Mchungaji amzawadia NYUMBA mwanafunzi bora wa shule yake ya msingi (Best student)

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
5419279_fbimg1496261209008_jpegdb3edf4ae50d3e3ab49d40bff15da775

Mchungaji Chinyere(Mwenye shati yenye rangi ya maziwa) akiwa na furaha baada ya kukabidhi hati ya nyumba yenye jina la mtoto husika kwa wazazi wake.
5419280_fbimg1496261204901_jpegea7acdcceecd610b97b4ff3b7b420757

Hii ndio nyumba aliyopewa mtoto huyo wa kike kama zawadi ya mwanafunzi bora wa shule hiyo ya msingi.
Tukio hili ni nchini nigeria

Maoni.
Wachungaji pamoja na Kupokea zaka na sadaka zetu hadi kuwafanya kuwa matajiri wakubwa
Kumbukeni kurudisha kwenye jamii kwa mifumo inayohamasisha maendeleo...
 
Taarifa haijajitosheleza mkuu,,,mtoto anaitwa nani?shule anayosoma ni shule gani?huyo mchungaji ni wa kanisa gani,hiyo habari inatokea mkoa gani au nje ya tz...meza mate kwanza mkuu ili ulete habari inayojitosheleza
 
Kwahiyo huyo aliekumbatia hapo chini ndio mama??? (Nauliza tuuu)
 
5419279_fbimg1496261209008_jpegdb3edf4ae50d3e3ab49d40bff15da775

Mchungaji Chinyere(Mwenye shati yenye rangi ya maziwa) akiwa na furaha baada ya kukabidhi hati ya nyumba yenye jina la mtoto husika kwa wazazi wake.
5419280_fbimg1496261204901_jpegea7acdcceecd610b97b4ff3b7b420757

Hii ndio nyumba aliyopewa mtoto huyo wa kike kama zawadi ya mwanafunzi bora wa shule hiyo ya msingi.

Maoni.
Wachungaji pamoja na Kupokea zaka na sadaka zetu hadi kuwafanya kuwa matajiri wakubwa
Kumbukeni kurudisha kwenye jamii kwa mifumo inayohamasisha maendeleo...
Nimeipenda hii,kama anavyofanya TB Joshua,niliwahi kuona amepeleka msaada wa chakula wenye thamani ya tani kadhaa nchini Equado .
 
:) :) duniani siku hizi ukifanya jambo jema watu lazima wakushangae tu!!!, mzee wa watu labda kajitolea kweli ila lazima watu wamtilie shaka maana kwa karne hii nothing goes for nothing "quid pro quo"
 
mimi siwezi kutoa sadaka kanisani wala dhaka wala chochote. mungu hana soko huko mbinguni pesa twampa ili iweje? mimi hutoa sadaka kwa wagonjwa, wasiojiweza, wajane na wengine wenye mahitaji. hawa wachungaji wa siku hizi kanjanja, wanatumia ujinga wetu kujitajirisha. tena wengine wanatumia nguvu za kiza kuwavuta waumini dhaifu. watasubiri sana kwa mie. mingu kaeleza utaratibu mzuri wa kutoa sadaka. si kumpa mtu yeye anunue prado waumini muendelee kuwa masikini, kisha awarubuni wake zenu. swine
 
usitoe sadaka kanisani. kawasaidie yatima, masikini, wagonjwa, majeruhi, wahitaji, vilema. hawa kanjanja wanajiita wachungaji wenye upako waepuke sana. wanatajirikia ujinga wetu. wanatutia hofu kuhusu maisha ya baada ya kifo na kututia matumaini ya uongo. wanatumia giza kutupofusha.
 
Back
Top Bottom