Mdahalo wa vijana- Nshamba Muleba

Omulangira

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
230
29
Wapendwa makamanda, wapambanaji na wapenda mabadiliko ya nchi yetu. Vijana wa CHADEMA wa Tarafa ya nshamba, Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera wanaandaa mdahalo mkubwa utakaofanyika Nshamba mjini kwenye ukumbi wa Bantu tarehe 21/12/2012. Mada itakuwa ni (Maandalizi ya vijana kuelekea uchaguzi mkuu 2015).

Mnaalikwa kuandaa presentation ya mada hii tajwa hapo juu kwani tunahitaji watu angalau 4 wa kutoa presentation kwa ajili ya kuwaasa vijana.
Lakini pia vijana wanahitaji majembe kama matatu kutoka ngazi ya kitaifa kwa ajili ya kuongeza hamasa zaidi kwa vijana na wanajamii ya Muleba. Tunategemea baada ya mdahalo pia ipigwe mikutano ya hadhara kwenye maeneo 3 tofauti.

Tunakaribisha michango yenu ya mawazo, hali na mali na tusaidieni ni kwa jinsi gani tunaweza kupata majembe kutoka ngazi ya taifa na logistics zote za kuwapata.

Wasalaam
 
Vipi mkuu ili zoezi lilifanyika.Hii habari nimeipata baada ya Ku-Google.
 
Back
Top Bottom