mdahalo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu,

Saom

Member
Nov 27, 2011
5
0
habari wana JF?
Kutakuwa na mdahalo Wa wanafunzi wa vyuo vikuu utakaofanyika katika Chuo Cha Uhasibu(T I A).
Mdahalo huo utakuwa na mada isemayo;Kwa hali halisi ya TANZANIA Je kuna haja ya wanafunzi wa Vyuo vikuu kutumia Uniform?
SIKU:JUMAPILI;TAREHE 22/04/2012.
MUDA:SAA 8:00 MCHANA
MAHALI UTAKAPOFANYIKA:MAIN HALL
NJOONI TUCHANGIE HOJA.
KARIBUNI WOTE!
 
TIA ndio hiki huku Kilwa road? na je tuje na vitambulisho vya chuo?
 
hata o-level shuleni kwetu hatukuwahi kujadili mada ya kipu.uzi namna hii
 
hata o-level shuleni kwetu hatukuwahi kujadili mada ya kipu.uzi namna hii

wanaopemda kuoneshwa mbweche class utawajua tu! Wataanzisha mijadala ya kijinga wakijua kuna wajinga wengi wataenda kuwasapoti.
 
Nini kimewakumba nyie wasomi wa zama hizi?Kama nyie vijana wa Elimu ya Juu mnajadili mada nyepesi kiasi hicho, Kibasila Sekondari wajadili nini?
Inawezekanaje ,kati ya mambo nyeti yanayolikabili taifa muda huu, kama vile mchakato wa katiba mpya,mabadiliko ya Tabia Nchi,na Ufujaji wa Mali za Umma nyie mnaamua, kujadili mavazi...Hamjui kuwa mada za wasomi lazima zitofautiane na zile zinazoendeshwa na baadhi ya redio za FM?
Sasa ,mmeanza kuchezea hadhi ya usomi,tafadhali sana Matriculation Examinations irudishwe,
Nitashangaa sana mkipata wahudhuriaji.
 
Hii mada siyo ya kijinga! Mimi naona kwa mwendo wa wakuu wa vyuo, wanaweza kusema wanafunzi wote wavae uniform. Psychological implication ya uniform ni kuwadominate the subjects., kuwalazimisha kuwa humble, submisive. Mwanafunzi wa university anahitaji zaidi ya uhuru ku-explore nature!
 
habari wana JF?
Kutakuwa na mdahalo Wa wanafunzi wa vyuo vikuu utakaofanyika katika Chuo Cha Uhasibu(T I A).
Mdahalo huo utakuwa na mada isemayo;Kwa hali halisi ya TANZANIA Je kuna haja ya wanafunzi wa Vyuo vikuu kutumia Uniform?
SIKU:JUMAPILI;TAREHE 22/04/2012.
MUDA:SAA 8:00 MCHANA
MAHALI UTAKAPOFANYIKA:MAIN HALL
NJOONI TUCHANGIE HOJA.
KARIBUNI WOTE!
siku mtakayo jadili kuhusu hatma ya Tanzania, ukiliritimba wa HESLB, degree za kupeana kwa kufanya mapenzi na kuonga, kukomboa hii nchi, jinsi ya kujiajiri, namna ya kuwasidia wahitimu kupata mtaji wa kujiajiri, jinsi ya kuwashughulikia mafisadi, na kuwaadaabisha mawaziri ambao wengi wao ni wezi, niiteni nitakuja mapema hata kabla VC wenu hajafungua office na nitaacha kazi zangu
 
Hawawezi tena kujadili mada zekosoazo serikali kwasababu kama waki-organize mjadala labda juu ya ''USAHIHI WA MAHAKAMA KUTENGUA UBUNGE WA WAPINZANI KIRAHISI-RAHISI'' hata ukumbi wa kujadili hawatapewa nawaambia! Labda kama principal au Chouncillor hataki kazi! Wewe unacheza na hii nchi ya kusadikikae! Oohoo!
 
habari wana JF?
Kutakuwa na mdahalo Wa wanafunzi wa vyuo vikuu utakaofanyika katika Chuo Cha Uhasibu(T I A).
Mdahalo huo utakuwa na mada isemayo;Kwa hali halisi ya TANZANIA Je kuna haja ya wanafunzi wa Vyuo vikuu kutumia Uniform?
SIKU:JUMAPILI;TAREHE 22/04/2012.
MUDA:SAA 8:00 MCHANA
MAHALI UTAKAPOFANYIKA:MAIN HALL
NJOONI TUCHANGIE HOJA.
KARIBUNI WOTE!

haki ya nani, wanataka kulipa 150/- nao kama wanafunzi. hivi nao ni elimu ya juu? du hii kali ya mwaka
 
habari wana JF?
Kutakuwa na mdahalo Wa wanafunzi wa vyuo vikuu utakaofanyika katika Chuo Cha Uhasibu(T I A).
Mdahalo huo utakuwa na mada isemayo;Kwa hali halisi ya TANZANIA Je kuna haja ya wanafunzi wa Vyuo vikuu kutumia Uniform?
SIKU:JUMAPILI;TAREHE 22/04/2012.
MUDA:SAA 8:00 MCHANA
MAHALI UTAKAPOFANYIKA:MAIN HALL
NJOONI TUCHANGIE HOJA.
KARIBUNI WOTE!

Hii ni takataka kabisa. Sikutegemea wananafunzi wa Chuo Kikuu washindwe kutafuta "Topic" ya maana ya kujadiri. Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi sana yanayotaka wanafunzi wa Vyuo Vikuu wayajadiri kwa undani. Wanafunzi wanatakiwa wajadiri mada za maana kwani wakitoka huko watapambana na wanafunzi waliotoka kwenye vyuo vingine duniani kwenye "forums"kama za World Economic Forum, World Bank, IMF, etc. Inakatisha tamaa kabisa.

Kwa mtazamo wangu ningependa kuona mada za maana na zikijadiriwa kwa Kiingereza kwani hiyo ndiyo lugha inayotumika kufundishia Vyuo Vikuu na ndiyo lugha watakayopambana nayo mara nyingi wakiajiriwa.
 
Back
Top Bottom