Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa
hawezi kuongea na kuwekewa oxgen.
Akawa anaombewa na Mchungaji.
Akiwa anaombewa, yule mgonjwa
akachukua kalamu na karatasi,
Akaandika na akampa yule Mchungaji. Ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.
Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemu. Akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema;
"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA"
Akampa mmoja wa wanandugu akisome. Haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa: "UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN,