Media kususia habari za fulani: Je, Tanzania tuna Independent Media yenye jeuri hiyo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Declaration of interest: Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, niliyeamua kujikita katika kuandika habari za kimaendeleo. Uzi huu sio wa kutetea ujinga na upuuzi wa mvamizi wa Clouds media, ila ni uzi wa kuzuia ujinga na upuuzi mwingine unaotakwa kufanywa juu ya ujinga na upuuzi uliokwisha fanyika.

Nikiwa mwana wa tasnia ya habari, leo nimelisikia tangazo la Jukwaa la Wahariri TEF kuhamasisha media kususia habari za fulani. Swali ni who the hell is TEF?, na Jee Tanzania tuna independent media yenye jeuri ya kuweza kususia habari za mtu fulani? .

Jibu ni TEF is nothing! TEF sio bona fide media representative organization in Tanzania, hivyo sio wawakilishi halali wa media wanaoweza kuendesha mgomo halali kususia habari za fulani. TEF ni Editors Forum, yaani ni Jukwaa la Wahariri, but very unfortunately, hao editors are not media owners, hivyo ili zoezi hili la kususa lifanikiwe, lazima kwanza media owners wa hizo media waridhie msimamo wa editors wao. Kwa hesabu za haraka haraka kwa kumfikiria who is behind Bashite, then who are the media owners that can dare do that?

Pili ni Jee Tanzania tuna independent media ambayo have the capacity and the capability ya kususa? Ukiondoa media za The Nation, (Citizen na Mwananchi), na vyombo vya habari vya IPP Media ambayo ni notorious kwa kususa habari za kila anayetofautiana na Mwenyekiti wa IPP, pamoja na Moat ambayo ni just a puppet organization ya Chairman wa IPP, kiukweli kabisa, Tanzania hatuna independent media zenye the capacity and the capability kususia habari za fulani!

Japo nakiri tuna magazeti machache yenye pseudo-independent ya umiliki, yenye jeuri hiyo ya kususia habari za fulani, ambapo hata mfalme akifanya makosa, yatasema loud and clear bila kumung'unya maneno kuwa Mfalme amekosea. Miongoni mwa media zenye jeuri hiyo, jf ni one of them.

Only some few media zenye independent editorial policy, ndio zita implement hili la kususia kwa sababu wanayo jeuri hiyo ya kususa. Media nyingine zote zikiwemo media zote za umma, media zote za serikali, media za chama na media zenye njaa (ambazo ndizo nyingi zaidi), ambazo lazima lazima zijipendekeze, hazina jeuri hiyo ya kususia habari za fulani!.

Tusitegemee media kama TBC, RTD, Daily News, Habari Leo, Uhuru-Mzalendo, Radio Uhuru, Idara ya Habari Maelezo na mitandao ya kijamii, kususia.

Jambo kama hili limeishatokea huko nyuma baada ya kifo cha Daudi Mwangosi, kwa kuuliwa na polisi, ikaamuliwa habari za polisi zisuswe. Kususa huko kulidumu kwa siku moja tuu, na kesho yake walianza kugeukana

Sababu ni hizi.

1. What is News?
Kazi ya media zote ni kuihudumia jamii kwa kutoa kutoa habari, yaani kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Hivyo jukumu la media kuhabarisha jamii is a duty na sio favour, hivyo responsible media haiwezi kususa kutoa habari za fulani kwa sababu mlaji wa habari sio huyo fulani anaesuswa bali ni jamii, huwezi kuiadhibu jamii kwa kuikosesha habari kwa kisingizio cha kususia habari za fulani sio kuwatendea haki jamii.

Katika kutekeleza kususa huko, ziko media zinafanya kazi ya media kama huduma (not for profit) hivyo zinahudumia jamii as a duty, hizi hazita susia habari yoyote muhimu kwa jamii.

Pia na ziko media zinafanya biashara ya media for survival ili kuishi, yaani ili kuuza gazeti, sasa kama huyo fulani ndio habari ya mujini inayouza gazeti, huwezi kuacha kumripoti sio tuu utalala njaa, bali utakuwa hujatimiza wajibu wako na kubwa zaidi ni kutoiendea haki jamii unayowajibika kwake. Hivyo hata leo, kesho na keshokutwa, mtashuhudia headlines zenye hilo jina.

