Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' awaombea kifo waandishi wa habari

siku hizi izraili mtoa roho!embu akamatwe haraka huyu awekwe ndani kama lema,nyambaffff
 
Anazidi kujiharibia biashara yake ile ...mana haya makanisa ni biashara tu no more
 
Tofauti yetu sisi na watumishi wa zamani akina
mfalme Daudi ni kwamba,akina Daudi
walipoambiwa walipokosea walitubu mara moja
Sisi tunapoambiwa tulipokosea tunaanza kujenga
hoja za kujitetea na ndo hapo Mungu
wa rehema anatuacha tutumie akili na maarifa yetu
kuweka mambo sawa.
 
Neno linasema kimjazacho mtu ndio kimtokacho sasa amekosa mfano wa biashara nyingine hadi aseme atauza gongo

Pombe ndio zimemjaa moyoni mwake taratibu anaanza kuanika utupu wake Mungu alimvua nguo yeye anamalizia kujivua nguo za ndani
 
Amakwili dini ni biashara,inamana jamaa wamemwalibia ,kwann mcha Mungu anakuwana hasira?
 
Hata Yesu mwenyewe hakuwahi kuwa na aina hii ya injili. Neno linasema uovu usitajwe kwenu. Kama hajafanya anayodai anasingiziwa, anyamaze, kisasi ni juu ya Mungu mwenyewe, wasipokufa ni kweli atauza gongo? Na huo ndio utumishi? Yusufu alisingiziwa kutembea na mke wa Potifa ikapelekea kufungwa gerezani lakini hakutoa Maneno ya aina hii.
Tunashuhudia aina mpya kabisa ya watumishi wa kizazi chetu.
 
Mbaya zaid kugundua ukatoliki ni uongo alaf unahamia kwa walokole kwa mbwembwe msiba mkubwa unagundua mchungaji muhongo, mlevi na mpga lamri daah.
 
Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.

Mchungaji gani analaani watu ili wafe? Alitakiwa awaombee ili waongoke kama wamemsingizia. Kwani akiacha kuhubiri atakayethirika ni nani? Sana sana ni yeye atakosa sadaka.
 
Duh....

Na sisi tulio comment JF kuhusu yeye tutakufa?

Waandishi wakashtaki kutishiwa kuuliwa. ....
 

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.
Sasa hii hatari viongozi wa dini mnaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom