Megan na Roc kufikishwa mahakamani

Megan na Roc kufikishwa mahakamani

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
170
Reaction score
382
Rapa Megan Thee Stallion na kampuni yake ya Roc Nation watalazimika kukabiliana na kesi mahakamani baada ya jaji kukataa kufuta baadhi ya madai yaliyowasilishwa na aliyekuwa mpiga picha wake, Emilio Garcia.

Garcia alifungua kesi mwaka 2024, akidai kuwa wakati wa ziara ya Megan barani Ulaya, alilazimishwa kushuhudia tukio la ngono lililodaiwa kufanyika ndani ya gari. Hata hivyo, haya bado ni madai ya Garcia, na mahakama haijathibitisha kwamba tukio hilo lilitokea. Mbali na hilo, Garcia anadai kwamba hakulipwa vizuri, alibaguliwa na pia alilipiziwa kisasi baada ya kulalamika kuhusu malipo yake.

Jaji Gregory H. Woods ameamua kwamba baadhi ya madai hayo yanaweza kuendelea mahakamani, Na pande zote zitatoa ushahidi, kisha jury itaamua kama madai hayo yana ukweli au la.
SaveClip.App_772604266_18372113863227783_4692030406334233515_n.jpg
 
Ngoja tuone kama huyo Emilio ana picha kweli au ni drama tu za kutaka kulipwa hela.
 
Back
Top Bottom