Mdee amlipua Pinda

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,060
309
WABUNGE WAGAWANYIKA,MBOWE AOKOA JAHAZI.

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemlipua hadharani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akidai ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu ambao wametajwa kuhusika katika kushinikiza ugawaji huo wa ardhi.

Mdee ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiwasilisha hoja binafsi inayolenga kuitaka Serikali kusitisha ugawaji wa ardhi kwa wawekezaji kutokana na hofu wanayoipata katika mazingira yasiyo halali ikiwamo kuwatumia vigogo serikalini.

Alisema katika baadhi ya maeneo nchini, uwekezaji umekuwa ukifanywa kutokana na shinikizo la viongozi wa ngazi za juu serikalini huku pia akiwataja wawekezaji waliogeuka kuwa ni matatizo.

Katika hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa upinzani na pomoja na wawili wa CCM, Lekule Laizer (Longido) na Dk. Faustine Ndugulile (Kigamboni), Mdee alitaka ugawaji ardhi kwa wawekezaji wa nje na ndani usitishwe hadi hapo tathimini ya kina itakapofanyika kubaini ni kiasi gani kipo mikononi mwa wawekezaji.

Hoja hiyo pia inataka tathmini ya kina ifanyike kuweza kubaini raia wa kigeni na wa ndani waliojipatia ardhi kinyemela kupitia Serikali za vijiji kinyume na matakwa ya sheria ya ardhi Na. 5 ya mwaka 1999.

Mdee alisema kwa muda mrefu kumekuwapo na uwekezaji usiokuwa na tija kwa taifa, hivyo akawataka wabunge kuunga mkono hoja yake ili kunusuru taifa. Alisema kumekuwa na ubabaishaji mkubwa katika sekta hiyo na kwamba katika mazingira mengine Serikali imekuwa kuwadi wa wawekezaji.

Mdee alisema inakadiriwa kuwa kati ya mwaka 2001 hadi 2010 kulikuwa na maombi ya wawekezaji kutaka ardhi zaidi ya hekta milioni 203 katika nchi zinazoendelea barani Afrika.

"Hii ni sawa na maombi ya hekta 55,616 kila siku katika kipindi cha miaka 10. Halikadhalika nchini Tanzania katika miaka ya karibuni takriban hekta milioni nne zimeripotiwa ‘kuombwa' na wawekezaji wa nje kwa kilimo cha mazao ya mafuta na chakula.

"Mheshimiwa Spika, ninaliomba Bunge lako tukufu, likubaliane na hoja ya kuitaka Serikali kusitisha ugawaji wa ardhi ili kuweza kutoa fursa kama nchi kuweza kujitahmini kwa kina, wapi tulikosea ili tuweze kujipanga upya kwa manufaa ya nchi na wananchi," alisema.

Hata hivyo, Mdee alisema hakuna anayepinga umuhimu wa uwekezaji, lakini ni muhimu vile vile ikaeleweka kuwa taifa haliwezi kuendelea kukabidhi kila kitu kwa wageni.

"Sote tunajua ni kwa namna gani dhahabu, almasi na Tanzanite zimetumika kujenga uchumi wa mabeberu! Hatuwezi kufanya makosa tena kwenye rasilimali hii muhimu ya ardhi inayopanda thamani kwa kasi sana. Uchumi hauwezi kuachwa uendeshwe na watu wa nje," alisema.

Kwamba kuna haja kubwa kwa wabunge kutambua kuwa matatizo ya ardhi yanayoikumba Rufiji, Kilombero, Bagamoyo, Kisarawe na Lugufu yanaikumba pia Muheza, Pangani, Katavi, Meatu, Kinondoni, Njombe na Ngorogoro.

"Maeneo mengi ardhi yanayochukuliwa na wawekezaji hao huwa hayaendelezwi kama inavyopasa na yale ambayo yanaendelezwa, yanaendelezwa kwa kiwango kidogo sana huku wananchi wengi wakiachwa pasi na ardhi ya kutosha kwa kilimo. "Katika hatua nyingine, wawekezaji baada ya kupata /kumilikishwa ardhi kwa bei ya kutupa, hawaitumii, wanasubiri ipande thamani, kisha kuiuza kwa faida kwa wawekezaji wengine," alisema.

Mdee alisema Kampuni ya kimarekani ya Agrisol imepewa eneo kubwa mkoani Rukwa linalohusisha hekta 80,317 (Katumba) na 219,800 ( Mishamo).

