Mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Bukoba mjini unaendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Bukoba mjini unaendelea

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Oct 19, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wana JF sasa hivi kuna mdahalo unaendelea Bukoba katika hotel maarufu ya Kolping. Sijajua ni nani ame organise mdahalo huu lakini wagombea wengine wa CCM na CUF hawajahudhulia kwenye mdahalo huo. Lakini ni mbunge wa Chadema ndiye aliyehudhulia tu.
  Ninasikia kupitia redio ya Kasibante inayomilikiwa na Hamis Kagasheki mgombea wa CCM
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Naona mgombea kaulizwa kuhusu suala la elimu bure.
  Anajibu kuwa hili linawezekana kwa sababu ni sera ya chadema kutokana na raslimali. Anasema kama yeye alisoma bure wakati nchi ikiwa haina raslimali zote zilizopo leo hivyo linawezekana
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna swali kuwa watu wamechoka na ahadi. Sasa kama yeye ambaye amewahi kuwa mbunge na mtumishi wa serikali anaweza kusema huko nyuma aliwahi kufanya nini?
  Anajibu kuwa yeye ndiye mwasisi wa ujenzi wa barabara za lami hapa Bukoba. Alipingana sana na utaratibu wa kuweka vifusi maana kulikuwa ulaji mwingi. Mkuu wa mkoa wa wakati ule alikubaliana naye na alisimamia hilo na leo mambo ni mazuri
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna swali kuwa yeye ndiye alianzisha sera ya (bana bashome) yaani "watoto wasome"
  Yeye anajibu kuwa yeye alipata mawazo ya elimu kwa watoto wote hata kabla haijawa sera ya ccm na sasa hiyo ndiyo wanayotumia kunadi sera zao bila kujua kuwa hayo yalikuwa malengo yake yeye na alianzisha mradi wa kusomesha watoto kwa kuchangisha pesa za kujenga shule za sekondari za kutwa mjini
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna muuliza swali anauliza vipi mgombea aliwahi kushiriki katika michezo akiwa mbunge na hata alipokuwa si mbunge
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna anayeuliza swali kwamba je mbona wananchi wa Bukoba hawana haki sawa ya kutumia chombo cha utangazaji cha Kasibante ambayo ni redio ya Kagasheki
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna anayeuliza je atasaidiaje katika upatikanaji wa viwanja vya ujenzi mjini?
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna swali kuwa je atafanyaje katika kudumisha demokrasia ya uchaguzi baada ya kuchaguliwa kwenda bungeni?
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swala la uchaguzi anajibu kuwa kukiwa na udanganyaji wapige simu na atashughulikia.
  Kwa redio anasema ipo kisheria na ni biashara huru lakini anasema redio itajifuta yenyewe kwa kukosa watangazaji kama itatangaza mambo ambayo hayana maana
  Kuhusu michezo anasema yeye binafsi alikuwa mchezaji na akiwa bungeni alikuwa akicheza namba tatu. Kulikuwa na kombe lililokuwa likijulikana kama jimbo cup. Lilianzishwa na mbunge wa zamani Kataraiya na hajui kama linaendelea. Hata hivyo anasema alikuwa akisaidia vijana wengi katika nyakati zake lakini kama kawaidia ya maadili huwa hatangazi kila analotoa katika vyombo vya habari.
  Kuhusu viwanja anasema atalishughulikia na zaidi ataanzisha kamati itakayoshauri hata wale wali karibu na mjini wanaotaka kuuza viwanja vyao waviuze kwa bei nzuri ya faida. Anakazia kuwa kuna mpango wa UN habitant kuhusu mji wa Bukoba aliouacha wakati akiwa mbunge na anaamini ulikuwa ni mpango mzuri ambao atahakikisha unafanyiwa kazi.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kutoka kwa mlemavu kuwa atwasaidia vipi walemavu maana huwa hawapati msaada upande wa elimu na afya
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu vyanzo vya maji. Muulizaji anasema zilitolewa sh milioni 130 kufidia watu ili watoke katika maeneo yao ya asili yaliyobainishwa baadaye kama vyanzo vya maji. Kwa sasa wamelipwa sh milioni 47 na bado wanadai sh.90 milioni je atawasaidiaje kupata malipo yao?
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuna swali la afya kwamba atawasaidia vipi maana wanapata shida sana wanapokwenda hospital kwa kukosa sh 5000 za kuchangia.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  safi sana MF

  yaani huku lindi nakupata kama nakuona

  hao wengine wa cuf sijui na chama gani kingine wameshakubali matokeo.
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu barabara mbadala baada ya kupanua uwanja wa ndege na fidia kwa wale ambao nyumba zao zinaharibika tokana na baruti zitumikazo kutetengeneza uwanja wa ndege
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Anajibu kuhusu uwanja kuwa ni janga la kata ya Kashai kwa kuwa uwanja umejengwa bila kufanyiwa utafiti. anahidi kuwa atahakikisha walioharibikiwa watalipwa fidia.
  Na kwa sasa hakuna jinsi ya kufanya ni kuhakikisha barabara inayotumika sasa ipanuliwe mara mbili au tatu maana hakuna jinsi ya kuhamisha investment ya uwanja ambayo pia ni kubwa. Anadhani ni vizuri serikali ikubali kulipa fidia kwa wenye nyumba zilizo pembeni mwa barabara ili njia hiyo ipanuliwe.
  Lakini pia anafilia kuwa barabara nyingine iendayo kilima hewa ipanuliwe kwa kiwango cha lami.
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuhusu walemavu anaelezea sera ya walemavu kama ilivyo katika ilani ya chadema
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu wanafunzi kushindwa kusoma katika shule ambazo ziko pembeni mwa uwanja wa ndege tokana na baruti na kelele za ndenge je atawasaidiaje wananchi wa kata ya Kashai?
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu uwepo wa bus stand yenye hadhi ya kutosha manispaa ya mji wa Bukoba?
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu kulipia mita ya maji atasaidiaje kupunguzia watumiaji wa maji gharama hizo?
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Swali kuhusu viwanda kwamba kuna umeme ardhi na maji lakini hakuna viwanda na ajila hakuna. Viwanda vilivyopo ni vile vya zamani vya kahawa abavyo hata uzalishaji wake umeshuka.
   
Loading...