SoC02 Babu amenisimulia kuhusu mgonjwa wa ICU

Stories of Change - 2022 Competition

Kanal Hilal

Member
Feb 4, 2017
62
121
Babu yangu amenisimulia kuhusu athari zinazotokana na kupuuza mambo au kuchukulia "poa" kila kitu. Kupitia simulizi hii nataka nawe ujifunze, na ikibidi ikufanye kuwa mpya kabisa.

Bwana mmoja alikuwa mgonjwa sana ICU akipumua kwa msaada wa mashine maalumu ya kupumulia- oxygen machine. Muda wote alikuwa kitandani hoi asiweze hata kuongea.

Ndugu zake walipokuja kumjulia hali, waliwasiliana nae kwa kutumia vikaratasi vya maandishi. Mgonjwa alipotaka kitu, aliandika katika karatasi na kuwapatia ndugu zake. Na alifanya hivyo hata kwa madaktari na wahudumu wa pale hospitali.

Siku moja ndugu zake walipokuja kumtazama wakaanza kupiga "story" ya mambo yao binafsi. Wakiwa pembeni ya kitanda cha yule mgonjwa, soga ikawashika kweli kweli. Kama ilivyo kawaida yake, mgonjwa akachukua kalamu na karatasi, akaandika ujumbe na kumpatia mmoja kati ya wale ndugu zake. Kutokana na kunogewa na "story" jamaa aliyepewa ile karatasi hakuisoma, akaikunja na kuiweka mfukoni. Na haikuchukua muda mrefu, mara yule mgojwa akafariki.

Loooooh, kulikoni?

Baada ya uchunguzi wa madaktari ikagundulika kuwa, mgonjwa alishindwa kupumua vizuri na ikasababisha kifo chake. Maswali yakawa ni je, alishindwaje kupumua wakati alikuwa akitumia mashine ya kupumulia- oxygen machine?! Na je, kama alishindwa kupumua vizuri, ni kwanini hakutoa taarifa kwa nduguze ili wawajulishe madaktari?!

Maswali hayo yakawakumbusha wale ndugu kuusoma ule ujumbe wa kwenye karatasi ulioandikwa na mgonjwa kabla ya kifo chake.

Loooooh!

Ile karatasi iliandikwa hivi, "inua mguu tafadhali, umekanyaga mpira wa oxygen, nashindwa kupumua".

It is too late.

Ujumbe wangu wa leo kwako wewe rafiki yangu. Acha kupuuza mambo na kuchukulia "poa" kila kitu, ni hatari sana. Kumbuka hakuna mambo madogo wala makubwa, ilimradi tu mambo hayo ni muhimu kwako au hata kwa wengine.

Usikiapo muito wa SMS kwenye simu yako, ifungue hiyo SMS na uisome. Na ikiwa inahitaji kujibiwa, basi ijibu papo hapo. Acha kuchukulia "poa" kila jambo, kwani wakati mwingine kuchukulia kwako "poa" kila kitu, huwaumiza sana watu wanao kuzunguka.

Jirekebishe na uwe mpya.

Picha: Regency Medical Center

Na Hilal Kanal
Daressalaam, Tanzania.

shutterstock_500901592-1-scaled.jpg
 
Back
Top Bottom