Je, Dunia ni battle field ya UJASUSI kati ya ufalme wa Nuru vs ufalme wa Giza?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,638
25,213
Salaam shalom!!

Maandiko yanasema vita na uasi ulitokea Mbinguni, ndipo Dunia ikaumbwa tukaletwa hapa Kisha shetani pia akatupwa huku tulipo Ili vita iendelee,

Tafsiri hapo ni kuwa, battle ground ya vita ilihamishiwa duniani, sasa twende mbele kujua mambo kadhaa wa kadhaa.

Mifumo yote ya kiuongozi, kiutawala, kiuchumi, kisiasa ni copy and paste Toka Ulimwengu usioonekana.

Kitabu kiitwacho BIBLIA, NENO la Mungu, ni kitabu chenye codes nyingi sana za kijasusi kati ya falme kuu mbili , Ufalme wa Giza na Ufalme wa Nuru.

Tupitie cases ZIFUATAZO;

CASE NO 1.

( Mwanzo 14:18-20).(Hebrews 7:1...)
Ibrahim anampa ZAKA mtu aitwaye MELKIZEDEK, Huyu anaitwa Mfalme wa Salem, na Ufalme wa huyu MELKIZEDEK ni mfalme asiekuwa na mwisho, Hana baba Wala mama, pia ni kuhani.

Hiyo ni code muhimu kujua kuwa huyo alikuwa Si mtu au binadamu wa kawaida.

CASE NO 2.

(Isaya 14:13), (Mwanzo 3:4-5),(Mithali 16:18),( Zaburi 9:20),(Ezekiel 28:1-19).
Anaibuka mtu na kutawala Nchi iitwayo TIRO, Ameandikwa alikuwa na HEKIMA kumzidi Danieli, wakati maandiko yatuambia Daniel alikuwa anaweza Hadi kutuambia Jana uliota nini Kwa uwezo wa Mungu, Mfalme wa TIRO,alitumia HEKIMA zake Kupata utajiri mkubwa,alikuwa kerubi aliyeasi mbingu,Ukisoma vizuri sifa za mtu huyo, mfalme huyo, utagundua kuwa , hakuwa mtu au binadamu wa kawaida Bali alitoka SAYARI Ingine kabisa.

Na hapa Wafalme wengi wa Dunia huvamiwa na kujikuta wanampa huyo Shetani kukalia KITI bila kujua Kwa kujiinua na kutaka kujitukuza na kusifiwa. Ujasusi ukaendelea!!

CASE NO 3.

( Mwanzo 18:15-32).
Watu watatu wanamjia Ibrahim na kuongea naye,

Walipokwisha kula na kuondoka kuelekea Sodoma na Gomora, Cha kushangaza, walifika Sodoma na Gomora watu wawili, mtu wa tatu, haijulikani alipotelea wapi,
Hiyo itoshe tutupa kufahamu kuwa watu wale hawakuwa wa kawaida wa Ulimwengu huu.

CASE NO 4.

( Genesis chapter 1&2).
Uumbaji wa Mtu pia ni Siri kubwa, Kuna uwezekano pia mwanadamu, mtu asili yake Si katika Dunia hii,

Neno la Mungu lasema, na tuumbe mtu Kwa Mfano wetu, Kwa sura yetu.

Hilo pekee litupe kujua kuwa sisi pia Si wa kawaida.

CASE NO 5.

( Mathayo 17:1-13).
Elia anatwaliwa akiwa hai kwenda Mbinguni Kwa kutumia gari la farasi liwakalo moto.

Yohana mbatizaji anakatwa KICHWA, baadae Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa, ikiwa mnapenda kuamini, aminini kuwa Elia ndiye Yohana mbatizaji aliyekatwa KICHWA. Ujasusi ukaendelea, watu midomo wazi.

CASE NO 6.

( Mathew chapter 1&2).
Kuzaliwa Kwa Yesu. Maandiko yanataja Yesu katika uzao wa kifalme wa Daudi, na vizazi vinamtaja Yusuph mume wa Maria kama ndiye aliyemzaa Yesu, hapo hapo kumbe WANADAMU wameshapigwa tukio la kijasusi, kumbe Yusuph Si baba wa Damu na nyama wa Yesu, kumbe Yesu ni mtu Kutoka Mbinguni kabisa,

Hadi anapaa Mbinguni, ndipo watu wakaja kujua kuwa kumbe Mungu mwenyewe ndiye alikuja katika mwili wa mwanadamu.

CASE NO 7.

(Job: 1,2,3......)
Toto Tundu ( shetani) linajipitisha Kwa Mungu, Mungu analiuliza, je umemwona mtumishi wangu Ayoub?

Shetani asema, wapi, anakutii sababu umempa Kila kitu, utajiri, Mali ,watoto na umemzungushia ulinzi, ukiviondoa hivyo atakuasi,

Mungu anatoa Ruhusa Ayubu ajaribiwe bila hatankumshirikisha Ayubu, ghafula moto unashuka Toka Mbinguni , unashushwa na shetani na kutekeleza Mali za ayubu, majanga mfululizo yanamfuata.

Ndipo WANADAMU tujue hapa duniani, tunafanyiwa Ujasusi tena wakati mwingi Baba yetu Mungu anaruhusu tupitie magumu Ili aone kama tutaendelea kumtumaini.

CASE NO 8.

Mfalme Daudi a apata wazo kichwani mwake, anawaza ghafula kuwahesabu Wana wa Israel anaowaongoza, na anaita watu na kuwaagiza waanze KAZI ya sensa, Mungu anamkasirikia Daudi na kumwambia, haya Mawazo Wala Si yangu, Wala hayakutoka kichwani mwako, Bali ni Shetani ndiye aliyeleta wazo Hilo nawe umemtii.

Ndipo hapo tujue kuwa hata Mawazo yetu tusiyaamini, tuyapime, yaezakuwa ni Ujasusi wa kifikra tunafanyiwa.

Swali no 1.
Je Ujasusi huu ni Hadi lini?

Swali no 2.
Je, Unajitambua wewe u nani wewe na asili yako?

Swali no 3. Umeshawahi kufanyiwa tukio la kijasusi Kutoka watu wa SAYARI zingine iwe Nuru au Giza?

Karibuni 🙏
 
Salaam shalom!!

Mifumo yote ya kiuongozi, kiutawala, kiuchumi, kisiasa ni copy ana paste Toka Ulimwengu usioonekana.

Kitabu kiitwacho BIBLIA, NENO la Mungu, ni kitabu chenye codes nyingi sana za kijasusi kati ya falme kuu mbili , Ufalme wa Giza na Ufalme wa Nuru.

CASE NO 1.

( Mwanzo 14:18-20).
Ibrahim anampa ZAKA mtu aitwaye MELKIZEDEK, Huyu anaitwa Mfalme wa Salem, na Ufalme wa huyu MELKIZEDEK ni ufalme usiokuwa na mwisho.

Hiyo ni code muhimu kujua kuwa huyo alikuwa Si mtu au binadamu wa kawaida.

CASE NO 2.

( Ezekiel 28:1-19).
Anaibuka mtu na kutawala Nchi iitwayo TIRO, Ukisoma vizuri sifa za mtu huyo, mfalme huyo, utagundua kuwa , hakuwa mtu au binadamu wa kawaida, Bali alitoka SAYARI ingine kabisa.

CASE NO 3.

( Mwanzo 18:15-32).
Watu watatu wanamjia Ibrahim na kuongea naye,

Walipokwisha kula na kuondoka kuelekea Sodoma na Gomora, Cha kushangaza, walifika Sodoma na Gomora watu wawili, mtu wa tatu, haijulikani alipotelea wapi,
Hiyo itoshe tutupa kufahamu kuwa watu wale hawakuwa wa kawaida wa Ulimwengu huu.

CASE NO 4.

( Genesis chapter 1&2).
Uumbaji wa Mtu pia ni Siri kubwa, Kuna uwezekano pia mwanadamu, mtu asili yake Si katika Dunia hii,

Neno la Mungu lasema, na tuumbe mtu Kwa Mfano wetu.

Hilo pekee litupe kujua kuwa sisi pia Si wa kawaida.

CASE NO 5.

( Mathayo 17:1-13).
Elia anatwaliwa akiwa hai kwenda Mbinguni Kwa kutumia gari la farasi liwakalo moto.

Yohana mbatizaji anakatwa KICHWA, baadae Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa, ikiwa mnapenda kuamini, aminini kuwa Elia ndiye Yohana mbatizaji aliyekatwa KICHWA. Ujasusi ukaendelea, watu midomo wazi.

CASE NO 6.

( Mathew chapter 1&2).
Kuzaliwa Kwa Yesu. Maandiko yanataja Yesu katika uzao wa kifalme wa Daudi, na vizazi vinamtaja Yusuph mume wa Maria kama ndiye aliyemzaa Yesu, hapo hapo kumbe WANADAMU wameshapigwa tukio la kijasusi, kumbe Yusuph Si baba wa Damu na nyama wa Yesu, kumbe Yesu ni mtu Kutoka Mbinguni kabisa,

Hadi anapaa Mbinguni, ndipo watu wakaja kujua kuwa kumbe Mungu mwenyewe ndiye alikuja katika mwili wa mwanadamu.

Swali no 1.
Je Ujasusi huu ni Hadi lini?

Swali no 2.
Je, Unajitambua wewe u nani wewe na asili yako?

Swali no 3. Umeshawahi kufanyiwa tukio la kijasusi Kutoka watu wa SAYARI zingine iwe Nuru au Giza?

Karibuni 🙏
Vipi umewahi kujaribu kuwaza kwamba hizo zinaweza kuwa ni stori tuu kama hadithi nyingine za alfu lela ulela zisizo na ukweli wowote?
 
Hizi Code Ni ngumu Sana Rabboni Unawapa Jf hakuna atakaye kuelewa..

Tena kama Ukiwaambia Melchzedek hana Baba wala mama Hana mwanzo wala Mwisho!
Utawachanganya waumini wako..

Halafu yesu Ni mfano wa Melchzedek
Mada zangu nyingi ni za kijasusi Toka kule nilikotokea,

Lakini mods wanashindwa kufungua " codes" , Kisha wanazihamisha au kuziground😌
 
Vipi umewahi kujaribu kuwaza kwamba hizo zinaweza kuwa ni stori tuu kama hadithi nyingine za alfu lela ulela zisizo na ukweli wowote?
Hivyo hizo Si story,

Mifumo yote ya kuendesha Dunia hii IPO controlled Toka falme hizo kuu mbili.

Dig deep& open your eyes and see!!
 
Hizi Code Ni ngumu Sana Rabboni Unawapa Jf hakuna atakaye kuelewa..

Tena kama Ukiwaambia Melchzedek hana Baba wala mama Hana mwanzo wala Mwisho!
Utawachanganya waumini wako..

Halafu yesu Ni mfano wa Melchzedek
Hizi codes ziliwahi taka kunipasua KICHWA!!

Yaani ni mtu, halafu ni mfalme, Hana Baba Wala mama.

Ni mfalme, tena kuhani,

Ibrahim alipofungua "codes" za kijasusi akampa ZAKA nyingi sana.

Na hiyo ndiyo chanzo Cha ZAKA na utajiri wa Ibraham.

Leo Kuna watu wajinga wanadai Musa ndiye aliyeleta agizo la ZAKA.

Wanaamini Eti Imani pekee bila kulipa ZAKA yaweza kukupa utajiri.

Wanasahau, falme zote, NURU na GIZA, Hazina za gizani zilizofichwa,kuzipata, ni Hadi ulipe ZAKA!!

KAZI IPO😎
 
Hizi codes ziliwahi taka kunipasua KICHWA!!

Yaani ni mtu, halafu ni mfalme, Hana Baba Wala mama.

Ni mfalme, tena kuhani,

Ibrahim alipofungua "codes" za kijasusi akampa ZAKA nyingi sana.

Na hiyo ndiyo chanzo Cha ZAKA na utajiri wa Ibraham.

Leo Kuna watu wajinga wanadai Musa ndiye aliyeleta agizo la ZAKA.

Wanaamini Eti Imani pekee bila kulipa ZAKA yaweza kukupa utajiri.

Wanasahau, falme zote, NURU na GIZA, Hazina za gizani zilizofichwa ni Hadi ulipe ZAKA!!