2. Pressures Shaping the News
Kwenye tasnia ya habari, kuna kitu kinaitwa "pressures shaping the news", hizi sio habari bali determinant factors zinazofanya habari fulani ama iandikwe ama isiandikwe, hivyo uamuzi habari ya fulani ianmdikwe au isiandikwe huamuliwa na hizi pressures na sio TEF.

Moja ya factor kubwa kuliko zote ni "money matters". Survival ya vyombo vingi vya habari sio circulation, sio readership, sio viewership au audience bali ni matangazo!. Watangazaji wakubwa wanaitwa sponsors ndio waamuzi wakubwa wa what is news na media lazima ziwasikilize. Hawa sponsors are the ones who pays the piper hivyo calling the tune!, they are the gun holders who are calling the shots!. "He who pays the piper, may call the tune". Huko ndiko mshahara na fedha za uendeshaji wa media zinakotoka.

3. Big Names Makes News
Jina kubwa linatengeneza habari kubwa. Sasa nyuma ya huyu anayesuswa kuna "jina kubwa lipitayo majina yote" (Not Jina Kubwa Lipitayo Majina Yote) ambalo ni jina la yule 'malaika mlinzi' wake, hivyo kama yeye ataamua kwenye kila tukio lake, ataambatana na 'mwanae mpendwa wake anayependezwa naye' na ndiye atakayekuwa Yohana Mbatizaji wake, ama akitangulia kuongea kabla yake ama akiongea kwa niaba yake kwenye kila tukio, nani atakuwa na jeuri ya kususa? au kumkwepa? ,atakuwa hakwepeki!.

4. Uandishi wa habari ni nobel professional
Yaani kazi ya wito, na kwa wengi ni kazi ya kuakuajiriwa, ni kazi ya kutumwa au kitumwa, wengi wa waandishi ni waajiriwa, ni watu wa kutumwa tu, hivyo ni watumwa, kazi yao ni kutumwa! Mtumwa hana uhuru wala ridhaa yake kuchagua atatumwa nini, jukumu lake ni kutekeleza tuu matakwa ya masters wake anayemtuma! Je, mtumwa anayesubiri kutumwa na bosi, ana jeuri gani ya kususa?

5. Waandishi Wengi wa Tanzania ni Watumwa!
Kumlaumu mtumwa ni kumuonea bure! Mtumwa ni mtu wa kutumwa tu kutekeleza, hivyo akitumwa kuripoti habari za fulani, yeye atatekeleza tuu.

Wengi wa waandishi wa Tanzania, ni waandishi watumwa. Hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kazi ya uandishi kwa utashi wa editors na editors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

Taarifa zozote muhimu za msuswa sasa zinaweza zikaletwa kupitia ile Kurugenzi ya Mawasiliano, je nani watakuwa na jeuri ya kususia habari za kurugenzi ya mawasiliano?.

Huko nyuma tuliwahi kujadili hili kwenye mada hii
Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya

Hivyo waandishi wa habari waajiriwa, hawana jeuri ya kususia habari za mtu yoyote kwa sababu ni watumwa, huko kususa, ni hasira za uchungu wa kuvamiwa kwa Clouds media, hasira zikipoa, wataendelea kuandika habari za huyo msuswa.

Waandishi wenye jeuri ya kususia kuandika

au kuripoti habari fulani ni ama sisi waandishi wa kujitegemea, ambao tuko independent, hatumtegemei mtu, au waandishi ambao ndio media owners kama kina Manyerere na Balile ambao wanamiliki gazeti, hawa wana pseudo-independence ya umiliki, lakini gazeti lao bado linategemea matangazo ku survive, ili wapate full independence, inabidi gazeti lao lisimame kwa kutegemea circulation. Magazeti yanayo survive kwa kutegemea circulation nchini Tanzania ni magazeti ya udaku!

