zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,156
- 28,895
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.
Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni
UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.
Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.
Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki
Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??
Je huyu melchizedek ni nani hasa?
UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???
Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!
Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.
Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.
HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.
Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??
Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??
Je historia yake ni ipi??
Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?
Karibuni....