MDC ya Zimbabwe yasherehekea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MDC ya Zimbabwe yasherehekea

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, Mar 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wabunge wa Zimbabwe wamemchagua tena mshirika wa karibu wa waziri mkuu Morgan Tsvangirai kuwa spika wa bunge baada ya uchaguzi wake wa 2008 kufutwa.

  Lovemore Moyo kutoka chama cha MDC alipata kura 105, na kumshinda mgombea kutoka chama cha Zanu-PF cha Rais Robert Mugabe ambaye alipata kura 93.

  Kura katika bunge hilo lililkuwa na utata kufuatia madai ya rushwa na kukamatwa kwa baadhi ya wabunge wa MDC.

  Zanu-PF na MDC waliunda serikali ya umoja miaka miwili iliyopita.

  Lakini wasiwasi unaongezeka tena kabla ya kuwepo uwezekano wa kufanyika uchaguzi mwaka huu.

  Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesihi viongozi wa majimbo kuishinikiza Zanu-PF kuacha kwa kile walichoita usumbufu na ukamataji holela wa wapinzani wa kisiasa.

  Wito huo umetolewa kabla ya mkutano wa jumuiya za kimaendeleo wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika siku ya Alhamis.
   
Loading...