KAZI IPO😎
Zaka imeanza kwa Ibrahimu ikatekelezwa na Yakobo Musa kaipata Kwa sababu Israel waliacha Kuifata Walipokuwa Misri
 
Dunia sio battlefield, ni GEREZA.

This prison is guarded by the CONQUERORS who conquered it in a cosmic Battle long ago, and WE ARE THEIR SLAVES AND PRISONERS.

This world was once FREE, but it was HIJACKED and CONQUERED.

There is no BATTLE. It was already fought and won.

Cc DR Mambo Jambo Rabbon
There is some truth to what you say--not exactly that way-- the way, you as a person put it...

The world as 'semi-isolated' realm of 'human experience'--true...

The world as a 'Prison'--Not really so...

The world 'being free' some time ago--this depends upon the 'depth of rational interpretation' pertaining to the notion of 'Being Free/Freedom'...

Being 'Hijacked' and 'Conquered'--not really the case...

Yes the Earth, as a planet from a certain space point of view, is being 'monitored' and 'nurtured'. All this within the viable possibilities -- capable of being both, 'good and/or bad terms'; thus depending upon one's comprehensible 'depth of rational interpretation'.

In overall, those who watch over the Earth, most of them--and with the military capability to intervene if the need occurs, do not really hold 'bad intentions' towards Earthly Affairs and Global Self Determination. However, there are independent 'verdants' in the 'cosmic ecology'. Those 'unwise' who can 'mingle' with Earthly Affairs for private interests and detrimental to 'the temporary Earth game'...

It is just one contextual matter pertaining to the 'exo-politics affairs'... There is a Cosmic 'United Nations' above for a certain 'good reason'; not necessarily 'infallible cause' accounting for 'the well beingness of Galactic Ecology'...

'Umoja wa Mataifa' uliyo Juu, na tena wenye kuyatupia macho masuala ya Dunia, mambo yake kuhusu uangalizi wake huo una mengi ambayo hapa Duniani watu hawajaandalika kuyafahamu--lakini sasa, 2024-2036, yanakwenda kufahamika na hakuna wa kuweza kulizuia hili tena.

Duniani, unayoyaona kama 'Umoja wa Mataifa'--harakati za kujenga 'Umoja' na 'Amani' Duniani ni mawazo yaliyoshawishika kutoka 'Juu'... Kwa upande wa mambo kutoka JUU, zipo kanuni zinazozuia 'Umoja wa Kimataifa wa Makabila/Mbari za Manyotani' kuingilia moja kwa moja masuala mbalimbali ya maisha duniani--huitwa >'Elekezo Primu'<.... Elekezo moja lisilo na mbadala kuheshimiwa.

Ni 'elekezo primu' ndilo kwa namna fulani linafanya kama 'maisha duniani' kuwa kama kifungo -- kifungo kwa kuwa yeyote anaweza kutafsiri kama: kumbe wapo 'wadau wenye mbavu' wanaoona kila kitu lakini 'wanakausha'--inakuwa aje?

Kuna mengi ya kuyafahamu na kuyaelewa ili kumalizana na shauri la kujibu 'mikausho ya wadau kutoka JUU'...

Kiukweli binadamu wote ni raia wa ulimwengu wote mzima--kuzaliwa na kuishi Duniani hakufanyi mtu kuwa wa Duniani peke yake--kana kwamba, hayuko kungine kokote...

Sisi wote ni 'Mbegu Nyota'--watu tunaoishi kama wanadamu lakini tunaishi na kungine pia japo fahamu zetu za kawaida zimefumbika macho...

Ni muktadha wa Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ndiyo 'itakayotuweka sawa'--kuja kufahamu haya yote na zaidi; hili ndilo hasa kiini cha Yesu kupata kusema "Tafuteni Ufalme wa Mbingu na Haki yake na mengine mtazidishiwa"...

Ufalme wa Mbingu uko ndani yetu, ni asili ya sisi kuwa huku na kule, jana-leo-na kesho... Kila mtu ana sehemu ya yeye yenye asili ya kutokufa--asili hii ndiyo fumbo la 'Uzima wa Milele'; Duniani, sehemu ya mchezo wa kuishi hapa, ni kuyasahau haya yote na kuanza 'kuhangaika na Dunia'...

Kwa kuwa humu JF, haya yanakuja kutokana na habari za vitabu vifanyavyo Biblia--kuna mengi yataanza kufahamika kuhusu habari za kwenye masimulizi ya Biblia--'kupanga na kupangua' yale yote umma wa wasomi, wadadisi na zaidi waumini umekuwa 'ukisadiki' ama 'kudhani' ni ukweli wa mambo kama vile inavyowasilishwa hapa na pale na kumbe sivyo hasa...

Watu wa JUU, wanaujuzi na utalaam wa mengi kupita hata kawaida tuliyoizoea hapa Duniani. Wanaweza kulala kwenye 'viambaza-mwili vya maji ama hewa' na halafu wakazaliwa Duniani kama watu, kuishi toka kuzaliwa hadi kufa; Ama wanaweza moja kwa moja 'Wakashuka' kama wanadamu na kuishi na wanadamu na tena kama wanadamu kwa muda unaowafaa wao na 'mipango yao'...

Hao wanaoweza kushuka moja kwa moja na kuishi na wanadamu ni wale wenye 'Miili na Mionekano' kama wanadamu; lakini huko JUU siyo kila kiumbe-mtu ni 'Mwanadamu'...

Duniani, historia ya 'Watu kutoka Juu' kushuka duniani na kuwa Miungu miongoni mwa wanadamu si habari ngeni... Watu hawa huitwa 'Miungu' ama hata 'Malaika'--pia 'Askari wa Jeshi la Mbinguni'...
ChurchAges.net - Swahili Union Version - 2 Wafalme 23
2 Wafalme 23:4

View: https://www.youtube.com/watch?v=fAvAQrDOE6k

Kuna namna basi, hata pamoja na uwepo wa 'Elekezo Primu'--mara kwa mara watu wa Juu hulivunja hilo na kuchangamana na watu wa Duniani; na basi wakati mwingine kuuhamishia 'uhasimu fulani' wa 'Wana wa Miungu' kufanyika hapa duniani pia kwa baadhi ya watu na mataifa hapa duniani...

Mambo mengi yanayosomwa kwenye habari za simulizi za Biblia ni drama za 'Wanadamu' na 'wana wa Miungu'... Iwe habari za 'mambo ya makuhani' na utundu wa 'madhabahu': mambo ya 'Maagano' ama/na 'upatanisho'--mawasiliano ya kimaingiliano ya utamaduni na ustawi na viumbe watu kutoka Juu...

Dini zote ni muktadha wa 'Miundo thibitifu' ya Utamaduni na Ustawi wa watu... Ni biashara inayobidi kuwepo kulingana na 'ufahamu pofu/hafifu wa kibinadamu' dhidi ya urithi wa kimbingu -- urithi wa kimbingu uliyo ni mawezekano wa wanadamu wote-- 'Uwezo/Utukufu/Maarifa/Ufahamu wa Uzima wa Milele'.

Karne hii ya 21, hili ndilo linaloleta shauri la 'Kurejea kwa Kristu'--Kristu ni Ufahamu; Ufahamu unaokomboa mtu kutoka kwenye 'jela ya kufikirika'--Matriksi...

Hmmm

Mark 3:11

View: https://www.youtube.com/watch?v=SDkAGkd4NLc
 
Hizi Code Ni ngumu Sana Rabboni Unawapa Jf hakuna atakaye kuelewa..

Tena kama Ukiwaambia Melchzedek hana Baba wala mama Hana mwanzo wala Mwisho!
Utawachanganya waumini wako..

Halafu yesu Ni mfano wa Melchzedek
Yesu sio mfano wa Melkizedeki, la hasha. Ni aidha Yesu ndie Melkizedeki, au Ni Mungu mwenyewe, au ni Roho Mtakatifu.

Yeye ndie mfalme wa Amani, hana mwanzo wala mwisho, kila kilichoelezewa kwenye Mwanzo ndio kimedhihirika kwenye Waebrania 7...sasa hapo upewe nini tena cha kuelewa...kama kweli na wewe ni jasusi, unamalizia tuu ku-decode kisha unakula madini.

Its clear.

Leo ndio nimepata kuelewa mtu wa tatu ambaye hakufa..kwa undani zaidi.

Ahsante sana mtoa mada, Mungu akubariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom