Membe 'aitesa' CCM, wanachama wajipanga 'kumrudisha' chamani kwa namna yoyote

Hiyo ni ngojera na mambo ya vijiweni, kudanganya kwingiii!

Nje ya CCM, kiongozi nchini ni sawa na samaki nje ya maji.

Asingefukuzwa angekuwa na kiasi fulani cha nguvu ya ushawishi. Maadam amefukuzwa kwenye chama ni yeye binafsi anaweza kuomba msamaha kupitia vikao husika vya chama.
 
Hapa sio ishu ya umaarufu bali ni mahitaji ya nyakati, halafu kumbuka Membe sio Lowassa japo wote ni makada maarufu..

Jr
Do you think that will ever happen in CCM? Lakini sio vibaya kuzipooza nafsi. Kufikiria ni kitu chema hata kama tunachofikiri hakitakaa kuja kutokea tukiwa hai
 
Bavicha mchukueni Membe,tumeshamalizana nae
Mlisema tunamuogopa,niguse ninuke,sasa mmekuja na hekaya za kurudishwa
Kurudishwa chamani sio sawa na kumpeleka mke kwa mumewe
 
Katika hali ya kushangaza na kushtua, aliyekuwa kada wa CCM Benard Membe bado ameendelea kuwa mwiba mkali ndani ya CCM kwa kugawanya makada ndani ya CCM. Membe ameendelea kutajwatajwa kwenye vikao vya kichama na kati ya makada binafsi pamoja na kufukuzwa kwake ndani ya CCM.

Membe anatajwa chamani kama kiungo muhimu wa Umoja, mshikamano na maridhiano ndani ya chama na karata muhimu ya CCM kwa siasa za Kusini. Makada waandamizi ndani ya CCM wanapishana na kutofautiana (kama walivyopishana na kutofautiana Wajumbe wa Kamati ya Maadili) kuhusu adhabu aliyopewa Membe ya kufukuzwa uanachama.

Benard Membe alifanya mazungumzo na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM chini ya Komredi Mangula jijini Dodoma na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM na Kamati Kuu ya Taifa ya CCM iliyo chini ya Dr. J.P. Magufuli. Tangu afukuzwe uanachama, Membe amekuwa kimya na ukimwa wake unaumiza viongozi na wanachama wa CCM.

Katika kuchagiza kutofautiana kwa msimamo baina ya makada waandamizi wa CCM, makada maarufu wamejipanga kuhakikisha kuwa Membe anarejea CCM kwa namna yoyote ile. Tayari nyaraka mbalimbali za kichama zimeshaandaliwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka mbalimbali chamani kufanikisha mpango huo. Mambo yanaanza kunoga chamani.

Tuwe makini na ugonjwa wa Corona!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)
Membe tulishamng'oa meno na kumkata mkia. Hana tena ubavu wa kumsumbua mlala kwenye mawe
 
Hapa sio ishu ya umaarufu bali ni mahitaji ya nyakati, halafu kumbuka Membe sio Lowassa japo wote ni makada maarufu..

Jr
Ila Lowasa alikuwa na ushawishi kumzidi Membe. Afterall Membe simuoni kama anauweza huo urais
 
Hapa sio ishu ya umaarufu bali ni mahitaji ya nyakati, halafu kumbuka Membe sio Lowassa japo wote ni makada maarufu..

Jr
Membe ni dhaifu. Kwanza alivuruga sana chama. Ukitaka kujua nguvu ya Lowasa ni kuwa hata mwenyekiti jk alipotaka kumbeba Membe kwenye kura za maoni bado alifeli.
Membe hata ukienda Rondo hawamkubali wanamuona kama mtu wa kuja tu.
Alihisi chama ni chake na aliamini ana nguvu baada ya jk. Yeyote aliyetofautiana nae alitupwa benchi. Ni yeye ndii alitangaza kuwa na maadui na iwapo angeshinda urais hao maadui wake sita wangehama nchi.
Jiulize Membe na Lowasa + Rostam nani wana base ndani ya ccm. Ndio utapata jibu mzee mshana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakimrudisha watakuwa wamemjenga sana kisiasa na hilo nadhani ndiyo linawatesa sana. Membe naye amecheza karata zake vizuri kwa kutokurupuka na kufanya maamuzi yoyote huenda waliomfukuza walitegemea ataenda upinzani ila kwa kukaa kimya na kutoonyesha move yoyote inawatesa sana.
Muda bado. Kwa sasa gazeti la Chadema Tanzania daima bado liko bize kumuuza kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pigeni kelele za kipumbavu alafu muda unakwenda mbio. October mkipigwa za uso muanze kulialia mara tume haikuwa huru,mara polisi waliiba kura, mara mlivunjwa mikono hamuwezi kuandika.
Wenzenu tayari walisha maliza maana siku hizi ni vitendo tu,vituo vya afya 400+,hospital za wilaya 60+,Sgr,JNHHP n.k
Nyinyi mmebaki na ngonjera za kishamba.
Ccm itaondoka madaraka siku corona ikituondolea watu wenye akili Kama hizi
 
Watanzania tumezidi ushabiki mpaka tumepitiliza.

