitaka muungano muwe tayari kuchangia, hamuwezi tulieni mgongoni tutawapa chupa za maziwa

Tuacheni tupumue jamani, miaka 48 mgongo unapindai!

Maalim Nonda vipi VISA inatolewa na Membe? GHIBUU Waziri wa mambo ya nje wznz kabla ya 1990 alikuwa nani?

  • Thanks
Reactions: FJM
Kwanza habari za mzalendo ni majungu.
Pili, elimu ya mzalendo.net ni majunguTatu, elimu ya wznz kusoma na kutafuta ukweli ni ndogo.
Naonyesha uongo wa huyu bwana.

1.Membe amewanyima wazanzibar Visa kuhuduhuria vikao vya kimataifa kwa kuwanyima VISA
Wazanzibar visa ya nchi nyingine haitolewi na wizara ya mambo ya nje ya Tanzania.
Kama unakwenda US visa inatolewa na ubalozi wa US kama itakavyokuwa kwa visa ya UK, China n.k.
Kauli hii ni ya uongo na ni wajinga tu, narudi wajinga tu watakaokubali.Ni kauli ya kupuuza sana.
Membe hawezi kutoa visa ya Marekani. Wznz wanaafiki, uwezo wa kupambanua pumba na mchele mhh

2. Wanasema mambo ya nje yaondolewe katika muungano.
Hapa ni kuwa wanataka muungano lakini hawataki mambo ya nje yawe ya muungano.
Halafu anasema znz imeonyonywa na Tanganyika kwa miaka 48 wakati huo huo anataka muungano isipokuwa mambo ya nje.

Wazanzibar kataeni mambo ya nje yasiwe ya muungano, na msiishie hapo kataeni ulinzi na mambo ya ndani pia yasiwe ya muungao. Mkikubali kupewa ulinzi basi mjue na mambo ya nje yatakuwa ya muungano.
Hakuna nusu glasi.
Ulinzi na usalama hamzungumzii kwasababu mnajua ni suala la gharama, ndio utamaduni wa wenzetu, kubebwa rahaaaa mustarehe!

3. Hizi habari za Membe kukalia bilioni 200 zimekuja mwezi mmoja tu na ndio maana BLW wamejawa na ghadhabu na jazba

Huu ni uongo, hawana jazba wala ghadhabu wanafoka tu kwasababu wapo znz wakipanda meli kimyaa!
Juzi walikuwa Dodoma hakuna aliyenyanyua mdomo kusema leo ghadhabu inatoka wapi.
Ukumbi wa bunge la katiba unaandaliwa na wao wameomba idadi iongozwe, ghadhabu za muungano zitoke wapi!

4. Ushirikiano wa kimataifa umeingizwa baada ya sakata la OIC
Hapa ndipo utashangaa kuona wznz wanakubaliana na hili.
Hakuna anayekwenda maktaba kufanya hata kautafiti kasikohitaji fedha

Sakata la OIC limetokea miaka ya 1990 Mwinyi akiwa rais wa JMT.
Katika historia ya nchi hii kwa miaka 48 znz haijawahi kuwa na waziri wa mambo ya nje pekee.
Narudia pekee kwa maana kuwa hatujawahi kuwa na mawaziri wawili.

Kwahiyo suala la mambo ya nje lilikuwepo kuanzia mwaka 1964 kwasababu nilizosema.
Sijui hawa wenzetu uongo wanautoa wapi yarabi. Hata hili la miaka 20 linahitaji elimu kweli?

cc. JokaKuu Jasusi FJM Nonda Mchambuzi Mzee Mwanakijiji

Umefanya uchambuzi mzuri Nguruvi.......mimi naomba nikuongezee point moja ya msingi inayoonyesha habari hii ya Membe kukalia pesa za wazanzibari sio ya kweli.

1) Masuala ya Mikopo na Misaada kutoka Nje yanashughulikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

2) Sheria ya Mikopo na Misaada ya mwaka 1974 na kufanyika marekebisho mwaka 2003 (THE GOVERNMENTS LOANS, GUARANTEES AND GRANTS ACT, 1974 AMALGAMATED WITH THE GOVERNMENTS LOANS, GUARANTEES AND GRANTS (AMENDMENT) ACT, 2003 inatamka wazi kwamba Waziri wa Fedha ndiye mwenye mamlaka ya kuchukua mikopo na kupokea misaada kwa niaba ya Nchi.

3) Katika Sheria hiyo hiyo Sehemu ya 5, kifungu cha 15(1) inaeleza wazi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inao uwezo kisheria kupokea Msaada moja kwa moja bila kusubiria Waziri wa Fedha

kwa mantiki hiyo, hii habari ya Membe kukalia msaada wa Zanzibar si ya kweli kwasababu kisheria Waziri wa Mambo ya Nje hana mamlaka wala wajibu wa kushughulika na mikopo na misaada. Nionavyo mimi, waliotengeneza story hii ni wale maadui zake kisiasa wakitaka kumchonganisha na Wazanzibari katika agenda zao za 2015.
 
Mbona umempa Mh.Membe majukumu ambayo hata si yake ndugu yangu......Membe akutafutie Visa?!!!! Jamani muwe mnashughulisha vichwa kidogo
 
Wazanzibari ndio hao wanalalamika, faida hawaioni wanachokiona ni hasara tu. Kama na sisi hatuna faida nao na una hasara tu kwanini tuung'ang'anie?

Kama inabidi uwepo, Serikali tatu. Kila mtu awe huru kufanya maamuzi yake.

Kila mmoja anatamani iwe hivyo lakini bado kibali hakijapatikana kutoka sehemu moja tu, ndio yenye pengo.
 
Back
Top Bottom