Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' awaombea kifo waandishi wa habari

Huyu mbona hakamatwi na amewatabiria waandishi [HASHTAG]#watu[/HASHTAG] wengi....kuliko LEMA ye 1tu
 
Huhitaji darubini kumtambua nabii wa uongo. Papa Yohane Paulo II alipopigwa risasi ya tumbo, baada ya kupata nafuu alimtembelea aliyeshambulia huko jela na akambusu, akambariki, na kumsamehe. Huyu amesemwa maneno tu anawatangazia watu hukumu ya kifo!!! Wanaoendelea kumuamini huyu na kumfuata akili zao zinatia shaka.
 
Yeye kaa nani mwenye mamlaka ya kuhukumu watu kifo??? MUNGU PEKEE NDO MWENYE MAMLAKA YA KUHUKUMU
 
Hiyo kauli yake tuu ya kuwaombea kifo watu wenye msimamo tofauti na wake ni tayari ameshajifelisha kukalia hiyo nafasi ya Mchungaji,Sasa Kama angekuwa yeye ndio Nabii Issa au jina lingine Yesu Kristo si angeteketeza Dunia yote kwa waliompinga na kumdhiaki.??,Nyinyi waumini acheni kutoa sadaka katika hayo Majumba yao ya kupigia dili,hao watu ni wapiga dili na ufuska tuu kwa Wanawake.
 
Mm simshangai muhubiri, nawashangaa hao wanaokwenda kuvunwa kila siku kumbe mwenzao anapeleka kwenye vyama vingi ( wanawake) na viroba

Mkuu Imani ni jambo jengine kabisa ,Imani ndio ilipelekea Kibwetere kuwaua waumini wake kirahisi kabisa..
 
ila pale mwisho kamalizia kwa kusema, mimi sihukumu ila namuachia mungu mwenyewe ahukumu.

kwa iyo anafuta kauli yake ya kuhukumu, ni style fulani ya uzungumzaji

Hapana pale alishatia nia na kama ingalikuwa nia yake tungeigeuza kuwa risasi basi angalikuwa alishawaua.Unapokuwa kiongozi (hasa wa ki-imani) ni muhimu sana upime kauli zako kutokana na mazingira kabla ya kuzitoa..
 
Kumbe matukio yote anayotuhumiwa mchungaji ni uwongo na ilitolewa na wabaya wake kwa nia ya kumchafua?
 
Hahaha, naomba niulize swali la kizushi:

Na Mzee wa upako anakuwa inspired na Holy Ghost?
Au waumini wake pia wana Holy Ghost?

Huyu Mzee naona naye ni mpiga dili tu.
 
Hahaha, naomba niulize swali la kizushi:

Na Mzee wa upako anakuwa inspired na Holy Ghost?
Au waumini wake pia wana Holy Ghost?

Huyu Mzee naona naye ni mpiga dili tu.

Mkuu huyu mwehu siku una muda wa ziada jaribu kumcheck Channel Ten uone lilivyo lisanii....halafu waumini wanakaa kitako kabisa wanamsikiliza like seriously.....

Yaani tuna safari ndefu kweli...

Zee huni kweli
 
Pia biblia katika Warumi 12:21 inasema,"Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema". Sasa huyu ni mchungaji gani anayefanya tofauti na mahubiri! Amekosewa sawa, kwa mujibu wa maandiko anatakiwa asamehe saba Mara sabini.Ana imani mfu ya kulipiza kisasi. Mungu amekataa kisasi na katika Warumi 12:19, anasema tusilipize kisasi, kwani kisasi ni juu yake yeye atatulipia. Hii inatufanya tuamini kuwa huyu si mtumishi wa Mungu bali ni mpiga dili kwa kutumia uchawi wa Nigeria na miujiza yake feki.
 
Hakuna atakaekufa hata mmoja tuone kama ataacha huduma, cha msingi angeonyesha busara ya kunyamaza sababu hawezi shindana na Media ni kubwa,
 
Kwani wamemsingizia? Kama kufa watakufa kwa mapenzi ya Mungu na sio kwa neno lake labda awauwe. Kwanza angewataja majina ili tuwe tunafuatilia kama huo unabii wake utatimia au la!!!!
 
Back
Top Bottom