MkikiMkiki2015
Member
- Jul 2, 2015
- 20
- 23
- Thread starter
- #21
Asante
Mimi nataka kujua wamefanya nini kwenye nafasi zao mpaka sasa (i.e. watuambie mafanikio yao kila mmoja - vitu gani vipya walivyovifanya baada ya kuchaguliwa kuwa viongozi - maana wawili ni manaibu mawaziri; na mmoja ni mbunge). Pia watuambie wana vision gani (2015-2025)? - wanataka waipeleke Tanzania wapi? Maana naona wagombea wengi wanasema tu wanagombea ili kutoa foleni Dar es Salaam; wengine wanagombea tu sababu waliambiwa 2005 kuwa wataachiwa kijiti. Watanzania tunataka zaidi ya hapo - haswa kwenye maswala ya uchumi. Ni kweli wataweza kutupeleka kwenye uchumi wa kati? Na wakishidwa baada ya kuchaguliwa tuwafanye nini? Maana siku hizi kuna technology tutawarekodi hayo wanayosema sasa - halafu baadae tuone kama kweli wameyatekeleza.