Mchungaji atabiri Krismas kuwa tete

Mchungaji atabiri Krismas kuwa tete

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,482
Reaction score
286,932
Mchungaji wa KKKT usharika wa Karanga Dayosisi ya Kaskazini , Fred Njama ametahadharisha kwamba sikukuu ya Krismasi mwaka huu haitakuwa nzuri kama miaka iliyopita .

Alitaja sababu za hali hiyo kuwa ni wananchi kuathiriwa na mzunguko wa fedha , ukosefu wa ajira na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu .

" Nimekwenda ibada ya nyumba kwa nyumba unakuta vijana wana degree zao nzuri lakini hawana ajira , wengine hawajapata mikopo , mioyo yao inaumia , watoto wangetamani nguo lakini hali si hali "

Chanzo - Mwananchi .
 
Hapo hajatabiri kitu labda kachelewa tuu kujua .
Swala ni kwamba hali ni mbaya hapo hamna cha utabiri wala sizani kama ameumiza kichwa kufikiria/kutabiri bali hali ni mbaya haswa kifedha
 
Mkuu huyu mchungaji ni mchochezi ... Hili ndio jibu utakalopata. Mm natumia uber sana kwa siku mara 5 na zaidi aisee na kila driver nnakuwa nae ni kulalamika hii hali je wananifanyia mm tu mpaka naamua kukaa kimya
 
Atakuwa mpga dili,maana tunaolalamika siku hizi ni wapiga dili watupu
 
Haha, mwaka huu mtashika kila tawi na kuliachia,

Naona mmehamia mpaka kwenye sikukuu za kidini...

Hii ni dalili mbaya sana ya ukosefu wa Hoja za kisiasa.
 
Mchungaji wa KKKT usharika wa Karanga Dayosisi ya Kaskazini , Fred Njama ametahadharisha kwamba sikukuu ya Krismasi mwaka huu haitakuwa nzuri kama miaka iliyopita .

Alitaja sababu za hali hiyo kuwa ni wananchi kuathiriwa na mzunguko wa fedha , ukosefu wa ajira na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu .

" Nimekwenda ibada ya nyumba kwa nyumba unakuta vijana wana degree zao nzuri lakini hawana ajira , wengine hawajapata mikopo , mioyo yao inaumia , watoto wangetamani nguo lakini hali si hali "

Chanzo - Mwananchi .
Hivi chagadema mmechan
Ganyikiwa na nini?
Mbona wenzenu maisha yanasonga tuu!
 
Hapo hajatabiri kitu labda kachelewa tuu kujua .
Swala ni kwamba hali ni mbaya hapo hamna cha utabiri wala sizani kama ameumiza kichwa kufikiria/kutabiri bali hali ni mbaya haswa kifedha
Kama wizi umekomeshwa kwa 78% sekta ya umma, what do you expect then?
 
Back
Top Bottom