Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 60
- 1,237
Baada ya mwenyekiti wa Chadema taifa kutangaza maandamano ya amani January 24, 2023 ilichukua dakika 40 tu kwa mkuu wa mkoa Dar kujibu maandamano hayo ya CHADEMA. Tena alilazimika kutumia madhabahu ya kanisa takatifu kujibu maandamano hayo kwa udharura.
Wakati tukiwa tunatafakari ushapu wa serikali kujibu/kuchukua hatua dhidi ya wapinzani wa serikali tunapigwa na butwaa kuona serikali hiyohiyo imeshindwa kuchukua hatua zozote za kukabiliana na maafa ambayo yametokana na mvua nyingi kunyesha jiji la Dar kwa siku ya pili leo. Pamoja na kwamba mvua hiyo imeharibu miundombinu ya serikali ikiwemo madaraja lakini bado serikali haijachukua hatua yoyote zaidi ya kukaa kimya.
Nilitegemea mkuu wa mkoa wa Dar angekuwa wa kwanza kutoa kauli ya serikali na hatua ambazo serikali ingechukua kukabiliana na maafa yanayotakana na mvua hiyo. Kwa bahati mbaya imekuwa tofauti RC huyo yupo yupo tu anazunguka na tumbo lake akisubiri mshahara na posho akamalizie ujenzi wa ghorofa yake. Ndio maana nasisitiza kuwa hizi nafasi ya ukuu wa wilaya na mkoa ni mzigo na hasara kwa serikali na ni zao la kuwa na katiba mbovu.
Nilitegemea nimuone waziri mkuu ambaye kitengo cha maafa kiko chini yake. Nilitegemea kuona Chopa ikiruka angani kusaidia wahanga waliokwama maeneo yenye mafuriko, lakini kwa bahati mbaya waziri mkuu yuko busy kupambana na makundi ya Urais . PM Katelefone anaamini Urais ataupata huko anakonyukana na wenzake na wala sio kwa wananchi, hii ni zao la katiba mbovu pia.
Nilitegemea ningewaona wabunge wa mkoa wa Dar wakiwa site na kufuatilia uwajibikaji wa serikali, lakini kwa bahati mbaya wabunge wako Dodoma na miongoni mwao wengine muda huu wako wanakula bia pale Dodoma hotel na hawapokei simu za wananchi wao waliokumbwa na maafa. Wanafanya hivi wakiamini kwamba ubunge wao unatoka kwa Rais na sio kwa wapiga kura ambao ni wananchi. Haya pia ni matokeo ya katiba mbovu.
Nilitegemea kumuona Rais akitembelea maeneo ambayo yameathirika kuwafariji na kuwatia moyo wahanga huku akiagiza vyombo vilivyo chini yake kuharakisha kurudisha miundombinu iliyoharibiwa kwa udharura. Kwa bahati mbaya Rais yuko busy kwa Askofu Malasusa akitafuta sifa ambazo hastahili. Rais anaamini hata wananchi wasipompigia kura yeye bado atarudi ikulu kwa nguvu za vyombo vya dola. Hili pia linatokana na katiba mbovu.
Hivyo basi kutokana na mapungu hayo maandamano ya tarehe 24 January 2024 ni muhimu mno kwani hiyo ndio njia pekee ambayo inaweza kuleta matokeo ya viongozi wa serikali kuheshimu wananchi. Nategemea wahanga wote wa mafuriko tutaonana barabarani siku hiyo tukiimba nyimbo za ukombozi kuelekea ofisi za Umoja wa Mataifa.
Lazima tutumie kila njia kuweka misingi bora ya nchi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.