Media kususia habari za fulani: Je, Tanzania tuna Independent Media yenye jeuri hiyo?

Kwa style yako ya uandishi watu wanapokea kweli hizo unazoita makala? kama ungekua independent kama unavyojiita ungesha anzisha hata kaji digital circulation cha hizo makala zako kama unavyojinasibu...
 
Nilitegemea waandishi ni wanaume,mngesusa kwa Mwezi mmoja tu kutoa picha ya Baby yake,kama leo waandishi wako Protea baby yake iko Bandarini
Mkuu Shemeji Tetty, kwa sababu kuandika na kusambaza habari ndio the only survival kwa media, ili media ziweze kususa lazima ziwe na bima ya guarantee kuwa mkisusa mtaendelea kulipwa ruzuku ili muendelee kuishi. Then hili litawezekana.

Paskali
 
Kwa style yako ya uandishi watu wanapokea kweli hizo unazoita makala? kama ungekua independent kama unavyojiita ungesha anzisha hata kaji digital circulation cha hizo makala zako kama unavyojinasibu...
Mkuu Lyamber, mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika just for the love of it and not making my living kwa uandishi, hivyo ninazo shughuli nyingine za kunifanya niishi mjini na sio uandishi. Hivyo hii circulation kupitia JF, is more than enough.
Paskali
 
Jamani TEF wamesema msiandike Habari za makonda hamuelewi......
Sijui magezeti yatauza nini, na pia Maana yake story hii imeisha maana hatutoisikia Tena,
Asanteni TEF watu tufanye kazi Sasa
Ni kwamba magazeti hayataandika zile drama zake lakini akifanya uvamizi mahali; hiyo ni BIG news ambayo lazima ipate coverage ya juu!!!
 
Wanabodi,

Nikiwa mwana wa tasnia ya habari, leo nimelisikia tangazo la Jukwaa la Wahariri kususia habari za fulani. Swali ni Jee Tanzania tuna independent media yenye jeuri ya kuweza kususia habari za mtu fulani? .

Jibu ni hapana, hatuna hizo media japo nakiri tuna magazeti machache independent yenye jeuri hiyo ambapo hata mfalme akifanya vibaya yatasema loud and clear bila kumung'unya maneno na jf ni one of them.

Only some few media zenye independent editorial independence ndio zita implement hili la kususia kwa sababu wanayo jeuri hiyo ya kususa. Media nyingine zote zikiwemo media zote za umma, media zote za serikali, media za chama na media zenye njaa, zote hazina jeuri hiyo ya kususia.

Tusitegemee media kama TBC, RTD, Daily News, Habari Leo, Uhuru, Mzalendo, Radio Uhuru, Idara ya Habari Maelezo na mitandao ya kijamii, kususia.

Jambo kama hili limeishatokea huko nyuma baada ya kifo cha Daudi Mwangosi, kwa kuuliwa na polisi, ikaamuliwa habari za polisi zisuswe. Kususa huko kulidumu kwa siku moja tuu, na kesho yake walianza kugeukana.
Sababu ni hizi.
1. What is News?.
Kazi ya media zote ni kutoa kutoa habari, yaani kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa lengo la kuihudumia jamii. Katika kufanya hayo, zikomedia zinayafanya hayo kama huduma (not for profit) na ziko media zinayafanya hayo ili kuishi, yaani ili kuuza gazeti, sasa kama huyo fulani ndio habari ya mujini inayouza gazeti, huwezi kuacha kumripoti utalala njaa, utakuwa hujatimiza wajibu wako na kubwa zaidi ni kuitendea haki jamii unayowajibika kwake.Hivyo hata leo mtashuhudia headlines zenye hilo jina.

2. Kwenye tasnia ya habari, kuna kitu kinaitwa "pressures shapping the news", hizi sio habari bali determinant factors zinazofanya habari fulani iandikwe na habari fulani isiandikwe!. Moja ya factor kubwa kuliko zote ni "money matters"!. Survival ya vyombo vingi vya habari sio circulation, sio readership, sio viewership au audience bali ni matangazo!. Watangazaji wakubwa wanaitwa sponsors ndio waamuzi wakubwa wa what is news na media lazima ziwasikilize. Hawa sponsors are the ones calling the shots!. "He who pays the piper, may call the tune". Huko ndiko mshahara utokako.

3. Big Names Make News, yaani jina kubwa linatengeneza habari kubwa. Sasa nyuma ya huye anayesuswa kuna "jina kubwa lipitayo majina yote" (Not Jina Kubwa Lipitayo Majina Yote) ambalo ni jina la yule 'malaika mlinzi' wake, hivyo kama atahakikisha kila tukio lake, atakuwa na 'mwanae mpendwa wake anayependezwa naye' na ndiye atakayekuwa akiongea kwa niaba yake kwenye kila tukio, nani atakuwa na jeuri ya kususa? au kumkwepa? ,atakuwa hakwepeki!.

