Raisi wangu chonde chonde nakushauri uache udalali wa kupigia upatu biashara ya wazungu kutulisha sumu na chemical zao kwa ajili ya manufaa yao.Katika nchi yetu kubwa yenye nguvu ya <75% ni wakulima mashambani na ardhi ya kutosha zaidi ya hekta <4.million za ardhi kuna haja gani ya kurasimisha sumu.?
Wataalamu wa kilimo na ufugaji mpeni ushauri raisi wetu japo wakati mwingine mbishi na mbinafsi gharama na hasara ya mazao ya GMO ni kubwa kuliko faida yake kwa kpindi kirefu kwa uchumi na afya za taifa letu.Wazungu nia yao ni kushika na kucontrol uchumi katika sekta ya kuuza mbegu,mbolea vitu ambavyo mkulima wa kawaida hataweza kupata kwa wakati mwafaka.Jamani GMO itatupotezea mchele wetu wa kienyeji super wa Kyela,kilombero,kahama,chato,Musoma na shemu nyingi walizoea vyakula vya asili.
Raisi Kikwete siyo kweli kuwa njaa katika nchi maskini itaondolewa na GMO kama ambavyo wabinfsi wachache wanakudanya na kushauri. Muhimu katika nchi yetu hii ni kuwekeza kikamilifu na kuunganisha program na miradi mbalimbali ya kilimo kulingana na mazingira ya mkoa au Wilaya.