Mechi ya Yanga FC Vs TP Mazembe - Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,095
103,345



Wakuu wote wa JamiiForums,

Leo jumanne jioni ya saa 10 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam itapigwa mechi kati ya Yanga ya Tanzania na TP Mazembe ya Congo DRC!

Ni mechi ya kimataifa, Kombe la Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF! Tayari Yanga ina rekodi ya kufungwa katika mechi ya kwanza na MO Bejaia ya nchini Aljeria.

Mechi ya leo Yanga imejigamba kushinda na imefanya mkakati wa kuingiza wanachama wake bure ili kutia nguvu. Tutakuwa Live hapa JF kuwaletea matukio yote kabla na baada ya mechi.

Pia Azam TV na Super Sport itakuwa live. Asubuhi na mapema mashabiki wa Yanga na wapenda kabumbu kwa ujumla wameanza kumiminika Taifa kushuhudia kipute
yctp-jpg.360844

Kikosi kamili cha Yanga leo
 
Yanga 3. T p Mazembe 1. Nina uhakika wa 100% yanga lazima ashinde. T.P. Mazembe baadhi ya wachezaji nimeongea nao wana mgomo baridi hawajalipwa mishahara baada ya bosi wao Katumbi kupata matatizo ya kisiasa Congo . hawana ari kabisa

Wewe jifariji tu lakini kipigo kiko pale pale.

Hata kama Katumbi angekuwa amekufa kabisa kushindwa kuwalipa wachezaji ndani ya muda mfupi hivi ni ndoto.

Hayo mambo yako bongo tu kwenye soka la magazetini yaani Muro kawa maarufu kuliko Amis Tambwe na Kamusoko.
 
Naomba tupatiane updates za mechi iliomake headlines mjini. Nasikia watu wapo Taifa tangia alfajiri. Itasaidia watu kujipanga muda WA kwenda au kutokwenda kama uwanja utajaa mapema.
 
Kutoka Mbagara kwenda mjini kunafoleni sana watu wanatembea kwa miguu sijui uko mbele ya mataa ya karibu na chuo cha uhasibu kuna nini au ndo watu washaanza kwenda uwanjani?
 
Hakuna lisilowezekana chini ya JUA

............GO YANGA GO ...............hata tunune hata tucheke wao ndio wawakilishi wetu Tanzania, nakumbuka Mchezaji mmoja wa Kongo hii hii aliwahi kushangaa sana ati watanzania wanashangilia timu ya kigeni.....................na ninawaza pia jinsi uwanja wa Mazembe unavyoisheheni jezi tupu...........ukweli sitashangalia Mazembe wala Yanga ila nawatakia Yanga kila la heri kiroho safi kabisa na ninajua nasi yangu kwa matokeo yoyote yale ya leo
 
mleta mada alivyomnafiki wala hajui mechi ya kwanza Yanga alicheza timu kutoka Nchi gani go yanga gooo hii ni timu ya WANANCHI
 
Yanga ya TANZANIA inacheza na tp mazembe ya DRC hii inanifanya nielekeze nguvu zangu kuisapoti yanga
 
washabiki wa Yanga washafika uwanjani muda huu
 

Attachments

  • IMG-20160628-WA0003.jpg
    IMG-20160628-WA0003.jpg
    63 KB · Views: 206
Back
Top Bottom