Mdudu gani huyu?

Mdudu gani huyu?

nsharighe

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
1,461
Reaction score
2,249
Nimekutana na huyu kiumbe nje ya Nyumba yangu jioni, hii namfananisha na Nungu Nungu japo Sina hakika.

Mwenye ufahamu na haya maswala ya wanyama na wadudu au Kama ni ishara yeyote anijuze.

Eneo naloishi si rahisi kwa kiumbe wa namna hii kuonekana, Naishi Dar Es Salaam Tabata na hakuna mapori

Ntanguliza Shukrani .
IMG_20221111_194015_650.jpg

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Wadudu wa kawaida hao hasa kipindi cha mvua huwa wanakaa kwenye vichaka au maua ya pembezoni mwa nyumba
 
Huku Mwanza wapo wengi sana hasa huu wakati wa mvua mvua na mara nyingi wanapenda kupiga misele mida ya giza giza......... Hana tatizo mwache asepe zake akale wadudu.
 
Nimekutana na huyu kiumbe nje ya Nyumba yangu jioni, hii namfananisha na Nungu Nungu japo Sina hakika.

Mwenye ufahamu na haya maswala ya wanyama na wadudu au Kama ni ishara yeyote anijuze.

Eneo naloishi si rahisi kwa kiumbe wa namna hii kuonekana, Naishi Dar Es Salaam Tabata na hakuna mapori

Ntanguliza Shukrani .View attachment 2413880

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Mmh
 
Huyu nikibahatika kumuona jioni kesho yake lazima nipige mpunga.
 
Mchomoe vimwiba vyake sita alafu chukua majivu, paka kwenye hiyo miba yake kisha mwambie karungeyeye usiye na baya na mtu nifikishie salamu zangu kwa mbaya wangu. Kesho muda kama huo ulionuiza utapata taarifa ya msiba, na huyo ambaye atakuwa amerehemika ndio mbaya wako.
 
singida wakati niko chuo walikuwa wengi sana usiku tukiwa tunaenda kupiga prepo tukiwa tunapita uwanjani
 
Anaitwa karunguyeye.

Wanapatikana kwa wingi sana Dodoma.

Na baadhi ya watu humla kama kitoweo
 
Back
Top Bottom