4. Aandishi wa habari ni nobel professional yaani kazi ya wito, na kwa wengi ni kazi ya kuakuajiriwa, ni kazi ya kutumwa au kitumwa, waandishi ni watumwa tuu, kazi yao ni kutumwa!. Mtumwa hana uhuru wala ridhaa jukumu lake ni kutekeleza tuu matakwa ya masters wake!.Hivyo mtumwa akitumwa na bosi, ana jeuri gani ya kususa?
Kumlaumu mtumwa ni kumuonea bure!. Mtumwa ni mtu wa kutumwa tuu kuhurumiwa!.

Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na editors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

Taarifa zozote muhimu za msuswa sasa zinaweza zikaletwa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, je nani watakuwa na jeuri ya kususa? .

Huko nyuma tuliwahi kujadili hili kwenye mada hiiWaandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya

Hivyo waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za mtu yoyote kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu wa Clouds kuvamiwa, hasira zikipoa, wataendelea kuandika!.

Waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.

Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu nyingine za kufanya kuendesha maisha yetu and to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!.

Ila watu kama mimi kama Paskali, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.

Bado naendelea kulia kuwa tuna tatizo kubwa humu jukwaani jf, kwa watu wengi humu tuna tatizo la kuukubali ukweli halisi unaitwa "is" na kuukumbatia ukweli tunaoutaka uwe unaitwa "ought". Mimi ni mtu wa mkweli wa ukweli halisi "is" na sio so "ought" ambao ndio ule ukweli ambao wengi wanaupenda use, yaani ukweli wa kujifurahishia.

Kususia huko kulidumu kwa siku moja tuu ya uchungu ule, amini msiamini kesho Bashite akiitisha Press Conference, hamtaamini macho yenu.

Let's hope for the best ya hiki kisuso this time, sijui kitadumu kwa muda gani na ni media zipi bold enough kususa!.

Hongera JF nilinote hili jina la Bashite limefutwa.
Paskali.
Safi saana Mzee wa kiti moto ni ukweli halisia.
Bashite ni habari ila asilembwe toa kavukavu kama inawezekana..
 
Utajuaje pingamizi hili litafanya kazi bila kujaribu? Ngoja wajaribu na ikishindikana wataangalia nini kikwazo na wakabiriane na hicho kikwazo vipi?
Obviously vyombo vya habari vya serikali na chama ni ngumu kutekeleza hili agizo. Lakini wangapi wanaangalia, kusikiliza na kusoma habari za vyombo hivi? Maana Raisi na hata huyo Daudi wamekuwa wakitumia vyombo binafsi wakijua wazi vyombo vyao si vyakutazamwa/kusikizwa kiasi hicho ukiacha gazeti la daily news. Mfano, mimi husikiliza tbc pale kunakuwa na kipindi cha mtangaziji/mburudishaji Masoud Masoud tu - labda waanzishe kipindi Makonda time ili wenye mahaba na RC wao wawe wanakisubiri. Hivyo somehow makonda taarifa zake hazitasambaa sana. RC anaweza itisha press conference akapata mwitikio lakini hiyo haiyoshi, je what next habari zitarushwa hewani? Nafikiri sasa huyu RC atategemea zaidi social media ili habari zake kusambaa. Akiona haifanyi kazi atarudi kuomba msamaha.
 
Uzuri wewe ni mwandishi alafu ni mwanasheria nguli,ninakufahamu kiasi na ulishanitembelea kwangu mwaka2012 ukiwa na gari yako kama sikosei ilikua rav4 short cheses nyeusi,hope itakua umenikumbuka kiasi.BACK TO TOPIC:tangu Sakata la huyu bwana limeanza sijaona topic yako yoyote ya kuonesha kumlazimisha atoe vyeti,mbaya zaidi umekua ni mtu wa kumtetea kiaina hivi.
Nina wasiwasi na wewe mkuu,nahisi kuna masirahi fulani unayapata kwa kumtetea huyu bwana,na mm nakushauri ni bora uendelee kumtetea otherwise tutakukosa.Endapo kituo kikubwa kama kile kimevamiwa kwa kukataa tu kuonesha 'udaku' vipi wewe mwana JF kipenzi cha wengi?
Ni hayo tu kwa leo kaka angu Pascal Mayalla
Ila kumbuka Pascal ndo mtu WA kwanza kuandika habari za kufoji vyeti mwaka Jana mwezi WA 12. Kumbuka vzr mwanzilishi wa hoja hiyo ni nani?
 
nape nnauye alishiriki kutuletea sheria mbovu ya habari haijapata tokea hafu Leo Hi anajifanya anataka huruma kutoka kwa waandishi na watz kwa ujumla
 
Wanabodi,

Nikiwa mwana wa tasnia ya habari, leo nimelisikia tangazo la Jukwaa la Wahariri kususia habari za fulani. Swali ni Jee Tanzania tuna independent media yenye jeuri ya kuweza kususia habari za mtu fulani? .

Jibu ni hapana, hatuna hizo media japo nakiri tuna magazeti machache independent yenye jeuri hiyo ambapo hata mfalme akifanya vibaya yatasema loud and clear bila kumung'unya maneno na jf ni one of them.

Only some few media zenye independent editorial independence ndio zita implement hili la kususia kwa sababu wanayo jeuri hiyo ya kususa. Media nyingine zote zikiwemo media zote za umma, media zote za serikali, media za chama na media zenye njaa, zote hazina jeuri hiyo ya kususia.

Tusitegemee media kama TBC, RTD, Daily News, Habari Leo, Uhuru, Mzalendo, Radio Uhuru, Idara ya Habari Maelezo na mitandao ya kijamii, kususia.

Jambo kama hili limeishatokea huko nyuma baada ya kifo cha Daudi Mwangosi, kwa kuuliwa na polisi, ikaamuliwa habari za polisi zisuswe. Kususa huko kulidumu kwa siku moja tuu, na kesho yake walianza kugeukana.
Sababu ni hizi.
1. What is News?.
Kazi ya media zote ni kutoa kutoa habari, yaani kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa lengo la kuihudumia jamii. Katika kufanya hayo, zikomedia zinayafanya hayo kama huduma (not for profit) na ziko media zinayafanya hayo ili kuishi, yaani ili kuuza gazeti, sasa kama huyo fulani ndio habari ya mujini inayouza gazeti, huwezi kuacha kumripoti utalala njaa, utakuwa hujatimiza wajibu wako na kubwa zaidi ni kuitendea haki jamii unayowajibika kwake.Hivyo hata leo mtashuhudia headlines zenye hilo jina.

2. Kwenye tasnia ya habari, kuna kitu kinaitwa "pressures shapping the news", hizi sio habari bali determinant factors zinazofanya habari fulani iandikwe na habari fulani isiandikwe!. Moja ya factor kubwa kuliko zote ni "money matters"!. Survival ya vyombo vingi vya habari sio circulation, sio readership, sio viewership au audience bali ni matangazo!. Watangazaji wakubwa wanaitwa sponsors ndio waamuzi wakubwa wa what is news na media lazima ziwasikilize. Hawa sponsors are the ones calling the shots!. "He who pays the piper, may call the tune". Huko ndiko mshahara utokako.

3. Big Names Make News, yaani jina kubwa linatengeneza habari kubwa. Sasa nyuma ya huye anayesuswa kuna "jina kubwa lipitayo majina yote" (Not Jina Kubwa Lipitayo Majina Yote) ambalo ni jina la yule 'malaika mlinzi' wake, hivyo kama atahakikisha kila tukio lake, atakuwa na 'mwanae mpendwa wake anayependezwa naye' na ndiye atakayekuwa akiongea kwa niaba yake kwenye kila tukio, nani atakuwa na jeuri ya kususa? au kumkwepa? ,atakuwa hakwepeki!.

4. Aandishi wa habari ni nobel professional yaani kazi ya wito, na kwa wengi ni kazi ya kuakuajiriwa, ni kazi ya kutumwa au kitumwa, waandishi ni watumwa tuu, kazi yao ni kutumwa!. Mtumwa hana uhuru wala ridhaa jukumu lake ni kutekeleza tuu matakwa ya masters wake!.Hivyo mtumwa akitumwa na bosi, ana jeuri gani ya kususa?
Kumlaumu mtumwa ni kumuonea bure!. Mtumwa ni mtu wa kutumwa tuu kuhurumiwa!.

Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na editors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

Taarifa zozote muhimu za msuswa sasa zinaweza zikaletwa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, je nani watakuwa na jeuri ya kususa? .

Huko nyuma tuliwahi kujadili hili kwenye mada hiiWaandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya

Hivyo waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za mtu yoyote kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu wa Clouds kuvamiwa, hasira zikipoa, wataendelea kuandika!.

Waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu!. Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!.

Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha kuandika just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu nyingine za kufanya kuendesha maisha yetu and to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!.

Ila watu kama mimi kama Paskali, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!.

Bado naendelea kulia kuwa tuna tatizo kubwa humu jukwaani jf, kwa watu wengi humu tuna tatizo la kuukubali ukweli halisi unaitwa "is" na kuukumbatia ukweli tunaoutaka uwe unaitwa "ought". Mimi ni mtu wa mkweli wa ukweli halisi "is" na sio so "ought" ambao ndio ule ukweli ambao wengi wanaupenda use, yaani ukweli wa kujifurahishia.

