Mchungaji Anthony Lusekelo awapa onyo CHADEMA

,pesa kwake zipo maana yeye si analetewa sadaka na watu wake, anatafuta wapi?
 
Japo mimi siwafagilii CDM huyu mchungaji nae VEPE???!!!
Jamani mkiwa wachungaji na watu wa dini jaribuni kutoonesha upendeleo...mna waumini wa pande zote ...
 
Yeye ni Mtumishi Wa Mungu, afanye Kazi ya Mungu. Siasa awaachie wenyewe
 
Wachungaji wa shilingi wa kidigitali

Yeye anasema maisha yametulia sababu anajua ana uhakika wa kula kwa wale anaowadanganya kila siku
Anakusanya hela kwa kisingizio cha kumtolea Mungu hivi ni lini waliwahi kumpelekea hizo hela?
 
Yeye apokee sadaka atulie
Siasa awaachie wenyew kama hawezi ahamie kwenye siasa aache kazi ya utumishi
 
No comment; naona mabishano kati ya timu pinzani yanaendelea.
 
Tatizo viongozi wa dini wengi wa hapa tz ni wanafiki.
 
Sasa mkuu Lusekelo , unafahamu kwanini Gabon au Brazil watu waliandamana ? Baada ya kuhongwa barabara ya kuja kanisani kwako ndio umejisahaulisha haki za raia zilizomo kwenye katiba ?

Poor Mzee wa upako ! usicheze na haki za raia kukandamizwa , Mwl Nyerere aliwahi kusema hivi , nanukuu , " HATA KAMA TUTACHAGUA ASIYEAMINI MUNGU TUTATAFUTA UTARATIBU WA KUMWAPISHA , NA NI LAZIMA AAPE , KWAMBA ATAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA TANZANIA " mwisho wa kunukuu , nakuuliza Tena ndugu yangu Antony , Ambaye tukisafiri kwenda nyumbani wote tunakula lunch pale KITONGA COMFORT , ulielewa maana ya hoja hii ya Mwl Nyerere ?
 
Mimi nchi hii namwamini mwalimu mwakasege, hao wajanja wa mjini hapana kabisa Mungu atusaidie
 
Mwakasege huyu aliyetaka kugombea ubunge Arusha mjini kwa tiketi ya ccm au mwingine ?
Humjui vizuri Huyo mtu hajawahi kuwa na hayo mawazo ni propaganda za ccm tu, the man is strong himself angalia hata Huduma anayofanya ni kwa kila mtu na hana majivuno kama wachungaji wetu wengi habagui na kitu unachopaswa kujua mwakasege ni mchumi na aliacha kazi hiyo ili amtumikie Mungu wake vizuri kwa uhuru usitegemee atakuja kugombea ubunge sahau kabisa
 
Tangu malaika amtembelee kanisani kwake bac chadema hatupumui!!
 
Ninamuheshimu sana mzee wa upako ila kuongelea siasa kwenye mahubiri Hapana! Si vyema! Ni kama kanunuliwa anashusha hadhi yake
 
Kutoka kwako hakuna jema la kutararajiwa
 
Hivi ile barabara inayoelekea kanisani kwake aliyoahidiwa imeshajengwa?wachungaji awamu hii wamekuwa watiifu kwelikweli kwa...zama zile saahizi kwa yanayoendelea tungesikia matamko mengi ya kulaani,kuna ka aina fulani ka ubaguzi.
 
Najua sana Maswala ya Imani za Kipentecoste, Wapo wachungaji ambao kweli Nia yao Ni Kusaidia Wakristo walio makanisani mwao kiroho na Kijamii. Ila Nasema Mbele za Mungu na ananisikia, Nina Uhakika 900,000% Kuwa Anthony Lusekelo ni TAPELI. ajaribu Kubisha kuna Nyeti zake mahali fulani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…