Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

......ama kweli.......ninamsikiliza...................THIS PERSON IS PRESIDENTIAL MATERIAL
 
Ameulizwa swali
Atasaidiaje kutokana na migogoro ya Aridhi mingi iliyopo,

Anasema, matatizo mengi ni kutokana na watendaji ambao wanaendekeza Rushwa, kwa mfano ufisadi ni mwingi sana na unasababisha migogoro,
Mfano , mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ni migogoro inayotokana na uzembe wa serkali, mfano wafugaji wa ‘barbari ‘ waliondolewa na serikali kwenye maeneo yao. Wakaachia, lakini serikali haikuwapatia mahali pa kwenda, serikali makini ni ile ambayo inamuondoa mfugaji alipo na kumepeleka mahala pengine pazuri.

Tatizo ni serikali kukosa umakini, wamelalamika sana hakuna anayewasilikiza, amesema pia wafugaji Wasukuma wanamatatizo yahoo hayo, na serikali haiwasaidii
Hapa kwa kweli ndio pa muhimu maana inapokuja suala la ardhi watu wanachinjana sana hasa wakulima na wafugaji
 
Dr anatoa ufafanuzi wa maslahi bora kwa watumishi wa umma na analiunganisha na suala la makazi. Anasikitishwa ha hali duni ya makazi ya watu; hivyo maadui wawili wanaandama nayo yaani maradhi na umasikini. Kodi kwenye cement na bati itaondolewa kuwawezesha watu kujenga nymb bora. Anatoa ufafanuzi wa kodi ktk eneo la Afrika mashariki.
 
Anasema alivyokua tanga, anashangaa hawajui nyumba za tembe. ukitaka kujuwa umasikini wa mtu tizama nyumba yake. bei ya simenti na bati atarudisha sh 5,000. vijana hawana matumaini ya kujenga. Tanzania tunalipa VAT 18%. Kenya wanalipa 15% na wana nyumbo nzuri.
 
Ni nini Serikali yake itafanyia watanzania wafanyakazi wa serikali na wa sekta binafsi baada ya kumaliza muda wao wa kazi

Dr slaa anasema, ukitaka kujua umaskini wa mtu tanzama nyumba yake, Chadema wamepita kila mahali na wamewaambia watanzania wakipewa Ridhaa wanaenda kuondoa kodi ya Cement na Bati, ili watu waweze kujenga nyumba, ametolea mfano wa waalimu, askari, machinga, mama lishe, vijana wasio na kazi nakadhalika, kwa kuondoa kodi wataweza kumudu ghalama hizo.

Anaongelea tamko la waziri kuwa akiondoa kodi italeta matatizo na nchi za Africa mashariki.
Anasema amemshangaa sana waziri, anasema Tanzania ina kodi ya juu zaidi kuliko nchi ya Kenya na Uganda,
Dr. Anasema yeye haendi kuwa Rais wa Africa Mashariki, anakwenda kuwa Raisi wa watanzania, hivyo atawatetea watanzania
 
anazungumzia suala la nyumba. anazungumza asilimia 80 wanaishi kwenye nyumba duni ama tembe.anazungumzia kutoa kodi kwnye bati na cement bei hiwe 5000.watu wanashangilia. anamshangaa dr kamala kuhusu kauli kutowezekana kushusha bei .anazungumzia tofauti za kodi wa EAC. anasema yy aendi kuwa raisi wa EAC.
 
yeye haendi kuwa rais wa afrika mashariki anakuwa rais wa tanzania,haendeshwi na afrika mashariki anaendeshwa na wananchi wa tanzania
 
ukienda shule unaondoa matabaka,ila leo hii kuna tabaka la maskini kama yeye na mimi,halafu kuna tabaka la kati,ametoa mfano wa wanafunzi wanaofaulu halafu wazazi wanashindwa kuwalipia,anaipa elimu kipaumbele,anasema bomu baya katika taifa ni kuweka matabaka
 
anazungumza ukweli mtupu,pls mpeni kura slaa am dying for him uuuwi nataka awe rais
 
Ahahahahahaaaaaah kasema tusipozingatia elimu eti hata walinzi watatoka nje!
 
anasema falfasa ya elimu ya bure. ukienda shule unaondoa matabaka ya matajiri na masikini. kuruhusu matabaka kunavunja umoja. leo elimu ya darasa 7 haina thamani. katika nchi 50 za africa kwa elimu Tz ni ya 47.
 
Ni report gani hiyo inayosema Tanzania ni nchi ya 47 kwa ubora wa elimu? Kama kuna mtu anayo naiomba.
 
hana mpya huyu labda tusubiri atazusha uzushi gani saa hii maana jamaaa kwa kuropokwa huyu


Tunakufahamu wewe ni Alqaeda na chuki zako za kidini. Dini imekupofusha macho, wakati wenzanko tunapambana na ufisadi na wizi wa maliasili zetu wewe uko kwenye jihad. Haya endelea!
 
Hehe jk huwa anajidai eti ameboresha elimu hasa ya msingi wakati Dr. Slaa anasema kwa viwangu vya elimu Tanzania ni ya 43 kati ya nchi 50 wadanganyika fungukeni mawazo...
 
Nasikia uchungu sana nikimsikia Dr. Slaa akielezea kiwango cha elimu Tanzania
 
Kamjibu yule aliyetumwa na JK kuwa eti suala la kodi lipo ndani ya mkataba wa Afrika Mashariki. Sijui huko Kamala alipo anajisikiaje.

nadhani ameshaanguka mara tatu na anaenda kwa sheikh yahaya kuloga ila akifika njiani ataanguka tena
 
Back
Top Bottom