Mchungaji na Katekista wakimbia kutwaliwa Mbinguni

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Yupo katekista mmoja alikuwa mlevi sana wa pombe. Hata hivyo ulevi wake haukuwa kikwazo katika kazi zake za kuchunga kondoo wa Bwana, aliaminiwa kanisani. Jirani na kanisa analofanyia kazi katekista huyo mlevi kulikuwa na makaburi ambayo yalizungushiwa uzio. Basi siku moja Palitokea wezi wawili ambao usiku wa saa 6 waliiba maembe jirani na makaburi hayo.

Waliweka maembe haya katika viroba na kukubaliana kuwa waende makaburini kugawana sawa kwa sawa. Kwa kuwa makaburi hayo yalikuwa njiani wakakubaliana wakati wanagawana maembe watumie lugha tofauti ili kama wapita njia wakiwasikia wasijue nini kinafanyika. Wakaweka maembe juu ya kaburi na kuanza kugawana moja moja huku wakisema "wangu huyu" na mwingine anasema "wangu huyu".

Ikatokea wakati katekista mlevi anapita akasikia sauti zikitokea makaburi za "wangu huyu", "wangu huyu". Akakimbia hadi jirani na nyumba moja ya kanisa alikokua anakaa mchungaji wake na kumuamsha. Akumwambia amka leo kuna balaa makaburini shetani na Mungu wanagawana watu; wabaya kwa shetani wema kwa Mungu. Mchungaji akamwambia muongo wewe, huo ulevi wako twende na mimi nikashuhudie.

Basi wakaenda, walipofika wakasimama nje ya geti la kuingilia makaburi. Mchungaji naye akasikia sauti zile za "wangu huyu, wangu huyu". Sasa kumbe wale wezi wakati wanapita pale getini na maembe walidondosha mawili, hivyo walipomaliza kugawana yale waliyokuwa nayo wakasema twende getini tukawachukue na wale wawili tuliowaacha.

Hapo ikawa kizaazaa na paytashika kati ya Mchungaji na Ketekista walitimua mbio kukimbilia kanisani . Walijua sasa muda wao wa kuishi dunia ulikuwa umekwisha na ni zamu yao kugawanywa. Cha ajabu japo mchungaji alikuwa mzee kuliko katekista lakini alikuwa wa kwanza kufika kanisani.

Jamani mbinguni kunatisha kama hujajiandaa, hata wachungaji wanapakimbia kwenda.
 
tehe tehe tehe.......kwakwakwakwa...............laaaaa jamani!!!!!!unafanya mchezo na kufa weee
 
nitakushitaki kwa plagiarism wewe. Au nikuwekee link hapa ya hii kitu uliyochakachua?
 
Unadhani kukataa kura ni mchezo, tena kama ni mdhambikaji?. Lakini kama ni mfuasi wa Yesu Kristo huna haja ya kuogopa kifo.
 
Yupo katekista mmoja alikuwa mlevi sana wa pombe. Hata hivyo ulevi wake haukuwa kikwazo katika kazi zake za kuchunga kondoo wa Bwana, aliaminiwa kanisani. Jirani na kanisa analofanyia kazi katekista huyo mlevi kulikuwa na makaburi ambayo yalizungushiwa uzio. Basi siku moja Palitokea wezi wawili ambao usiku wa saa 6 waliiba maembe jirani na makaburi hayo.

Waliweka maembe haya katika viroba na kukubaliana kuwa waende makaburini kugawana sawa kwa sawa. Kwa kuwa makaburi hayo yalikuwa njiani wakakubaliana wakati wanagawana maembe watumie lugha tofauti ili kama wapita njia wakiwasikia wasijue nini kinafanyika. Wakaweka maembe juu ya kaburi na kuanza kugawana moja moja huku wakisema "wangu huyu" na mwingine anasema "wangu huyu".

Ikatokea wakati katekista mlevi anapita akasikia sauti zikitokea makaburi za "wangu huyu", "wangu huyu". Akakimbia hadi jirani na nyumba moja ya kanisa alikokua anakaa mchungaji wake na kumuamsha. Akumwambia amka leo kuna balaa makaburini shetani na Mungu wanagawana watu; wabaya kwa shetani wema kwa Mungu. Mchungaji akamwambia muongo wewe, huo ulevi wako twende na mimi nikashuhudie.

Basi wakaenda, walipofika wakasimama nje ya geti la kuingilia makaburi. Mchungaji naye akasikia sauti zile za "wangu huyu, wangu huyu". Sasa kumbe wale wezi wakati wanapita pale getini na maembe walidondosha mawili, hivyo walipomaliza kugawana yale waliyokuwa nayo wakasema twende getini tukawachukue na wale wawili tuliowaacha.

Hapo ikawa kizaazaa na paytashika kati ya Mchungaji na Ketekista walitimua mbio kukimbilia kanisani . Walijua sasa muda wao wa kuishi dunia ulikuwa umekwisha na ni zamu yao kugawanywa. Cha ajabu japo mchungaji alikuwa mzee kuliko katekista lakini alikuwa wa kwanza kufika kanisani.

Jamani mbinguni kunatisha kama hujajiandaa, hata wachungaji wanapakimbia kwenda.

katekista na mchungaji mbona hapo umetuchanganya maana katekista ni wa Roma Catholic na mchungaji niwa madhehebu ya kilokole? Alafu pia sio wachungaji wote unaowaona na kuwasikia wanamtumia Mungu bali hata wa nguvu za giza wapo
 
Mkuu Shine!
Nimejua hv karibuni nawe ujue leo:
mchungaji wa protestant= pastor= padre.
Katekista wa RC=
Katekista wa Protestants.
Protestants = madhehebu mengine ya kristians.
INSHORT KAT. YUPO KOTEKOTE RC + HUKO USEMAKO.
 
unatake long time kueleza point yako..
Jarib kuwa sharp..
kama unaimbisha dem itakutek a yea..

Then unafika at the point tayari kadem kameshavimbisha tumbo na wazee wa fast track. Mbaya zaidi kumbe kadem kalikuwa kanakumind pia long tym b4. Lakn sasa its 2 late.
INAUMA! INAUMA! INAUMA!
 
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hii kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaallllllllllllllllliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii aiseeeeeeeeeeee je ingekuwa wewe ungesubiri????????????????????????????????????????????????
 
Back
Top Bottom