Leo nimewaelewa Mchungaji Msigwa na Lema Baada ya Pastor Ezekiel kudai Kanisa lisipofunguliwa atakosa Tsh 400 Milioni za Sadaka

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,020
Lema ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema aliwaonya Wananchi kuhusu Fedha wanazopeleka kwa manabii.

Mchungaji Msigwa naye akasema Baadhi ya wachungajj hugeuza makanisa yao kuwa vitega Uchumi hivyo Serikali iwachunguze na kuwachuja.

Leo huko Kenya ambako Mchungaji Msigwa alikuwepo juzikati Pastor Ezekiel Odero alitishia kuidai Serikali fidia ya zaidi ya Ksh 20 million endapo hawatafungua Kanisa lake na kumruhusu kuendelea na Ibada.

Odero alisema kwa kawaida misa moja huchukua waumini 45,000 ila kufuatia matatizo yaliyomkuta anategemea Jumapili ya leo waumini 100,000 watahudhuria hivyo makisio ya Sadaka na Ahadi ni zaidi ya Ksh 20 million.

Hatimaye police walilegeza msimamo Kanisa likafunguliwa na Ibada ikaendelea nasi tukaona kupitia Citizen TV.

Mlale Unono!
 
Back
Top Bottom