Meli mpya nyingine yaja

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Meli mpya ya kisasa inayoundwa katika bandari ya Itungi Kyela ipo katika hatua za mwisho kukamilika ambapo itarahisisha safari za Kyela, Songea, Mbinga, Njombe na Malawi kupitia Ziwa Nyasa
FB_IMG_1552383088135.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mashujaa wa mbele ya laptop wanaoishi Dar, wanakwambia hakuna chochote ambacho awamu ya tano imeshakifanya mpaka leo hii.

Mkuu siasa zimekuathiri sana, Kazi ya serikali ni kutenda na isipotenda lazima ilaumiwe. Usiumie sana unapoambiwa hakuna kilichofanyika safari bado ni ndefu hivyo hatupaswi kujisifia kwa hivi vitu vidogo vidogo, Wanaosema hakuna kilichofanyika wako sawa maana matatizo ni mengi kuliko vilivyofanyika ila kama vilivyofanyika vingekuwa vingi kuliko matatizo usingesikia kelele maana wengi wangekuwa wamefikiwa.. Madawa, Elimu, Miundombinu hizo bado ni basics mkuu tunafanya karne hii.
 
eti ya kisasa😜 mbona ni ya kawaida sana haina tofauti na mV kazi
 
Tafuta kazi ufanye uingize pato, ukiwa mvivu kila rais utamuona hafai, kila awamu utaiona mbaya.
MIAKA YA NYUMA TULIZOEA HOJA ZA WAPINZANI KUJIBIWA KWA HOJA ZENYE MASHIKO NA KINA NAPE NA KINANA, ILA SASA HOJA ZA WAPINZANI ZINAJIBIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI NA POLISI
 
MIAKA YA NYUMA TULIZOEA HOJA ZA WAPINZANI KUJIBIWA KWA HOJA ZENYE MASHIKO NA KINA NAPE NA KINANA, ILA SASA HOJA ZA WAPINZANI ZINAJIBIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI NA POLISI
Pengine ni msaliti wa taifa lake, anawasaliti watu milioni 55 na maslahi yao ndio maana risasi zinamfaa zaidi.
 
Back
Top Bottom