Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Mji wote ulizizima! Mchungaji mashuhuri, anayeheshimika kwa mahubiri yake makali ya utakatifu, alijikuta kwenye kashfa nzito baada ya kufumaniwa na mke wa mtu. Tukio hilo la kushtua lilitokea katika mji mmoja huko Mashariki ya Kati, na chanzo chetu cha kuaminika kimedokeza kuwa Mchungaji huyo alitumia mamlaka yake kumshawishi mke wa mmoja wa waumini wake na hatimaye kuingia katika uhusiano wa siri.
Mume wa mwanamke huyo, ni mwanajeshi jasiri aliyekuwa mstari wa mbele katika ulinzi wa taifa. Alipotakiwa kwenda vitani, Mchungaji huyo alipata nafasi ya kutimiza tamaa zake za mwili. Lakini kilichofuata ni zaidi ya sinema! Mchungaji alipoona kuwa mambo yameharibika, alihakikisha kuwa mume wa mwanamke huyo anashiriki katika mapambano makali zaidi ya vita, ili afe vitani.
Baada ya kifo cha mwanajeshi huyo, Mchungaji alimuoa mke wake kwa haraka, akidhani kwamba siri yake ingefunikwa milele. Lakini mambo hayakuishia hapo! Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba japo alijaribu kuficha, mwishowe ukweli ulijulikana, na familia yake ilipata mapigo mazito. Hadi leo, tukio hilo linaendelea kusimuliwa kila mahali duniani.
Najua unafurahia kusikia habari mbaya, hasa za Watumishi wa Mungu, ndicho kilichokuvuta hapa. Kwani wewe ni mtakatifu? Hesabu dhambi ulizofanya tangu mwaka huu uanze. Si umefanya zaidi ya huyo Mchungaji? Huyo Mchungaji alitubu. Wewe umetubu dhambi zako? Tubu haraka. Kuna mapigo mazito yanaandaliwa kwa ajili ya watu watendao dhambi. Soma Ufunuo wa Yohana.
Kwa habari zaidi za Mchungaji huyo soma 2 Samweli sura yote ya 11 na ya 12.