Mdee uko wapi? Viwanja vya Madale walalahoi wanadhulumiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdee uko wapi? Viwanja vya Madale walalahoi wanadhulumiwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanaharakatihuru, Aug 17, 2012.

 1. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana na mkuu wa mkoa wa dar es salaam kwa kutoa kauli ya dharau namna hiyo eti kuna vijana elfu moja wanaovamia maeneo ya watu madale na kujitwalia kutoka kwa wamiliki halali wa mashamba yao ili hali twajua kabisa ni mpango mzima wa mwenye nguvu mpishe.

  Mh Halima Mdee baada ya sikukuu ya IDDI tunakuomba uje jimboni kwako utueleze wanataka kutupoka eneo letu wapi nasisi tufanyaje kama wakuu wengine wanahatarisha haki yetu???
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na nyie mmezidi..si mrudi kijijini mapori kibao tu aaagh
   
 3. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante tutarudi
   
 4. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante tutarudi tatizo wamepewa ardhi yote wawekezaji wanalipa 220 kwa mwaka kodi
   
 5. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,402
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mbunge hayupo kwa ajili ya kutetea uovu,,mimi nimejitutumua kutafuta vipesa af ninunue eka kama 10 then nikiwa najipanga nakuta eti watu wamekaa na familia zao bila aibu.kuweni wastaarabu kama una hati miliki ya hiyo sehemu kaa kama hauna nyie ni wavamizi,matapeli mnaochelewesha maendeleo ya nchi sababu yawekuwa hayo maeneo yangekuwa yameendelezwa kwa makazi ya bei rahisi wananchi wakaishi nyie muombe msamaha tu na muombe mpewe muda mfungashe msisubiri kuaibishwa:
   
 6. peri

  peri JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  subirini mumuadhibu kwenye uchaguzi 2015.
  Ndivyo wanasiasa walivyo, hawatofautiani sana.
  Jaribu kuchunguza kdg, co wa ccm, cdm wala cuf.
  Wengi wametelekeza majimbo.
  Jaribu kuchunguza utajithibitishia mwenyewe.
   
 7. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa ndio utaona kwanini chura humnyima tembo kunywa maji hakuna fisadi atakaye shinda heka kumi wewe si fisadi mamae
   
 8. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,402
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hivi unafikiri kila mwenye hela ni fisadi?acha mawazo finyu wewe!azam utamwita fisadi ilhali unanunua juice na maji yake kila siku?nenda popote duniani utakuta kuna matajiri,daraja la kati na maskini,,wewe kutokuwa na uwezo usilazimishe kila mtu,for your information ukienda magu mza kuna sehemu unanunua heka ef 10,mtu sasa ashindwe kununua heka kumi?hebu waambie na wenzenu mtoke la sivyo kama mna hekima na najua wewe ni great thinker ndo maana upo hapa,waiteni mmiliki muwaombe msamaha na muwaeleze shida zenu na kuwaomba wawamegee hata a piece of land mkae sehemu nyingine mumuachie,sasa mtu kaweka investment kwa ajili ya watoto ama wajukuu za af mnang'ang'ania tu.fanyeni hivyo.
   
 9. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  halima tulikuita kabla ya leo lakini umetutelekeza
   
 10. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Angalia damu inamwagika na wewe uliapa kuilinda, ndio ukaribu huu unaouhubiri??
   
 11. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,402
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  viongozi tunaowachagua ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wote,ila sio kuisapoti uovu wa aina yeyote.
   
 12. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,402
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  hapana usimsingizie mheshimiwa mbunge,hili suala litaisha mkuu,naomba nikuulize swali mkuu hapo unapokaa umepanga au ni kwako?na nani alikuuzia?ni either ulidhulumiwa kwa kuuziwa ardhi isiyo yako ama wewe ni mvamizi.
   
 13. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,455
  Trophy Points: 280
  tatzo nchi hii kisa mtu akionekana ni maskini akikutwa anabishana na aliyemzidi kipato basi watu lazima watamsema yule aliyemzidi kipato kuwa anamuonea masikini.
  Back to the topic, hao waliofukuzwa ni wavamizi na naweza waita wanyanganyi. Mfano mimi nilikuwa je ya nchi nikadunduliza vijisenti nikanunua kiwanja heka 14, nikajenga kibanda nikamweka mtu awe ananilinida akae pale na nikawa nikimtumia ela. Ajabu niliporudi tanzania nikakuta kajimilikisha bila aibu kama hanijui vile. Lakini bahati nzuri nilikuwa na hati ya hicho kiwanja. Kuwaondoa kwa nguvu tuliona si busara tufuate utaratibu lakini wakagoma kabisa ikabidi twende mahakamni na tukashinda still kuondoka wakagoma ndipo serikali ikafanya kazi yake.
  Acheni kusema mambo msiyo yajua mnalalamika sana jamani sa kwani kazi ya serikali si kutekeleza sheria. Wale wanyanganyi ni lazima waondoke au wewe ukinyanganywa kiwanja chako utakaa kimya
   
Loading...