Mchungaji na mkewe wanusurika kuuawa

Mkuu hiyo ni fursa.Kama una uwezo wa kumkemea jambazi mpaka akakauka basi fungua kampuni za kulinda(Security Companies)ili ulinde kwa kukemea tu.
Za kuambiwa changanya na zako.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ aloooo!
 
Kweli duniani kuna mengi. Ni ajabu mwanadamu anamuwinda mwanadamu mwenzake utafikiri tunaishi katika mbuga za wanyama.

Siku kadhaa zilizopita, mimi na Mchungaji wangu pamoja na mke wake, tulinusurika kuuawa. Ilikuwa alasiri, mimi na Watumishi hao wa Mungu, tulienda kufanya huduma katika mji mmoja. Barabara inayokwenda katika mji huo ilikuwa ya vumbi na ilikatisha katika pori kubwa lenye miti mirefu.

Baada ya kufika katika mji huo, tulifanya kile kilichotupeleka kisha tukaanza safari ya kurudi. Wakati huo ilikuwa inakaribia saa 12 jioni. Tulivyolifikia lile pori tukaona mbele yetu vijiti vyenye futi kama mbilimbili vimesimikwa chini kwa karibu karibu, mstari mmoja. Mchungaji wangu ndiye aliyekuwa anaendesha gari, akaona sio vema kuvikanyaga vile vijiti akatafuta upenyo pembeni ya vijiti hivyo tukafaulu kupita bila kuvikanyaga. Kwa mawazo yetu tulifikiri labda ni watoto walikuwa wanacheza kwenye barabara hiyo wakaona wasimike vijiti hivyo. Kwa sababu hiyo tuliendelea na safari bila kuhisi chochote kibaya mbele yetu. Siku hiyo hakukuwa na magari wala pikipiki tulizoziona zikipita barabara ile.

Kabla ya kulipita lile pori, tukaona kikwazo kingine kikubwa mbele yetu. Gogo kubwa, refu, lilikuwa limelazwa barabarani kuzuia gari lisipite. Gogo hilo lilikuwa nene sana hivyo kulikuwa hakuna uwezekano wa kulivuka kwa gari. Pembeni ya barabara hiyo hapakuwa na upenyo kama ilivyokuwa pale mwanzoni hivyo ilibidi Mchungaji asimamishe gari. Tulipoangalia kulia kwa barabara, mita kama kumi kutoka kwenye gogo hilo, tukaona mtu ameshika upanga mkononi. Ghafla tulipaza sauti na kuanza kumuomba Mungu atupiganie huku tukimkemea shetani ashindwe kwa Jina la Yesu, sawasawa na Neno la Mungu katika Yakobo 4:7-10. Tulikemea sana, kisha Mchungaji akaniomba nishuke niliondoe lile gogo. Mungu alinipa ujasiri usiokuwa wa kawaida, nikashuka kutoka kwenye gari nikaliendea lile gogo. Nilitumia nguvu nyingi kulivuta na kuliondoa barabarani; kisha nikapanda tena gari, tukaanza kuondoka. Tulivyomtazama yule mtu mwenye upanga, alikuwa bado amesimama palepale alipokuwa. Naamini Mungu alimpiga upofu, kama alivyofanya wakati wa Elisha(2Wafalme 6:18) ndio sababu hakuweza kusogeza unyayo wake kutukaribia. Tuliendelea na safari kwa furaha kubwa huku tukimsifu Mungu aliyetuvusha salama eneo lile.

Kazi za Ibilisi ni kuiba, kuchinja na kutafuta kuharibu maisha yetu(Yohana 10:10), lakini Mungu anapokuwa upande wetu, shetani na majambazi yake yanashindwa na kulegea.
Utukufu kwa Mungu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ aloooo!
Ilitabiriwa zamani kuwa siku za mwisho watu watapenda pesa kuliko kumpenda Mungu. Unabii umetimia

2 TIMOTHEO 3:1-5​

Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..."
 
Kweli duniani kuna mengi. Ni ajabu mwanadamu anamuwinda mwanadamu mwenzake utafikiri tunaishi katika mbuga za wanyama.

Siku kadhaa zilizopita, mimi na Mchungaji wangu pamoja na mke wake, tulinusurika kuuawa. Ilikuwa alasiri, mimi na Watumishi hao wa Mungu, tulienda kufanya huduma katika mji mmoja. Barabara inayokwenda katika mji huo ilikuwa ya vumbi na ilikatisha katika pori kubwa lenye miti mirefu.

Baada ya kufika katika mji huo, tulifanya kile kilichotupeleka kisha tukaanza safari ya kurudi. Wakati huo ilikuwa inakaribia saa 12 jioni. Tulivyolifikia lile pori tukaona mbele yetu vijiti vyenye futi kama mbilimbili vimesimikwa chini kwa karibu karibu, mstari mmoja. Mchungaji wangu ndiye aliyekuwa anaendesha gari, akaona sio vema kuvikanyaga vile vijiti akatafuta upenyo pembeni ya vijiti hivyo tukafaulu kupita bila kuvikanyaga. Kwa mawazo yetu tulifikiri labda ni watoto walikuwa wanacheza kwenye barabara hiyo wakaona wasimike vijiti hivyo. Kwa sababu hiyo tuliendelea na safari bila kuhisi chochote kibaya mbele yetu. Siku hiyo hakukuwa na magari wala pikipiki tulizoziona zikipita barabara ile.

Kabla ya kulipita lile pori, tukaona kikwazo kingine kikubwa mbele yetu. Gogo kubwa, refu, lilikuwa limelazwa barabarani kuzuia gari lisipite. Gogo hilo lilikuwa nene sana hivyo kulikuwa hakuna uwezekano wa kulivuka kwa gari. Pembeni ya barabara hiyo hapakuwa na upenyo kama ilivyokuwa pale mwanzoni hivyo ilibidi Mchungaji asimamishe gari. Tulipoangalia kulia kwa barabara, mita kama kumi kutoka kwenye gogo hilo, tukaona mtu ameshika upanga mkononi. Ghafla tulipaza sauti na kuanza kumuomba Mungu atupiganie huku tukimkemea shetani ashindwe kwa Jina la Yesu, sawasawa na Neno la Mungu katika Yakobo 4:7-10. Tulikemea sana, kisha Mchungaji akaniomba nishuke niliondoe lile gogo. Mungu alinipa ujasiri usiokuwa wa kawaida, nikashuka kutoka kwenye gari nikaliendea lile gogo. Nilitumia nguvu nyingi kulivuta na kuliondoa barabarani; kisha nikapanda tena gari, tukaanza kuondoka. Tulivyomtazama yule mtu mwenye upanga, alikuwa bado amesimama palepale alipokuwa. Naamini Mungu alimpiga upofu, kama alivyofanya wakati wa Elisha(2Wafalme 6:18) ndio sababu hakuweza kusogeza unyayo wake kutukaribia. Tuliendelea na safari kwa furaha kubwa huku tukimsifu Mungu aliyetuvusha salama eneo lile.

Kazi za Ibilisi ni kuiba, kuchinja na kutafuta kuharibu maisha yetu(Yohana 10:10), lakini Mungu anapokuwa upande wetu, shetani na majambazi yake yanashindwa na kulegea.
Mbona heading inasomeka mchungaji na Mke wake wanusurika kuuawa? Alafu kwenye habari yenyewe anaonekana wewe na mchungaji????? Kama sijaelewa vile!!!!!
 
Kwani heading huwa inaeleza kila kitu?
Ulisoma kiswahili japo kwa level ya darasa la sita na ukajifunza kuandika Insha? unawezaje kuandika kichwa cha habari KUKU NA BATA wanasurika kuliwa na mwewe alafu habari yenyewe ikaishia kuelezea jinsi kuku na mbuzi na si bata na kuku walivyonusurika? Bata kwa maana ya mhusika mkuu na namba mbili unamwachaje? Wahusika wakuu kwenye habari ni mchungaji na mkewe na siyo mchungaji na msumliaji, hakukuwa na sababu ya msimliaji kuwa sehemu ya habari.
 
Kwanini kila mara unapatwa na majanga tu! Mara majambazi mra kuunguliwa moto nk! Na je umeokoka hivi karibuni?
Umesoma habari za Paulo? Mimi sijafikia hata robo ya majanga yaliyompata. Sikia anavyosema katika
2 Wakorintho 11:23-27
"...katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.
Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;
katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi..."

Unaonaje majanga hayo. Unafikiri ni kwa sababu ya kuokoka hivi karibuni?
 
Mtu anakuteka na panga we unamkemea shetan unaakili kweli bro? Utakuja kufa kijinga acha uboya
Ndo maana mchungaji alikufanya kimbola wake akakutuma ukatoe gogo jamaa wa panga angeanza na ww ndo ungejua mchungaji aliwahi kushiriki mbio za magari
 
Mtu anakuteka na panga we unamkemea shetan unaakili kweli bro? Utakuja kufa kijinga acha uboya
Mambo ya rohoni ni vigumu kuyaelewa kimwili.

Mkuu, umewahi kusoma Mathayo 16:23? Imeandikwa hivi:
"Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, β€œRudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

Hapo aliyekuwa anakemewa ni nani? Ni Petro au Shetani? Ni Shetani, ingawa maneno yalikuwa yanamlenga Petro. Kinachomfanya mtu ashike upanga na kutaka kumuua mwanadamu mwenzake ni nini? Hiyo roho ya Shetani iliyokuwa inamsukuma mtu yule kutaka kuiba na kuua ndiyo tuliyoikemea. Na kwa Jina la Yesu hiyo roho chafu ilisalimu amri. Jina la Yesu ni Jina Kuu kupita majina yote. Haleluya!
 
Mkuu hiyo ni fursa.Kama una uwezo wa kumkemea jambazi mpaka akakauka basi fungua kampuni za kulinda(Security Companies)ili ulinde kwa kukemea tu.
Za kuambiwa changanya na zako.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom