Mdahalo wa katiba ITV

Mdahalo wa katiba ITV

Mbona mnabagua mtu wa Pemba??
Wabara tuna ubaguzi sana!
 
Mamaaaaaaaaaaaaaaaaa mpemba katamka live Watu wa bara hatupendwi na watu wa Visiwani,,,,,
 
duh! jamaa kumbe mzenji... anachekesha sanaa...
 
Hahahahhahaha nimecheka sana mkuu sio mchezo aisee....hahaha au sio upo chini ya mwembe......

Nina ka shamba kangu hapa Sungwi-Kisarawe ndio nilikua nimekuja! Vp upo mjini hapo nikubebee nazi na mananasi? Nimeshindia mananasi leo, safi sana naona mdahalo umetulia! Nafuatilia Mzee mwenzangu japo niko mbali na network niya manati
 
Rais wa Tadei kazomewa sana kwa kuimbwa ccm ccm ccm alikua anauliza je yanayozungumzwa na Jukwaa la Katiba linaifikia gvt?

aliuliza swali zuri tu, maana hata kama watazungumza kila siku kama hakuna kinachofika kwa wahusika haitasaidia. Watupe feedback ya kinachoendelea
 
hiyo ni matokeo ya mfumo mbaya wa elimu wa magamba mkuu,tunataka mabadiliko ili kubolesha hayo madahaifu..

Ni kweli mkuu, tunahitaji mabadiliko katika mifumo mingi sana inayomgusa mtanzania.
 
wamekosa kazi za kufanya.... Hii nchi ya wavivu tuu mpaka kiama. Mvua zimeanza kunyesha kwa nini msiende kulima tukaondokana na njaa. hivi kila mtu mwenye akili timamu angelima hekari moja ya mahindi au mpunga au zao lolote tungekuwa na njaaa... Kila siku mijadala mijadala...tumewachoka.. Kwanza mnatumia resources zetu bure..nyie vipi hamsomi alma za nyakti??

profesa wa kuzibua vyoo
 
Watanzania wanaonyesha isia zao ole wao wabunge kesho
 
Hata wizi wa ikulu inawezekana!

utabaki na mawazo hayo hayo..sisi tunasonga tu

CCM? labda kutuibia na kutudanganya kuwa kuna AMANI
Huoni wanachadema wanaojilipa per diem za 600,000 kwenye kila maandamano? Huoni mtu mmoja kwenye chama kinachohitaji kujijenga anajilipa mshahara wa milioni saba bila kodi?
Kuna wizi zaidi ya huu?
 
Yule Lifa Chipaka wengamsikiliza kwanza mwisho wake alikua anataka kusema nn maana nina amini sio CCM kama walivyokua wanamzomea.....aliuliza swali la msingi kama hayo yote wanayojadili yanafika mbele????sasa kabla hajamalizia wakaanza kumzomea hahaaaaa,inawezekana alikua ana point nzuri tu.
 
Yule mpemba ni kiazi sasa atajuta na maneno aliyotamka.......jazba mbaya sana aiseee.
 
Vipi mkono upo au wanatishiana tu? Wajiandae vizuri kesho ndio kesho, mbona mmepunguza spidi ya kuweka updates?
 
Back
Top Bottom