Mchungaji Yehova jela kwa wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Yehova jela kwa wizi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MCHUNGAJI wa Kanisa la Yehova la mjini Songea mkoani Ruvuma amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na kosa la wizi wa vifaa vya umeme.Hukumu hiyo ilitolewa dhidi ya mchungaji huyo na
  mwenzake, katika Mahakama ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya hiyo, Bw. Frank Mahimbali.

  Awali Mwendesha Mashtaka, Inspekta Saana alidai mbele ya hakimu huyo kuwa tukio hilo la wizi lilitokea Agosti Mosi mwaka huu katika Shule ya Sekondari St. Luise iliyopo Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga.

  Inspekta Saana alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Issaya Mwakalinga (32) mkazi wa Songea mjini na Denice Masetti (28) mkazi wa Namabengo Wilayani Namtumbo.Alidai kuwa watuhumiwa hao waliiba vifaa viwili vya kuzalisha umeme jua, yenye thamani ya sh. milioni mbili, mali ya shule hiyo.

  Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kwamba mchungaji huyo na mwenzake walipanda juu ya paa la jengo la shule hiyo na kuiba vifaa hivyo.
   
 2. S

  Sun de Terry New Member

  #2
  Mar 20, 2013
  Joined: Mar 8, 2013
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa kesi hiyo ilikuwa ni nini!!? I mean,Huyo ndugu bado yupo Jela!?
   
Loading...