"Katika eneo hili majadiliano yanaratibiwa na viongozi wakubwa sana serikalini. Mradi huu umejikita kwenye uendelezaji wa mashamba makubwa na matumizi ya mbegu zenye viini tete (GMO). Kwa upande wa Mkoa wa Kigoma, alisema maeneo makubwa ya ardhi yameuzwa kwa kampuni za AGRISOL na FELISA. Alisema FELISA amenunua ekari 3,000 katika Wilaya ya Uvinza Kijiji cha Basanza Kata ya Uvinza.

Wawekezaji hawa wamewakuta wakulima na wafugaji katika maeneo haya. "Mwekezaji wa AGRISOL amepewa hekta elfu 10,000 eneo la Lugufu. Eneo hili ndio ili kuwa kambi ya wakimbizi. Eneo hili ndio limetengwa kuwa makao makuu ya wilaya," alisema.

Mdee alifafanua kuwa kwa kuwa rasilimali ardhi ndio urithi pekee wa asili ya Mtanzania katika kujitafutia riziki na kuendesha maisha yake uwekezaji katika ardhi unaofanywa na makampunicya nje haujawasaidia wananchi kwa maana ya fursa za ajira na upatikanaji wa chakula, analiomba Bunge liazimie kusitiza ugawaji huo. Baadhi ya wabunge waliochangia waliunga mkono hoja hiyo, huku wakisema kuwa migogoro ya ardhi ni tatizo sugu nchini na kwamba limetokana na kiwango kidogo cha ardhi kilichopimwa.

Laizer katika mchango wake alisema suala la ardhi halina itikadi ya kichama, hivyo akawataka wabunge wenzake kuunga mkono hoja hiyo ili kutoa fursa kwa taifa kujipanga na kufanya tahimini upya. Naye Waziri wa Mahusiano, Steven Wassira, alisema kuwa anakubaliana na hoja ya Mdee ya kufanya upya tathimini huku akisisitiza kuwa wakiendelea na mfumo uliopo ambao umejaa rushwa, watabaki bila ardhi.

"Huko kwenye ngazi ya vijiji, kuna watu wanapigwa rushwa kijiji kilichokaa kupitisha ardhi kina majina ya marehemu na sahihi zao mimi nafanya kazi Ikulu haya mambo yapo," alisema Wassira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk. Mary Nagu, naye alisema kuwa hawawezi kukataa wawekezaji ambao wanafuata taratibu huku akisisitiza kuwa wapo wasio matapeli. Hata hivyo, kabla ya hoja ya Mdee haijafanyiwa mabadiliko na kupita, Waziri wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka, aliomba azimio hilo libadilishwe badala ya kusitisha ugawaji ardhi ibaki hoja ya kufanya tathimini tu ambayo itabaini wawekezaji wa raia wa kigeni waliojipatia ardhi kinyemela.

Kauli hiyo ilizua mjadala kwa wabunge wa upinzani wakikataa huku wale wa CCM wakiunga mkono. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) aliungana na Mdee akisema kuwa hoja ya kusitisha haihitaji fedha ila tathimini ndiyo inayohitaji fedha.

"Ukiruhusu tathimini wakati bado unaendelea kugawa ardhi, utakuta umegawa yote. Halima alikuwa muungwana hakusema wawekezaji wanyang'anywe," alisema.

Msimamo huo wa Zitto ulionekana kuungwa mkono na wabunge wengi wa upinzani huku mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka aliyekuwa akiungwa mkono na wenzake wa CCM alipinga hali ambayo iliendelea kuzua mjadala. Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge) William Lukuvi, alilazimika kusimama akisema serikali inaunga mkono hoja hiyo na kwamba kama wangekuwa hawaiungi mkono wangekataa kwani kanuni inawaruhusu.

Lukuvi aliwataka wabunge waunge mkono hoja ya kufanya tathimini tu na kuasa kuwa endapo watasimamisha ugawaji ardhi kuna watu watakwenda mahakamani na kuhoji kwanini wanataka kujifedhehedha. Mbowe aokoa Jahazi Hata hivyo baada ya kauli ya Lukuvi, bado wabunge walionekana kutokubaliana, hali iliyomlazimu Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kusimama na kuokoa jahazi.

Mbowe aliwataka wabunge wote wakubali mapendekezo yaliyowasilishwa na Waziri Tibaijuka na kupendekeza tathimini tu ifanyike na kuiagiza serikali iilete bungeni Aprili kisha bunge lione mambo gani yafanyike. Ushauri huo wa Mbowe uliungwa mkono na Waziri Tibaijuka katika kauli yake na kumshukuru kwa kuwasaidi.