"freelance journalist"
Kwenye hii kada ya waandishi wa kujitegemea, tuko wa aina mbili, aina ya kwanza ni "freelance journalist", hawa wanaandika na kuitegemea hiyo habari ndio imlipe, newsroom nyingi zinalipa 3,000, 5,000 kwa habari moja itakayotoka, na labda 10,000 kama habari itakuwa ndio lead story!, huyu mwandishi akifanikiwa ku file story 1 tuu kwa siku na ikatoka, mwisho wa mwezi atavuta 90,000 tuu! Waandishi wa kada hii ndio hutegemea "bahasha" to survive!, hawa wana jeuri ya kususa kwa kuamua kuandika habari nyingine zozote, ila kama habari hizo hazilipi, wataishia kujifia njaa hivyo soon mtashuhudia waandishi njaa wakirejea kumtumikia kafiri!.

"independent journalists"
Kada ya pili ni "independent journalists", kada hii ndiko mimi niliko, inahusisha wanaoandika habari au makala just for the love of it, wengi wa kada hii tunazo shughuli zetu nyingine za kufanya kuendesha maisha yetu and to make our living, hivyo hatutegemei malipo yoyote kwa stories tunazotuma, mfano mimi silipwi hata senti tano kwa stories ninazofile kwenye media. Kundi hili ndio kundi kama la kina Mjengwa, Mzee Mwanakijiji etc, etc, enzi zile Mwanakijiji akitoa kile kijarida cha Cheche, alikitoa bure nasi tulikitawanya bure!. Kwa sasa Mjengwa, Mwanakijiji na wengine, ni waandishi wa makala mbalimbali kwenye magazeti mbalimbali. Kwa kawaida magazeti yanapaswa kuwalipa, sidhani kama wanaandika ili kujipatia hivyo vijisenti na I doubt hata kama wanachukua!. Kundi hili ndilo hatutumwi na mtu na hatumtumikii mtu zaidi ya jamii!. Sisi ndio wenye jeuri ya kususa, inapotokea need ya kususa, tunaweza kususa lakini kwanza lazima tujiulize, tunasusa for what?, and what are we trying to achieve?. Kususa ili kumkomoa tuu fulani, sio justified reason ya kususa!.

Ila watu kama mimi Paskali, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, kama ni gazeti, huamua gazeti gani nipeleke, au kama ni kwenye TV na redio, mimi mwenyewe ndio huamua pa kuipeleka!, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli kweli!

Hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote ni wale tuu ambao sio "watumwa" yaani wale waandishi wanaojitegemea na sio hawa waandishi "watumwa" wanaotegemea vyombo vya habari!, kutishia kususa kwa kujificha chini ya chaka la TEF, short lived, na muda ukifika, mtayakumbuka haya, msipoyakumbuka, nitawakumbusha!.

Ukweli wa "IS" na "Ought"
Bado naendelea kulia humu jukwaani jf, tuna tatizo kubwa la kuukubali ukweli halisi "is" na kuukumbatia ukweli tunaoutaka "ought". Mimi ni mtu wa mkweli wa ukweli halisi "is" na sio so "ought" ambao ndio ule ukweli ambao wengi wanaupenda kuusikia, yaani ukweli wa kujifurahishia. Tishio la kusuasi habari za Bashite ni kujifurahisha tuu!.

Somo la Kususa Toka Kifo cha Daudi Mwangosi (RIP)

Kususia kifo cha Daudi Mwangosi kulidumu kwa siku moja tuu ya uchungu ule, hivyo amini msiamini kesho, keshokutwa, Bashite akiitisha Press Conference, hamtaamini macho yenu jinsi watakavyo jazana!.

Let's hope for the best ya hiki kisuso this time, is real, sijui kitadumu kwa muda gani na ni media zipi bold enough kususa!.

Mwisho.
Media ni noble profession, hizi ni kazi za wito kama ualimu na udakitari, pia ni kazi za huduma kwa jamii, kama kazi za kampuni ya simu, posta, umeme, maji na udaktari,hospitalini etc, watumishi wa kada hizi kwa mujibu wa mikataba yao, hawaruhusiwi kugoma! Je, sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, tunaruhusiwa kugoma?, tukimgomea Daudi Bashite, jee tunawatendea haki wananchi na jamii tunayoihudumia?. Tukimgomea, tunamkomoa nani? Yeye anayependa kuonekana, au wananchi wanaopaswa kupata habari? Na habari zake zisipotoka kabisa, nani anaathirika kwa kutokuwepo kwa habari zake? Lets be objective kwenye hili!

Hongera JF nilinote hili jina la Bashite limefutwa.

Paskali.
 
Hata mimi nilijiuliza hili swali kuona kama itawezekana lakini nahisi watanywea tu.

Kama mtakumbuka kuna kipindi waandishi wa habari walitembezewa kipigo toka kwa polisi[sikumbuki tukio lakini siyo kwenye issue ya Mwangosi] then wakasema hawataripoti habari yoyote inayohusu jeshi la polisi kwa ujumla.

Baadae walikuja kusema kutokuripoti habari za polisi ni kuwanyima wananchi fursa ya kuhabarika. Hebu tusubiri kwenye hili la Makonda tuone watakuja na ''tafsida ipi ya kuficha njaa''
 
Jamani TEF wamesema msiandike Habari za makonda hamuelewi......
Sijui magezeti yatauza nini, na pia Maana yake story hii imeisha maana hatutoisikia Tena,
Asanteni TEF watu tufanye kazi Sasa
Ina maana hufanyagi kazi? Mbaya tutaendelea kuyaandika lakini asitegemee kuandika kwa jambo jema milele
 
Wahariri walikubaliana kutoandika chochote kuhusu Makonda iwe kwa baya ama zuri....Ndio maana humu JF wakaharamisha jina la Makonda, Bashite na Daudi.

Walivyogundua uamuzi wao unampa unafuu Makonda wakageuka eti wataandika mabaya tu ya Makonda....

Hapo utagundua vyombo vyetu vya habari vinatumika tu.

Mimi napendekeza msiandike wala kuripoti chochote kuhusu Makonda iwe kwa jema au baya.
 
Uzuri wewe ni mwandishi alafu ni mwanasheria nguli,ninakufahamu kiasi na ulishanitembelea kwangu mwaka2012 ukiwa na gari yako kama sikosei ilikua rav4 short cheses nyeusi,hope itakua umenikumbuka kiasi.BACK TO TOPIC:tangu Sakata la huyu bwana limeanza sijaona topic yako yoyote ya kuonesha kumlazimisha atoe vyeti,mbaya zaidi umekua ni mtu wa kumtetea kiaina hivi.
Nina wasiwasi na wewe mkuu,nahisi kuna masirahi fulani unayapata kwa kumtetea huyu bwana,na mm nakushauri ni bora uendelee kumtetea otherwise tutakukosa.Endapo kituo kikubwa kama kile kimevamiwa kwa kukataa tu kuonesha 'udaku' vipi wewe mwana JF kipenzi cha wengi?
Ni hayo tu kwa leo kaka angu Pascal Mayalla
 
Vyombo vingi vya habari hasa vyenye mlengo wa kibiashara vinapenda kuandika au kutangaza habari inayovutia wasomaji au wasikilizaji au watazamaji kifupi wanadeal na trending newz kwa sasa trending newz ni Makonda so sidhan kama kunachombo cha habari kinaweza kuandika habari za mkulima wa kisasa kama habari mpasuko na kuacha kuandika habari ambayo iko kwenye soko na habari pendwa habari zinazomuhusu Makonda
 
Hata mimi nilijiuliza hili swali kuona kama itawezekana lakini nahisi watanywea tu.

Kama mtakumbuka kuna kipindi waandishi wa habari walitembezewa kipigo toka kwa polisi[sikumbuki tukio lakini siyo kwenye issue ya Mwangosi] then wakasema hawataripoti habari yoyote inayohusu jeshi la polisi kwa ujumla.

Baadae walikuja kusema kutokuripoti habari za polisi ni kuwanyima wananchi fursa ya kuhabarika. Hebu tusubiri kwenye hili la Makonda tuone watakuja na ''tafsida ipi ya kuficha njaa''
Ilikuwa jeshi la magereza na waliamua kum-blackout Waziri Mapuri
 
Hawa ndo waandishi wa habari uchwara njaa mbaya sana tamko limeshatolewa na Jukwaa la Wahariri wewe kama bado unapenda kuandika habari za RC wa Dar Paulo endelea labda ndo unapata ujira wako huko.
 
Kama vipi jamii media, inayomiliki jamii forums nayo isusie habari zote zonazomhusu Bashite, japo hii ni user generated forum lakini wanaweza kuungana na ma-editors kwa sababu nao ni wanahabari.
 
Back
Top Bottom