Where did you get that "perfect" from?Nobody is perfect 100%,
alipoona akili imechoka ndo mana alipoona akili imechoka kaamua kung'atuka wengine waendelee.
Alikuwa navmapungufu mengi mno, na yanakuwa mengi zaidi ukimtazama kwa miwani ya SASA,
Kwanza alipata nchi ikiwa na wajinga milioni 10 tu! Yes, i mean wajinga, illiterate, unskilled stupid, ilibidi Nyerere aweke mpaka wahindi kwenye baraza lake la mwanzo la mawaziri ili angalau kuwa na watu wawili/watatu wa kushauriana nao, hawakutosha,,akalazimika kuweka hadi wakina kawawa, sasa kwenye industrialization huwezi kusema hakufanya chochote mkuu, Pamoja na kuzungukwa na umasikini,ujinga, na madhara yaliyobaki baada ya ukoloni lakini alijitahidi kujenga viwanda vingi ambavyo mtu yeyote angetegemea viwe constructive overtime, lakini viwanda hivyo viliuliwa mara tu alipotoka madarakani, vingine vilibinafsishwa kihuni mbele ya macho yake, ulikuwa na miaka mingapi wakati nyerere alipokuwa anaitetea NBC isiuzwe kihuni? Hadi chozi likamtoka na hakuna aliyemsikiliza, nbc ikauzwa!! Kuna record ndefu ya viwanda,biashara na taasisi zilizokufa baada tu ya Nyerere kutoka madarakani kuliko vilivyoanzishwa baadae, niambie, mwinyi kajenga viwanda vingapi? Mkapa vingapi? Kikwete? Magufuli alitujengea viwanda vya matofali na juisi ya miwa nk, viwanda 28,000 alivyovijenga magu labda amekufa navyo, ila vya nyerere hadi leo vipo na vinaonekana, japo hawa mafisadi wenu waliviulia mbali ili wapate 10% kwenye uagizaji wa bidhaa kutoka nje ila bado vipo, na vinawasuta,give credit when its due.
WatuIli tuendelee tunahitaji vitu vinne
WATU
ARDHI
SIASA SAFI
UONGOZI BORA.
JK Nyerere aling'atuka back 1985. Miaka 40 baadae bado tunahangaika na Ujinga, Maradhi na Umaskini
Ndo maana akiwa Mbeya Uwanja wa Sokoine alirejelea Kauli ya JF Kenned- Rais wa Marekani. Think what you will do to your Country!...habari ya kulalamikia mapungufu yake ni Upumbavu.Watu
Ardhi
Siasa safi
Uongozi bora.
Was he right or not?
Kuna sehemu pia alisema, ili kijana alete maendeleo kwa taifa inabidi awe na
Malezi bora.
Bongo kali.
Siha njema.
For me he was right kwa kipindi chake.
Tusipindishe maneno, leo yetu tunatakiwa kuipambania wenyewe, 40yrs bado lawama kwake?
Fikiria mtu kama Samia au Kikwete angekuwa Rais wa kwanza akadumu miaka 24. Hii nchi ingekuwa katika hali gani?Ukoloni Bado wa akili Bado unatutesa wa Africa.
Tunalaumiana sisi kwa sisi, ndio amekosea na alikiri hadharani Kuwa amekosa .
Sasa sisi kizazi tulichofuata baada ya yeye tulichukua mazuri yake na kuacha mabaya ?
Au tuliacha mazuri yake na kuchukua mabaya.
Basi sisi tutakuwa ni wapumbavu zaidi yake
Huyo Dogo anajiamini nini labda???
Na hiyo Ndio shida kubwa ya watu wasio civilized.Fikiria mtu kama Samia au Kikwete angekuwa Rais wa kwanza akadumu miaka 24. Hii nchi ingekuwa katika hali gani?
Labda mke, mtoto, mkwe angemfuata kuwa Rais na wangemiliki nusu ya Tanzania familia zao.
Katika pita pita zangu kwenye mitaa ya YouTube, nimekutana na video ya Rais Julius Nyerere akiwa New Delhi, India, akipokea tuzo.
Ilikuwa mwaka 1982.
View: https://youtu.be/aGHLfV4S3CM?si=y1MsBA83j5P1y4p0
Kwenye ukurasa wa mabandiko wa chaneli ya mwanahistoria Adeyinka Makinde, kuna mdau katema nyongo dhidi ya Nyerere. Kamchana sana.
View attachment 3486237
Haya hapa maoni ya huyo mdau:
View attachment 3486248
Julius Nyerere alikuwa janga kubwa kabisa kwa Tanzania na kwa bara la Afrika kwa ujumla. Ni kichekesho cha aina gani cha mtu ambaye, baada ya kushuhudia ukatili wa kinyama uliofanywa na Wazungu dhidi ya Waafrika kwa kutumia teknolojia yao ya juu, angeamua kuacha juhudi za kuharakisha mapinduzi ya viwanda — jambo ambalo lingewapa uwezo wa kujitegemea hata katika ulinzi wa taifa?
Bila shaka, Julius Nyerere alihitaji sababu fulani ya kuhalalisha itikadi yake isiyo na msingi ya Ujamaa wa kimarxisti, akiamini kwa upumbavu kwamba dunia ya kimarxisti iliyoendelea, ambayo ilipitia mateso makubwa kufikia maendeleo ya viwanda, ingewaruhusu yeye na watu wake kuendelea kutegemea bidhaa za viwandani kutoka kwao milele kama vimelea.
Hii ni fikra ya ajabu kabisa — wazo potovu kwamba Waafrika wanaweza kuacha maendeleo ya viwanda na badala yake kuunda aina fulani ya ushirikiano na mataifa mengine — ndilo chanzo kikuu cha hali ya sasa ambapo hakuna nchi hata moja ya Kiafrika yenye uwezo wa kiteknolojia wa asili unaofikia ule wa Korea Kaskazini. Matokeo ya upumbavu huu yamekuwa ya kusikitisha mno, na huenda yakaleta maafa makubwa zaidi siku zijazo.
Kwa sababu hiyo, Wana-Tanzania na Waafrika kwa ujumla wangepaswa kumlaani mtu huyu hata akiwa kaburini.
https://www.youtube.com/post/Ugkx9w...gyPRvKcfoS8AVZMxZ54AaABAg&si=SX342uvhHt1eeShY
Ukiachilia mbali ukali wa lugha yake, binafsi naona jamaa ana hoja yenye mashiko.
Nyie mnaonaje?