1. Hivi wewe tupatupa unakumbuka wakati wa kila duka mjini jereta linaunguruma mbele yake? Watu walifanya biashara ya mafuta na majereta. TANESCO ilichezewa na wakubwa, waliunda makampuni kuiuzia umeme TANESCO, hivi hawa wanaoutaka uraisi hawakuwa sehemu ya hayo mambo? Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi

2. Hivi unakumbuka kipindi wamachinga na mama ntilie wanafukuzwa mitaani na migambo kama wakimbizi kwenye nchi yao? Mimi nakumbuka kipindi hicho ndugu yangu, binadamu wenzetu watafutaji walionekana kama uchafu katika nchi yao wenyewe.
Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi

3. Unakumbuka ajali za barabarani kipindi ambacho kampuni za mabasi na maloli yanamilikiwa na wakubwa? Polisi trafiki hakuwa na sauti kwa madereva, walimjibu wanavyotaka, bila kujali nafasi yake. Ajali za barabarani zilichinja watu tukasema kafara huku madereva wakiendesha magari na viloba mkononi. Unakumbuka?
Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi.

4. Unakumbuka kipindi madawa ya kulevya yalipouzwa kama karanga. Sio ninyi wenyewe mliotuambia mtoto wa mkubwa amekamatwa China ndiyo maana tunalipa gesi mtwara? Sio ninyi na karamu zenu? Kwa mini mnatumia karamu kufanya biashara?
Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi.

5. Unakumbuka wakubwa walivyogawana maeneo kila mahali hekali kwa hekali bila kujali wengine wataishi wapi, mwishoni walitaka mpaka kuuza koko bichi bahati nzuri watu wa Mungu wakaikomboa. Leo watanzania hatuna hofu mbele ya wenyewe pesa.
Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi.

6. Unakumbuka jinsi watu walivyoichezea bandari, mafuta yalipitishwa katika mifumo ya wizi bila kulipia kodi. Hawa ndio unaowashabikia? Haya tupatupa endelea na Lumumba yako.
Ngoja niishie hapa kwa ufupi hatutaki turudi huko.
Acheni uchawi mwacheni Magufuli afanye kazi.
 
Mnalazimisha kuipiku corona ?,huyo Kama ni mwamba apambane nje ya1 ccm ndio nitamkubali ,na hawezi,ajiandae kufa kibudu tu,hakuna namna
Katika hali ya kushangaza na kushtua, aliyekuwa kada wa CCM Benard Membe bado ameendelea kuwa mwiba mkali ndani ya CCM kwa kugawanya makada ndani ya CCM. Membe ameendelea kutajwatajwa kwenye vikao vya kichama na kati ya makada binafsi pamoja na kufukuzwa kwake ndani ya CCM.

Membe anatajwa chamani kama kiungo muhimu wa Umoja, mshikamano na maridhiano ndani ya chama na karata muhimu ya CCM kwa siasa za Kusini. Makada waandamizi ndani ya CCM wanapishana na kutofautiana (kama walivyopishana na kutofautiana Wajumbe wa Kamati ya Maadili) kuhusu adhabu aliyopewa Membe ya kufukuzwa uanachama.

Benard Membe alifanya mazungumzo na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM chini ya Komredi Mangula jijini Dodoma na baadaye kufukuzwa uanachama wa CCM na Kamati Kuu ya Taifa ya CCM iliyo chini ya Dr. J.P. Magufuli. Tangu afukuzwe uanachama, Membe amekuwa kimya na ukimwa wake unaumiza viongozi na wanachama wa CCM.

Katika kuchagiza kutofautiana kwa msimamo baina ya makada waandamizi wa CCM, makada maarufu wamejipanga kuhakikisha kuwa Membe anarejea CCM kwa namna yoyote ile. Tayari nyaraka mbalimbali za kichama zimeshaandaliwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka mbalimbali chamani kufanikisha mpango huo. Mambo yanaanza kunoga chamani.

Tuwe makini na ugonjwa wa Corona!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishatupiwa virago na ushawishi wako unaishia hapo tena hizi zama za kudukuana mawasiliano hata Nape sidhani kama anawasiliana nae hata salamu tu.

Huyo ukurasa wake umeshafungwa rasmi ndani ya CCM labda kama lengo ni kupiga porojo tu.
 
Back
Top Bottom