Kwa muktadha wa huu mjadala, tunapoongelea Elimu, inamaanisha kiwango gani cha elimu? Ni elimu ya msingi, sekondari, chuo diploma, degree, Post graduate ( Masters, PhD)?
Tukirudi kwenye pesa nakwenyewe ni kiasi gani cha pesa tunakijadili hapa.
Kuna watu wana vyote, pesa na elimu, hali kadhalika wapo wenye pesa bila elimu huku tukiwa na wenye elimu bila pesa ( hawa ntawaita wenye vyeti).
Unaposema pesa ni bora kuliko elimu kumbuka hauwezi kuwakwepa wenye elimu kuanzia kuitengeneza pesa yenyewe hadi michakato kadhaa inayofanikisha mzunguko wa pesa.
Kuna mmoja ametoa mfano wa Billionaire Laizer, sina uhakika na shule yake lakini anahitaji watu wenye elimu katika shughuli zake.
Lazima wajuvi wa miamba na madini waweze kutoa muongozo wa eneo lenye madini. Watahitajika wataalam wa mitambo inayotumika kuchimba na kutoboa miamba.
Kuna wahasibu na watu wa mahesabu. Hao ni watu wenye elimu kwa uchache tu.
Kwa mtazamo wangu, elimu ni bora ( hapa ieleweke sio ile ya kufukuzia cheti). Mtu aliyezingatia kupata uelewa hata aishie kidato cha nne au ajisomee mwenyewe kupata maarifa, anaweza kufanya maajabu kulikk waliohitimu kiwango cha juu kabisa cha elimu.
Maisha yametawaliwa na maamuzi tunayofanya, kila kitu kinahitaji kufikiria na kutafakari ili kutoa maamuzi sahihi. Mwenye elimu akiitumia vizuri elimu yake anakua kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi kwakuwa ana taarifa za mambo mengi kumsaidia kufanya maamuzi sahihi.
Uzuri ni kwamba wote tunaweza kufikiri na kufanya maamuzi licha ya bila kujali kiwango cha elimu tulicho nacho, ubora na matokeo ya maamuzi yanaweza kutegemea elimu ya mhusika japo sio mara zote.
Tunashuhudia wasomi wetu wanavyodhalilisha taaluma zao kisa wajipatie kipato kupitia siasa.
Ikumbukwe mtu anaweza kupata rlimu kwa njia tofauti tofauti, sio lazima iwe darasani pekee. Ndio maana mwanzo nikasema elimu ya aina gani na kiwango gani tunaijadili hapa?