Source tanzania daima ijumaa.
 
huyuy mama bora angebaki hukohuko UN...ukishakuwa ccm basi ujue na wewe mchafu hata kama hupigi milungula directly,kama unaspoti mfumo wa sasa ambao ni mbovu na unanuka basi na wewe ni sehemu ya tatizo..
 
nyabhingi Hapana prof tibaijuka yuko sahihi, alichosuggest mdee ni dhana ya kufikirika haitekelezeki,huwezi stopisha miradi ya uwekezaji wa ardhi nchi nzima utaharibu the whole system na huwezi kuremedy.

Kuna miradi kibao iko kwenye process ukiistopisha then unasubiri tathmin ambayo hujui itafanyika na kukamilika lini kutokana na kutokuwa na rasilimal fedha.

Alimaanisha land delivery isimame kwa miaka kadhaa,so in the mean time kutakuwa kunafanyika nn? Hili ni swala linalohijaji reformation ya awamu, may b wangeanza na tathmin ya kanda lakin wakiwa wamejipanga kifedha na utaalamu.

Wizara ya ardhi na hata manispaa zina watendaji wachache kwa maana ya wataalam wanashindwa kuajiri kutokana na kutokuwa na rasilimal fedha za kutosha sembuse kufanya quick reformation kwenye hiyo miradi na proces nzima ya jinsi service ilivyotolewa.hakuna sababu za kukurupuka kama wanataka desirable results mbowe aliliona hilo na ndo mana akasema vile.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Nagu naye anajali wawekezaji tu bila kujali EIA ya maeneo na jinsi wananchi watakavyoathirika. Bora angebaki huko Hanang.
 
Magazeti mengi ya leo yana taarifa kuhusu waziri Mkuu Pinda kuchoka kujibu maswali ya Kafulila na kuomba Kafulila kuacha kumkoromea.

Jambo baya na la kihuni ni Pinda kushindwa kujibu hoja ya msingi na nzito ambazo Kafulila alikuwa akiomba ufafanuzi wake akiwa kama Waziri Mkuu.

Majibu mepesi ya Pinda kuwa Kafulila ni Diwani pia na kwamba hoja hizo zinaweza kumalizwa na Halmashauri ya Kasulu ni hoja DHAIFU kabisa.Kwa mujibu wa SHERIA za Uwekezaji ya 1998 na nyinginezo kama za EPZ na ESZ Halmashauri hazina nafasi yoyote ya kutengua au kujadili au kukusanya kodi kwenye taasisi zote zenye kupitia uwekezaji wa TIC ,EPZ,ESZ na kupata registration au leseni.

Kwa muktadha huo ni vema PINDA angekuwa muelewa na kujibu kwa hekima kuliko kutaka kuonekana yeye ni zaidi kwa Kafulila bila kutumia busara.

Ni wazi makampuni yaliyojimegea ardhi maeneo ya Uvinza ni wawekezaji kupitia TIC na Pinda ANAJUA ILO, TATIZO NI KUWA PINDA KACHOKA KUWATUMIKIA WATZ KUWA WAZIRI MKUU SASA AACHWE ARUDI KWAO KIBAONI AKALIME MAHINDI.
 
...Inawezakana. Kuna wakati Mkulu kama hayupo Vile. Kuna wakati kulikuwa na masuala muhimu sana yaliyokuwa yakilitikisa Taifa na tulitegemea Mkulu atoe Tamko lakini akawa kama hayupo vile...! Kulikono?
 
Siyo tu Pinda peke yake hata JK mwenyewe amechoka anasubiri siku zake ziishe asepe.

Huyu Pinda baada ya JK "kushinda" awamu ya pili aliomba apumzike u-PM amechoka. Lakini nasikia JK akambembeleza hadi akakubali. Sasa mtu aliyekwisha sema amechoka unataka afanye nini? Yuko hapo (PM) to buy time siku zake ziishe asepe.

Vijana ni hazina ya Taifa hili, hawezi kwenda sambamba na spidi za vijana kama akina Zitto, Kafulila, Machari, Nassari, Mdee, Wenje, Lugola, Filikunjombe, Bulaya etc.
 
Bobuk inawezekana approach zake kwenye issues unaona kabisa he is a liability to the nation.
 
