Mdada, uko 'single' na hauna mtoto 'housegirl' wa nini?

Mdada, uko 'single' na hauna mtoto 'housegirl' wa nini?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
61,742
Reaction score
126,662
Heshima kwenu great thinkers,

Naomba msiniambie tu nipambane na hali yangu ni hivi, nashindwa kuelewa sijui kwa ajili ya ushamba au umasikini wangu tu ndio unaonifanya nifikirie hivi.

Nimeshaona mara nyingi tu hii utaona mdada ana kazi yake wakati mwingine ya kawaida tu mshahara six digits, hana familia, wala kazi yake sio ya kumuweka bize kihivyo anakuwa na msichana wa kazi. Wa nini? Yaani wanaishi wawili tu yeye na binti wa kazi. Ni uvivu, wanapambana na upweke, au wanaogopa kulala peke yao?

Ninyi wenzangu mnafikiriaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Let me guess, kuna jamaa umempenda na unaumia kuona yuko house girl!!

Kama hujui wenda huyo hg yuko kwenye plans za jamaa na kama hg akikomaa anaweza kupandishwa cheo kuwa mke!!!

Btw kuna ubaya kutoa ajira??

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesema wadada hivi umesoma post kweli. Mwanaume kuwa na house girl siwezi kushangaa. Btw mimi sio 'domozege' nikimpenda mtu namfungukia tu kwani sh'ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda beki 3 anamsaidia kuweka ulinzi nyumbani muda bi mkubwa akiwa mzigoni...
Hii ni inaweta kuwa na mashiko kwa wale walio na nyumba zao au wamepanga nyumba kubwa sasa mwenzangu na mimi umepanga chumba kimoja au viwili uswahilini mmh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
»Wengine waoga, amepanga nyumba nzima ila hawezi kuishi peke yake.
»Wengine wanatafuta "mlinzi" wa nyumba when she's away, kazini, safari etc.
»Wengine wavivu wa kufanya shughuli za ndani (yes, some women CAN'T cook, neither can they wash), wapo wengi tu.
»Wengine wanashurutishwa na wazazi wao, first time kupanga hivyo gaining experience unahitaji mtu wa kuishi nae.

..zipo sababu nyingi Khantwe.
 
Mkuu utakuwa hujui kusoma labda hebu rudia kusoma nilichoandika

Sent using Jamii Forums mobile app


kweli mie kilaza!umesema unashangaa mdada ANA KAZI YAKE TENA MSHAHARA HAUZID 6 DIGITS! .ndo maana nikakuuliza na huo mshahara 6 digits unatka abebane na mtoto aende na kazini?? hebu soma ulichoandika tena! atleast ungesema mdada asie na ajira
 
Back
Top Bottom