Kususia huko kulidumu kwa siku moja tuu ya uchungu ule, amini msiamini kesho Bashite akiitisha Press Conference, hamtaamini macho yenu.

Let's hope for the best ya hiki kisuso this time, sijui kitadumu kwa muda gani na ni media zipi bold enough kususa!.

Hongera JF nilinote hili jina la Bashite limefutwa.
Paskali.
Noted
 
Mkuu Shemeji Tetty, kwa sababu kuandika na kusambaza habari ndio the only survival kwa media, ili media ziweze kususa lazima ziwe na bima ya guarantee kuwa mkisusa mtaendelea kulipwa ruzuku ili muendelee kuishi. Then hili litawezekana.

Paskali

Kila siku mnaandika nini??Nimeona Mkullu hajaandikwa na watanzani wengi wanahamu zaidi ya kumsikiliza Nape na Kinana kuliko Mkwe wangu sasa hili Shemeji nalo unalisemeaje??

Mbona kuna vitu vingi sana vyakuandika na si lazima Mkullu tu?
 
Wana JF nafikiri huu uzi utatusaidia kujadili kimakini bila mihemukokuhusu ususiaji wa kuandika habari za mtu fulani..

Agizo ama MAKUBALIANO kati ya TEF na UTPC ni ukiukaji mkubwa wa katiba ya nchi yetu. Hasa ikizingatiwa kuwa vyombo vya habari ndo vinatakikana kuwa MSTARI wa MBELE katika kuhamasisha kama kuna UKIUKWAJI wowote wa katiba kwa mtu yeyote pasipo kujalicheo chake.
Iwe ni katika kuikumbusha SERIKALI mahali imejisahau lakini si kushiriki katika KUIKIUKA katiba

Juzi juzi TEF na UTPC walikubaliana kumpa BLACKOUT mtumishi mmoja wa serikali.
Naomba NIELEWEKE uzi huu si wa kumtetea mtu yeyote bali ni kusimamia haki ya kikatiba.

Katika Katiba ya nchi yetu Article on RIGHT TO FREEDOM and CONSCIENCE 18 6{d} na
[1b] ya 2005.

Inasema nami nanukuu Hapohapo.I{b}inasema "Mtu ana HAKI ya KUTAFUTA, KUPOKEA na KUPATIWA HABARI"
]

[6d]"Mtu ana HAKI ya kujulishwa HABARI zinazotokea wakati WOWOTE ziwe ni za MATUKIO MUHIMU ya kimaisha na JAMII...." Mwisho wa kunukuu.

Ombi langu ni kuwa tafadhali TEF na UTPC msikiuke katibaya nchi kwa sababu ya KUTOELEWANA na mtu MMOJA.

Waingereza wanamsemo "TWO wrongs do not make a RIGHT"/MAKOSA mawili HAYAKUHALALILISHI utende kama ULIVYOTENDEWA"

Hivyo ni kusema Wananchi wana HAKI ya kusikia na kujua
habari za WABUNGE, MAWAZIRI AMA kiongozi yeyote wa KISERIKALI AKIWA KAZINI kwa manufaa ya UMMA bila KUJALI YULE ANAYEANDIKA nini ALICHOKOSEWA na mtu huyo.
Nafikiri hizo ni MOJA ya ETHICS za UANDISHI wa HABARI.

Hata kama mtu hataki kuomba msamaha, TAIFA na WATU wake ni la MUHIMUzaidi kuliko mtu mmoja!!!.
TEF na UTPC yatafakarini hayo.
 
kutoka kwa kiongozi yeyote wa SERIKALI
Ni uhuru wa mwenye chombo kuamua arushe nini hawalazimishwi hao. Ila natabiri mkwara wa kuvifuta vyombo vyote ambavyo havirushi habari za viongozi wa serikali nadhan itajengwa hoja ya namna hiyo
 
Katiba ya nchi ni sheria mama,yani sheria zozote zile za nchi lazime zitokane au zisikiuke katiba/sheria mama inamaana kwamba jukwaa la wahariri wanakatiba na sheria zao walizoziunda kutokana na katiba ya nchi na kupitishwa na vyombo husika,basi ni sawa kwa kuwa hawajakiuka katiba ya nchi...

Kwahiyo hakuna kosa kwa kuwa amejitakia mwenye...
Mwizi anakuja kwako anakuibia na unathibitisha kesho unampa chakula ujue wewe pia ni bashite kichwani!!//
 
Aah nani kasusa mbona bado wanamuandika tena kwa ukurasa wa mbele. Shukrani tu wahariri wamezima kiki za gwajima
 
Back
Top Bottom