OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,641
- 120,216
Wakuu wote wa JamiiForums,
Leo jumanne jioni ya saa 10 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam itapigwa mechi kati ya Yanga ya Tanzania na TP Mazembe ya Congo DRC!
Ni mechi ya kimataifa, Kombe la Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF! Tayari Yanga ina rekodi ya kufungwa katika mechi ya kwanza na MO Bejaia ya nchini Aljeria.
Mechi ya leo Yanga imejigamba kushinda na imefanya mkakati wa kuingiza wanachama wake bure ili kutia nguvu. Tutakuwa Live hapa JF kuwaletea matukio yote kabla na baada ya mechi.
Pia Azam TV na Super Sport itakuwa live. Asubuhi na mapema mashabiki wa Yanga na wapenda kabumbu kwa ujumla wameanza kumiminika Taifa kushuhudia kipute
Kikosi kamili cha Yanga leo