Mechi ya Barcelona na Sevilla kuhairishwa kuna kubwa la kujifunza

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,914
2,000
Jana nilikuwa nasubiri game ya Barcelona na Sevilla nikaona imehairishwa nikataka kujua kumetokea nini?

Katika kusoma sababu nikaona kwamba La liga waliomba chama cha mpira Spain ambao ndio kama TFF huku kufuta wiki hii ratiba ya game ya Barca na Sevilla sababu wachezaji wengi wamechelewa kurudi kutoka South America baada ya mechi za kufuzu kombe la dunia.

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Spain wakakataa kuahirisha mechi lakini La liga hawakuridhika wakaenda mahakama ya michezo sasa kwetu labda kama BMT hivi wakakata rufaa kwa bahati rufaa ikakubaliwa kuwa mechi ipangiwe siku nyingine, ndio maana mechi ile haikuchezwa wiki hii na game nyingine ya Villa real na Alaves kama sikosei, napia ku change muda wa game za wiki hii kidogo ikabidi mpaka ruhusa.

Naandika hii sio kwa sababu ya mechi hizi tu ila kuna la kujifunza kwa Bodi ya league yetu na TFF, kule kubadili au kuhairisha mechi tu ni drama sio jambo rahisi linapitia maombi na huwa linakataliwa labda kuwe na sababu za msingi sana kulinda heshima ya league kwa maana integrity ya mashindano.

Sasa huku kwetu nikikumbuka saa 8 tu watu wanabadili muda wa game mara kila wiki game zinawekwa viporo tu kwa matangazo ya vimemo tu hakuna kubanwa na sheria hebu tujifunze kwa hili la jana La liga na EPL hawa ratiba ikiwekwa imewekwa sio mtu anakuja tu na kubadili hakuna check and balance.

Kweli nimemini kitu bora kinajengwa na misingi bora ili league na mpira wetu uheshimike ni kujenga uaminifu kuwa league ya haki high integrity.
 

zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
7,161
2,000
Huku kwetu mtu anakuwa na viporo 23 wakati timu nyingine zimesha shuka daraja anakuja cheza nazo hapo kuna ushindani gani? Pumbavu T.F.F
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom