Mechi ya wabunge v/s wakuu wa Wilaya

Mechi ya wabunge v/s wakuu wa Wilaya

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,252
Reaction score
10,248
Wakuu JF, Amani iwe nanyi.

Nimeona hii Taarifa ITV kuwa kutakuwa na Mechi kati ya timu ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya.
Muamuzi atakuwa Ndugu Reginald Mengi.
Madhumuni ya Mpambano huo ni kuchangisha Fedha kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino)
Mechi ya Kwanza itafanyikia Dodoma na ya Marudiano sijui itakuwa Dar?? (Kama sikosei)

MASWALI

Hivi Wakuu wa wilaya Posho zao na Madereva wao Ni shiling Ngapi kwa Siku??
(Namaanisha Kuanzia Posho na Mafuta ya Gari etc etc)
Hiyo Mechi inatarajia kuingiza Kiasi gani cha Fedha?? Hicho Kiasi kitaweza ku Counter cost za Wakuu wa Wilaya kutoka huko (eg. Kibondo)
Kuja Dodoma

Najua watu wengi hawatahudhuria Hiyo Mechi, kwanini hizo Gharama ndo wasizipeleke Huko kwenye Matumizi ya Albino??
Huku kutaka sifa kwingine Hakuna Tija For Real
 
Umefikiria vyema,kama kweli huwa tunachagua viongozi wanatakiwa waachane na upuuzi huo na kufanya kama ulivyosema
 
ingekuwa ya wabunge wa magaidi vs wenyenchi.nione rafu ya mbowe kwa mwiguru.teh tehteh
 
Source taarifa ya habari ya itv usiku huu,waratibu wa pambano hilo betty mkwasa na venance mwamoto,sipati picha itakuwaje katika pambano hilo,sentaafu ama beki namba tano wa wabunge ni godbless lema huku sentafowadi wa Ma-rc akiwa magessa mulongo
 
Wabongo bhana tuko serious na vitu vidogo vidogo visivyo na umuhimu tunaacha mambo yenye umuhimu na maisha yetu ya kila siku. Hawa jamaa ndio akina Magesa Mulongo???
 
Wabongo bhana tuko serious na vitu vidogo vidogo visivyo na umuhimu tunaacha mambo yenye umuhimu na maisha yetu ya kila siku. Hawa jamaa ndio akina Magesa Mulongo???

Michezo ni sehemu ya seriousness katika maisha,kufanyakazi tu si afya ya mwili ama akili,lakini lengo la pambano hilo ni kuunga mkono jitihada za waziri mkuu pinda dhidi ya vita vya mauaji ta albino,najua utauliza serikali ipo wapi jibu ni kwamba ili kufanikisha ni vyema makundi mbalimbali yakashiriki kwa mbinu tofauti
 
Mulongo atakuwa anakabwa na Lema...
 
wewe member wa rebel group wa kule zaire bado hujarudi kwenu. au mashariki wa zaire kuna network? hahahaaa hongera jf for your wide coverage . mpaka ma rebels wanakusoma hongera sana
ingekuwa ya wabunge wa magaidi vs wenyenchi.nione rafu ya mbowe kwa mwiguru.teh tehteh
 
Wakuu JF, Amani iwe nanyi.

Nimeona hii Taarifa ITV kuwa kutakuwa na Mechi kati ya timu ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya.
Muamuzi atakuwa Ndugu Reginald Mengi.
Madhumuni ya Mpambano huo ni kuchangisha Fedha kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino)
Mechi ya Kwanza itafanyikia Dodoma na ya Marudiano sijui itakuwa Dar?? (Kama sikosei)

MASWALI

Hivi Wakuu wa wilaya Posho zao na Madereva wao Ni shiling Ngapi kwa Siku??
(Namaanisha Kuanzia Posho na Mafuta ya Gari etc etc)
Hiyo Mechi inatarajia kuingiza Kiasi gani cha Fedha?? Hicho Kiasi kitaweza ku Counter cost za Wakuu wa Wilaya kutoka huko (eg. Kibondo)
Kuja Dodoma

Najua watu wengi hawatahudhuria Hiyo Mechi, kwanini hizo Gharama ndo wasizipeleke Huko kwenye Matumizi ya Albino??
Huku kutaka sifa kwingine Hakuna Tija For Real

Huenda watakuwa na Semina elekezi huko Dodoma na kisha kuwa na Mkutano na Waziri Mkuu hapa Dar es Salaam! Si unajua ofisi za nchi hii ziko nusunusu; kuna ambazo zipo Dodoma na nyingine Dar es Salaam!

Hapo kwenye wekundu nakumbuka kuna wakati Mengi alichezesha mechi ya wabunge sijui na watu gani basi ikatokea mtu amechezewa rafu katikati ya uwanja Mengi akapiga filimbi kuashiria ipigwe penalti. Walipomwambia Mzee hiyo haiwezi kuwa penalti yeye akasema "Mimi ndiye mwamuzi" penalti ikapigwa!
 
Back
Top Bottom