Mkuu hapa naona umemshukia Ndugu Hamad with full force!!!
Ungepunguza ushabiki ungeiwasilisha vizuri na pengine ungemshauri nini afanye kuondosha mapungufu aliyonayo. Hakuna mkamilifu katika binadamu.
Lengo langu ni ku-comment katika hizo nukta ulizoziorodhesha. Nimechagua hizi:-
2. Haijui vizuri katiba ya JMT na kanuni za bunge
Alikaa bungeni zaid ya miaka 15 na alishashika madaraka mbali mbali serikalini. lakini haijui vizuri katiba ya nnchi na kanuni za bunge, kiasi cha kushindwa kujua kutoka bungeni kwa wabunge wa CHADEMA sio kuvunja katiba wala kanuni yoyote ya bunge.
6. Anajivunia uzanzibar kuliko utanzania. (ni mmbaguzi)
Kauli zake zinadhihilisha kilcho moyoni mwake.
9. Ni kigeu geu / Hana msimamo
Amekuwa akitoa kauli zinazopingana. Kwanza alishasema kwamba Mh.Mbowe hakumualika kuunda kambi ya upinzani, the akasema aliambiwa akakataa kutoka na tofauti za kimisimamo. Hata alipoulizwa aseme ipi ni kauli sahihi aliruka kwa ukali ule ule kwamba "mimi nipo very seriose na kauli zangu". Sijui swali hakuliewa ? alitumia ukali kuficha udhaifu au ndo udikteta?
1.Kwamba haijuwi katiba ya JMT.
Jamani katiba yenyewe katiba tia viraka. Sote tuna kilio, tunataka Katiba Mpya. Ni kuwa katiba iliyopo haikidhi matakwa ya Umma wa Tanzania kwa hiyo akiijuwa au akijifanya haijuwi si muhimu sana .Ukweli ni kuwa katiba iliyopo haitufai katika mazingira tuliyonayo leo. Kwa nini tutaendelea kutia viraka. Viraka ambavyo badala ya kusawasisha hali au jambo huwa inazidisha utata?
By the way, inaoneka wabunge wengi tu hawaijuwi, hawaielewi katiba ya JMT. Ubunge na siasa imekuwa ni short cut ya kupunguzia makali ya njaa kwa wabunge wengi.
2. Kwamba anajivunia uzanzibari kuliko utanzania na kwa hiyo ni mbaguzi.
Mkuu, Utanzania ni kitendawili, zari, mazingaombwe, kiini macho, changa la macho, danganya toto! tafadhali rudia "the articles of Union " zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baadae "Tanzania"
Umeshawahi kusikia kuna nchi inayoitwa " The European Union"?. nijuavyo Europian Union Ina members wake na ni nchi hizo ulizozifikiri katika kujibu suali nililokuuliza.
Mwalimu kama angekuwa yuko hai angekuwa mtu pekee aliye na uwezo wa kutujibu leo kwa nini allifuta Tanganyika? na serikali ya Tanganyika? Au kama Jaji Warioba anaweza kutusaidia katika hili basi atusaidie.
Mini nafikiri watu huwa wanajinasibu kwa daraja. hutamkuta mchaga akajivunia umakonde au usukuma. Mchaga atajivunia uchaga wake na sehemu alikotoka kama ni Arusha au Moshi.
Nina hakika ukikutana na Hamad nje ya Tanzania atajivunia utanzania wake na sio uzanzibari wake. na atakapokuwa katika kundi la waulaya na waamrika au waasia atajivunia uafrika wake kuliko Utanzania wake. after all, Wazanzibari hawajivunii sana ukabila kama wenyeji wa Tanganyika kwani ukabila wao ni huo Uzanzibari na wanapokuwa ndani ya Zanzibar hujivunia au hujiita kwa sehemu walizotoka kama mtumbatu, mpemba, muunguja, mkojani. Tupo pamoja ndugu?
3. kwamba ni kigeu geu/ hana msimamo
Kama mimi na wewe tumefuatilia mdahalo ule ule basi utaona kuwa Chadema kupitia Mbowe na cuf kupitia Hamad wamesema kuwa bado doors are open katika kuunda kambi inayoshirikisha vyama tofauti . Ki kanuni, Chadema wanaweza kuunda kambi ya upinzani peke yao bila ya kushirikisha wengine? Suali hapa ni at what cost? watapata nini? watakosa nini? wapinzani wote wakiungana au wakishirikiana hata kama kutakuwa hakuna mamluki au wasaliti au CCM B na C bado wanakazi kubwa ya kufanya kuichallenge CCM ambao wana support ya dola, kuanzia mjumbe wa nyumba kumi, mkuu wa wilaya , mkoa, usalama wa taifa, jeshi, polisi, magazeti, tume ya uchafuzi ..you name it! bado wapinzani wana muda wa malumbano ambayo hayawaletei tija yoyote?
Kama WATANGANYIKA NA WAZANZIBARI sisi wananchi tuwashawishi viongozi wa vyama vya upinzani kuweka mbele maslahi ya Taifa na sio kivyama. Taifa la Umoja wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania!!??) ni kubwa kuliko chama chochote na wananchi walio wengi katika Tanganyika na Zanzibar wako taabani, dhofu wa hali na mali,wamejichokea na wanakata tamaa sasa.