Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Najiandaa kufungua kesi mahakama kuu kwa hati ya dharura kuishtaki serikali kwa kutapeli pesa za wahanga wa tetemeko Kagera.
Nimesikitika sana baada ya serikali iliyovunja rekodi ya kukusanya mapato/kodi mpaka kuvuka malengo kukosa fedha za kujenga miundombinu ya serikali iliyoharibiwa na tetemeko Kagera na badala yake serikali imetapeli pesa ambazo zilichangwa na mashirika na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Kagera walioathirika na tetemeko hilo.
Yaani ni sawa na waumini kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa/msikiti halafu mchungaji au imam anachukua fedha hizo na kujengea nyumba yake binafsi wakati huo mchungaji au imam anapata posho ambazo angetumia kujengea nyumba yake, huo ni utapeli.
Nilitegemea serikali ingetumia pesa za serikali kujenga miundombinu kwa pesa za mfuko wa maafa ambazo hutengwa kila mwaka na serikali kwa ajili ya maafa.
Sikutegemea serikali kukosa fedha na badala yake kutapeli fedha zilizochangwa na mashirika na wananchi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenzao walioathirika na tetemeko hilo.
Na kama lengo la serikali ilikuwa ni hilo basi serikali ingekuwa wazi tangu mwanzo kwamba inaomba michango kwa ajili ya kurejesha miundombinu ya serikali na sio inaomba michango kwa ajili ya kuwasaidia wananchi walioathirika na tetemeko,huo ni ulaghai.
Utapeli huu wa serikali una utofauti gani na utapeli wa kuwaudhia watu dhahabu feki?mecury feki?.Nawaomba watanzania mniunge mkono nimedhamilia kwa hili ni lazima tufike mahakamani kwa kuwa mimi ni miongoni mwa watu waliochangia.
Mdude Nyagali
Sumu ya nyigu