Mchungaji Msigwa aboronga Bungeni

Umemdharau wewe kama nani? Kama umesoma mbona unatumia ID feki ili tusikujue? Wewe ni wakupigwa na kapuya tu, tumrchoka.
 
Kweli wewe ni abunuas la kike
 
Umemdharau wewe kama nani? Kama umesoma mbona unatumia ID feki ili tusikujue? Wewe ni wakupigwa na kapuya tu, tumrchoka.
Duh, naona umekuja kwa hasira sana. Wenzako wamechangia kistaarabu wewe unaleta za kuleta. Pole sana Mkuu
 
Ndo muone jinsi akili za watu zinamadudu! yaani watu badala ya kuangalia kusudi la ujumbe au swali la msigwa yeye anaangalia kosa! Ndo maana tanzania hatusongi mbele!!! kwenye masuala ya msingi tunaleta utani na ushabiki. Mimi Msigwa nimemuelewa kabisa tena hata hajakosea kihivyo!
 
Da! naona umejika kwenye vijihesabu vya std 3 na kuviletea thread.Hilo halikuwa suala la msingi. au kwa kuwa unakaa mjini huoni misitu inavyopukutika
 
Nimekuja mbio Mchungaji kaboronga nini tena Bungeni? Kumbe ni masuala tu ya kuteleza ulimi....
Kweli buku saba sasa mnaishiwa vya kukosoa, wasiwasi wangu sijui kwa thread hii kama watoto watakula leo, maana hata kama zinalipwa sio hii ya hivi....!
 

kwa serikali hii, mwananchi wa kawaida gas ataisikilizia kwenye bomba tu, haitamkomboa na bei ya vitu itazidi kusonga mbele! Uongo wa wanasiasa unatumika kuhalalisha ujambazi wao.
 
Kwa hiyo kulikuwa na umuhimu gani wa kutaja hizo namba? Msigwa kavurugwa kwa hili. Wala msimtetee
si kwamba namtetea msigwa kwa kukosea la ila kutunza mazingira ni muhimu kuliko huo ukosoaji wako, sijui kama unanielewa?
 
Kweli wewe ni abunuas la kike
mkuu umeelewa nilichojibu? je unakubali kuwa kwa siku ekari 300 za misitu zinakatwa kama alivyosema mch. msigwa? Tanzania ina ukubwa wa km2 945,000. sasa niambie kama kila siku ekari 300 zinakatwa kingibaki kitu. Anyway huenda na bishana na akili za bavicha. sio saizi yangu.
 

Jikite kwenye hoja ya msingi kuwa ni kweli mamilioni ya miti yanatekekea kwaajili ya nishati ya kupikia. Makosa ya takwimu si hoja. Hoja yako inaweza kujumuishwa kuwa wabunge wote na mawaziri waliopo bungeni ni mambumbu kwakuwa kama sivyo lazima angeinuka mmoja wapo kumsahihisha. Sasa kwakuwa hakuna aliyeinuka basi conclusion hapa ni kuwa wote waliopo bungeni wakati Msigwa anaongea ni vilaza isipokuwa wewe. Tatizo kubwa la baadhi ya JF members ni kuacha hoja na kujikita kwenye makosa madogo madogo ya lugha na takwimu na akili zao wakigundua kosa huwa wanajiona wao ni wasomi, wanaacha kuchangia hoja wanajikita kwenye kasoro ambazo haziondoi msingi wa hoja husika. Ona hata mtoa mada hajaongea lolote kuhusu uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji miti kwaajili ya nishati ya kupikia jambo ambalo ni kweli ni tatizo kubwa yeye kaona hoja ni tofauti kati ekari na hekta. Hivi msomi unaweza ukatoa hoja kwa kusema "Nijuavyo ni kuwa Ekari 300 ni sawa na Hekta 121.407" Kwahiyo ukijua wewe ndio sahihi? Na la ajabu kuonesha kuwa hana uhakika na anacho kijua anasema "Kwa wale wataalam wa kukokotoa wanaweza wakatusaidia"(sijui yeye na nani?) Na katika hali ya kushangaza anasema
"Kutokana na ufafanuzi huo, nimemdharau sana mchungaji Msigwa na napata shida kubaini uelewa wake" Hii maana yake ni kuwa hata mtoa mada akikosea yuko tayari kudharaulika. Badala ya kumsaidia kuelewa wewe unamdharau!
Kuna usemi usemao "Kila mjinga na kazi yake" Wewe unaweza kuwa mahiri kwa mfano katika kuendesha ndege lakini ukashindwa kuendesha piki piki au baiskeli. Na ndio maana unaweza kuwa mtaalamu wa sheria lakini ukiugua unakwenda kwa daktari ili akuambie tatizo lako na matibabu yake. Kila mmoja ni mahiri katika fani yake na pia ni mjinga katika fani ya mwenzake au asiyoijua. Yaani wewe "kujua" vijihesabu hivyo tu umeona ni issue ya kukupa ujiko na kujiona sasa wewe ni msomi wa kudharau wengine? Shame on you!
 

Mbona yule aliyesema Tanzania ni muunganiko wa Msumbiji na Zanzibar hujamuanzishia sredi?
 
Mbona yule aliyesema Tanzania ni muunganiko wa Msumbiji na Zanzibar hujamuanzishia sredi?

Mkuu, uzi huo ulikuwepo na ulichangiwa sana na machadema. sasa ni zamu ya mchungaji msigwa. mkuki kwa nguruwe
 

kwa hiyo umekosoa au umesahihisha. napata shida sana kujua point yako
 
Weka picha
 
kwa hiyo umekosoa au umesahihisha. napata shida sana kujua point yako
Sasa kama maelezo hayo unapata shida kuyaelewa, huna haki wala uhalali wa kudharau wengine wanapokosea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…