mkosa shingo
Member
- Jan 26, 2021
- 93
- 127
Mshana mi nahitaji nije unifundisheKwanza mniwie radhi nitachanganya lugha kiingereza na kiswahili
Pili post yaweza kuwa ndefu tuvumiliane lakini nitajitahidi kuifupisha
Wanaforum tumekuwa na masomo mengi mazuri juu ya meditation hasa toka kwa Pasco Mtambuzi heshima kuu kwao na ndugu yetu Rakims
Ni masomo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliwanufaisha wengi lakini bahati mbaya sana tulipitiwa na kudhani kuwa wote wako kwenye ile level moja nasi ya uelewa hivyo masomo mengi yakawa in deep na kiufundi zaidi bila kuelewa kuwa wasomaji wengine walihitaji kwenda nao kuanzia chini kabisa
Meditation bado ni kitu kigeni kwenye familia zetu na kwa kiasi kikubwa inahusishwa na nguvu za giza hasa kutokana na mapokeo yetu kwenye mambo kama hayo, hivyo ni vigumu mno kuwa na meditation huru uwapo nyumbani mtaani au kazini, lakini bado kukiwa na uhitaji mkubwa wa hiki kitu hasa kwa wale ambao tayari wana upeo na uelewa fulani wa meditation
Fuatana nami katika mada hii ambayo kwa njia mojawapo yaweza kukupa nafasi ya kufanya basics za meditation bila bughudha
1.Time management n discipline
Tengeneza utaratibu wa kufanya jambo moja kwa muda ule ule at least mara 5 kwa wiki! Yaani kwa mfano lazima uamke saa 12 kamili asubuhi, moja kamili lazima uwe uko njiani kwenda kazini saba kamili lunch mbili kamili dinner na saa nne kamili unapanda kitandani (huu ni mfano tu)
2.lishe na kinywaji
Hakikisha unakua na kipimo kisichobadilika kwenye chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku, maji pekeyake ndio unaweza kunywa mengi bila kipimo maalum
chakula ni kwa ajili ya afya ya mwili na si ladha ya mdomoni hivyo usiongeze kipimo kwa ile ladha upendayo na kupunguza kipimo kwa chakula usichokipenda
3.Jambo moja kwa wakati mmoja chochote ufanyacho na muda hata wa dk tano ukipata jaribu kumakinika na kufanya breathing meditation au counting breath meditation kimya kabisa.
Kama unadrive concentrate kwenye driving kama uko kwenye usafiri wa jumuiya kaa kimya na kuwa mtulivu ukiendelea na meditation yako usihamaki kuhusu foleni nk mwachie dereva hiyo headache
Haya yaweza kuwa rahisi kuyasoma lakini practice ikawa ngumu lakini msingi wa meditation huanzia huku
Weza kuji control kwenye muda Weza kuji control kwenye lishe na Weza kuji control kwenye kufanya jambo moja kwa wakati mmoja baada ya hapo tutapeana hatua inayofuata
Mimi ni muda tu nilianza kufanya meditation na kufata kanuni mpaka za ulaji ( kutokula nyama) japokuwa kwa sasa napiga nyama kidogo ki aina
Nilikuwa kwenye path society moja hivi na nikaanza safari ya kiroho ( Spiritual journey) kwa lengo la kufika ktk enlightenment, sijafika na bahati mbaya sijaendelea
Nimekaa sana nilipokuwa naanza kwenye Breath meditation/Pumzi, nikaja kwenye Mantra (chanting) ndo nikaanza safari ya kiroho ku meditate kwenye nuru na sauti na kama nilivyosema sijafanikiwa kufika mwisho wa self-realization
Ila yote kwa yote meditation/Tahajudi ni kitu kizuri sana hasa kuweza ku control mazingira yetu japokuwa pia unaweza ingia ktk ku manipulate hali fulani na zingine ni kinyume na kanuni za maumbile na mwishoe unawajibishwa na maumbile kwa kukiuka huko
Bado nina meditate japokuwa sio kama zamani nilikuwa naweza kaa hata masaa matano ndani ya meditation, ila mimi muda mwingi nikiwa kwenye utulivu wowote tu automatic inakuja sauti na pia natumia sana binaural beats za ( meditation, calmness, sleeping, positive vibes, cleansing chakra/ Aura) ni mimi Earpod/earphones zangu tu
Asante Mshana Jr kwa kutoa elimu hii na ni muda wa watu wengi kuanza kufahamu hizi elimu , blessed
Mshana Jr. Hapo Upanga darasa au kwani nahitaji uelewa wa hii Elimu.Tunakuwaga pale upanga kila Jumapili
Mkuu Mshana Jr nimeisikiliza hiyo "Buddhist song" mbona kama Ina vinanda vingi Sana na sauti za maneno, huoni kama Zita mchanga ya meditator? Kuna uhusiano gani wa yale maneno na ku-meditate, hata kama siyaelewi maana yake japo yananiondolea umakini kuyasikiliza Sio kama itakuwa inatengenezwa visualation/ imagination?
Vyote unapata hapoMshana Jr. Hapo Upanga darasa au kwani nahitaji uelewa wa hii Elimu.
Asante
Hiyo midundo na hivyo vinanda ndio vinapeleka vibrations za ku trigger on tafakuri zako...lakini si lazima usikize hii tu zipo za kila ainaMkuu Mshana Jr nimeisikiliza hiyo "Buddhist song" mbona kama Ina vinanda vingi Sana na sauti za maneno, huoni kama Zita mchanga ya meditator? Kuna uhusiano gani wa yale maneno na ku-meditate, hata kama siyaelewi maana yake japo yananiondolea umakini kuyasikiliza Sio kama itakuwa inatengenezwa visualation/ imagination?
Mshana unaweza nisaidia kupata mwalim Mwanza?Hiyo midundo na hivyo vinanda ndio vinapeleka vibrations za ku trigger on tafakuri zako...lakini si lazima usikize hii tu zipo za kila aina
Sent using Jamii Forums mobile app
Mku Ada ni kiasi gani na inalipwaje.
Mimi ni mwanamke. naweza nikija kujua vizuri ni mda gani kaka?
Ooh Mungu wangu hizi ID hizi..my apology..beginners course ile ya basics ukiwa na juhudi ni miezi 3Mimi ni mwanamke. naweza nikija kujua vizuri ni mda gani kaka?
Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Asante kaka hapo hapo upanga eneo gani nikifika naulizaje?Ooh Mungu wangu hizi ID hizi..my apology..beginners course ile ya basics ukiwa na juhudi ni miezi 3
Ukitoka fire kwenda Muhimbili, utaacha njia ya kwanza inayoingia kwenda Muhimbili utaingia njia ya pili nyumba ya tano mkono wa kushoto sorry wa kuliaAsante kaka hapo hapo upanga eneo gani nikifika naulizaje?
Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mshana Jr. Nashukuru sana