Last edited by a moderator:
Magazeti mengi ya leo yana taarifa kuhusu waziri Mkuu Pinda kuchoka kujibu maswali ya Kafulila na kuomba Kafulila kuacha kumkoromea.

Jambo baya na la kihuni ni Pinda kushindwa kujibu hoja ya msingi na nzito ambazo Kafulila alikuwa akiomba ufafanuzi wake akiwa kama Waziri Mkuu.

Majibu mepesi ya Pinda kuwa Kafulila ni Diwani pia na kwamba hoja hizo zinaweza kumalizwa na Halmashauri ya Kasulu ni hoja DHAIFU kabisa.Kwa mujibu wa SHERIA za Uwekezaji ya 1998 na nyinginezo kama za EPZ na ESZ Halmashauri hazina nafasi yoyote ya kutengua au kujadili au kukusanya kodi kwenye taasisi zote zenye kupitia uwekezaji wa TIC ,EPZ,ESZ na kupata registration au leseni.

Kwa muktadha huo ni vema PINDA angekuwa muelewa na kujibu kwa hekima kuliko kutaka kuonekana yeye ni zaidi kwa Kafulila bila kutumia busara.

Ni wazi makampuni yaliyojimegea ardhi maeneo ya Uvinza ni wawekezaji kupitia TIC na Pinda ANAJUA ILO, TATIZO NI KUWA PINDA KACHOKA KUWATUMIKIA WATZ KUWA WAZIRI MKUU SASA AACHWE ARUDI KWAO KIBAONI AKALIME MAHINDI.

Uwezo wake mdogo sana, ukilinganisha na nafasi aliyonayo
 
Siyo tu Pinda peke yake hata JK mwenyewe amechoka anasubiri siku zake ziishe asepe.

Huyu Pinda baada ya JK "kushinda" awamu ya pili aliomba apumzike u-PM amechoka. Lakini nasikia JK akambembeleza hadi akakubali. Sasa mtu aliyekwisha sema amechoka unataka afanye nini? Yuko hapo (PM) to buy time siku zake ziishe asepe.

Vijana ni hazina ya Taifa hili, hawezi kwenda sambamba na spidi za vijana kama akina Zitto, Kafulila, Machari, Nassari, Mdee, Wenje, Lugola, Filikunjombe, Bulaya etc.

Ukimsikiliza mwanasheria mkuu...safari ya kupata uhuru wa Tz kutoka mafisadi itapatikana kweli kwa dola hii....

NAWASALIMU WAKUU..!
 
Kuna baadhi ya maeneo katika nchi hii watu Hawthamini kabisa ardhi!! Kama Bagamoyo, Rukwa na Kwingineko!! Usitegemee Kama watajali sana hata ardhi yote Ikitolewa Bure!!
 
Siyo tu Pinda peke yake hata JK mwenyewe amechoka anasubiri siku zake ziishe asepe.

Huyu Pinda baada ya JK "kushinda" awamu ya pili aliomba apumzike u-PM amechoka. Lakini nasikia JK akambembeleza hadi akakubali. Sasa mtu aliyekwisha sema amechoka unataka afanye nini? Yuko hapo (PM) to buy time siku zake ziishe asepe.

Vijana ni hazina ya Taifa hili, hawezi kwenda sambamba na spidi za vijana kama akina Zitto, Kafulila, Machari, Nassari, Mdee, Wenje, Lugola, Filikunjombe, Bulaya etc.

Wakuu ukisha chaguliwa kuwa PM katika hizi nchi zetu na kwa mfano serikali hii ya TZ unaweza achia madaraka ndani ya mwezi tuu kuna uozo wa hali ya juu na siasa za juu za kinafiki na unaweza hata vaaa bomu ukalipue hata BUNGE lote hadi IKULU kuna viongozi wengine wanafanya miradi tuu humo na sio kuiongoza serikali

 
Kweli rushwa imeimaliza nchi, yaani watu wanajichukulia tu. ngoja na Mimi nikawahi la kwangu huko kujijini kwa pinda ili baadae nimuulie pinda mwenyewe maana asiyejua thamani ya dhahabu ukimpa kinachong'ara anapagawa. Hii miaka 20 ya MKP na Kiwete ardhi imetolewa kama peremende. Loh! AMA kweli kwa sasa sentensi ya JK kwamba ndani ya CCM hata kama atachagulia kichaa bado ataendelea kuwa kiongozi hadi mwisho wa uongozi wake no matter what happens!. Kweli tumekoma. Wenye masikio tulikusikia.
 
Back
Top Bottom