Mchungaji afumaniwa na Mke wa Mwanakondo LIVE. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji afumaniwa na Mke wa Mwanakondo LIVE.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jun 3, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa wale mnaojitutumia kuwa ni "wana wa mungu milio safi " lakini pia mnapenda kula uroda nje ya ndoa zenu na wana kondoo yawapaswa kuepuka jambo hilo kwani iajapo siku Mungu atasema nanyi kwa matendo ..Bofya hapo chini kushuhudis kisago kikali na matembezi ya "mshikamano ya aibu" kwa Mchungaji na Mke wa Afande huko Kenya waliofumaniwa wakivunja amri ya sita:

  Jungle Justice: Kenyan Pastor caught fornicating with a Policemans wife

  Ni kwa tahadhari tu ya kukumbushana. Nimeshindwa kuleta hizo picha za aibu hapa jukwanai labda kama mods wanaweza kufanya makeke ya kiatalaam zikae sawa kwa hadhi ya kuonywa hapa.
   
 2. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Lord have mercy
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hii mbona ipo zamaaani hapa.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  we ngoshwe ni una upungufu wa akili, nilikuwa sitarajii hata wewe ni mjinga kiasi hiki...sasa unachoshangaa ni nini hadi kuwatukashifu hao wanaojiita wana wa mungu, cha ajabu ni nini? kwa akili yako hii hujawai kuona?....

  sio wachungaji tu, mapadri pia wanazini na kuzaa watoto kibao...

  sio mapadri na wachungaji tu, mashehe nao wanafanya maovu mengi...wanazini, wanaua, wanafuga majini wanakuwa waganga wa kienyeji etc...izo zote ni dhambi usihesabu dhambi moja tu...

  sasa unachotakiwa kuelewa kwenye akili yako ni kwamba, mwanadamu yoyote kuna wakati anaweza kuwa mcha Mungu, lakini pia kwasababu shetani huwa anatafuta watu awaangushe, kama mwanadamu huyo hatakaa vizuri anaweza kutenda maovu kama kawaida hata kama ni mchungaji au padri au mtu yeyote yule...sasa kinachotokea ni kwa watu wa akili yako wanaochukulia mwanadamu mwenzao aliyeteleza hadi kuanguka kuwa ni ajabu kweli, kumbe wewe ngoshwe hapo unaweza kuwa unazini kila siku, unalawiti na kufanya uchafu wote,...lakini mwanadamu mwenzio akifanya hivyo tayari unakashifu na imani nzima..

  kinachokufanya uandikwe kwa malice ya kukashifu imani nzima ni nini? hakuna malaika, mtu yeyote kama hajakaa vizuri na MUNGU wake anaweza kutenda dhambi...na huyo mchungaji ni mmoja wapo wa watu ambao hawakukaa vizuri na Mungu...ndo maana wakafanya dhambi hiyo...na huyo si wa kwanza na wala si wa mwisho kwasababu shetani hajafa....kwanza hii issue ya kenya ilishajadiliwa hadi ikachoka, kisumu pastor hii si ngeni...huyo ni mmoja tu, mapadri na mashehe wanaozini huko na hawaongelewi ni wengi kuliko huyu mmoja.

  sisapoti alichofanya uyo pastor, lakini napenda kuwaambia kuwa, wachungaji si malaika..wanaweza kufanya kosa kama wewe kwasababu shetani anapigana nao usiku na mchana na wakiwa legelege...shetani anawadondosha na kuwaaibisha..LAKINI HIYO HAIMAANISHI KUWA WALE WANAOIFUATA IMANI YA KWELI WAMEPOTEA..HUYO NI MCHUNGAJI MMOJA TU na amedondoka kivyake, wengine wasiodondoka wanaendelea na Mungu wao kama kawaida...na tunazidi kusonga mbele....na wewe ngoshwe kama uko sawa uwe wa kwanza kurusha jiwe hapo...
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ngoshwe hii ilishawahi kuwekwa humu, ikitokea gpl
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  mzee ubungo..binafsi nimekuwa nikikuheshimu katika hili jukwaa, na hakika sijawahi kumtolea mtu kashfa za wazi wazi kama hizi. Nilichokiandika sidhani kama kinamgusa mtu binafsi kama ambavyo wewe ulivyoipokea na kunishambulia binafsi upeo wangu..sio vizuri mzee kulumbana kwa staili hii.
  Mimi ni mkristo kama wewe, na natambua mafundisho na kwa hilo siwezi kusema kuwa nipo safi..na hata nilivyoandika sikumaanisah kutaja kundi fulani la watu au dhehebu fulani nimeandika kwa ujumla "kwa wale wanaojiita wana wa Mungu lakini wanafanya uzinzi nje ya ndoa zao" .

  sijui kama kwa kauli hii nimekumaanishA wewe binafsi au imami yako, NA SIJUI KAMA WEWE UNAJIITA MWANA WA MUNGU NA UNATENDA UZINZI PIA.., ya nini kunishambulia KUWA NI MJINGA WAKATI SIJALENGA KUMTUKANA MTU AU IMANI YAKE KATIKA MADA YANGU?. Is not fair mzee kuniita mjinga kwa jambo kama hili ambalo ni dhairi sikumaanisha kumwelekezea mtu yeyote kwa nafsi yake binafsi katika hili jukwaa. Achilia mbali wewe uliedhamiria kunitusi kihivi wazi wazi. heshima hazina soko mzee..ni vizuri tukapima pia athari ya kauli zetu, zinatuanika na kuoneka kuwa hata yale tunayosema tunayafuata ni bure..mkristu safi hawezi kumtukana binadamu mwenzake iwe wa dini yake au nyingine eti kisa anatetea imani yake...labda kama anasukumwa na utashi usio wa kimungu!.

  Uungwana siku zote unatambua kuwepo kwa tofauti katika jamii, na fikra zetu ndizo zinatutofautisha pia. Jambo lililo jema ni kuelekezana tunapopotoka na sio kushutumiana na kukashfiana kwa jinsi hii tena katika mazingira mabayo tunataka watu waendelee kutuona sisi ni wasafi wa mioyo na matendo yetu..

  Kamwe haiwezekani kusema wote tumeokoka na kujivuna dhidi ya wenzetu wakati bado tu wadhambi. Tupime pia wanayosema wenzetu na kuheshimu pia utu wao kwani busara hainunuliwi sokoni.

  Mzee binafsi sijaona nilipokosea. Hivyo singependa kuvunjiana heshima. Nitaendelea kukuheshimu na kuchangia kwenye hoja zako pasipo chuki za wazi kama hivi.

  Mungu akufunulie kujua jinsi gani sijafurahiwa na haya makombora uliyonielekezea.

  Ubarikiwe katika imani yako, ukapate kuijua kweli na hiyo kweli ikakuweke huru.

  Amen.
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ngoshe hapa naona kama umeandika kwa visa fulani hivi...umeandika kwaajili ya kuisaidia jamii au kuwakashifu wafuasi wa imani hiyo?....mbona unakuwa kama waadishi wa magazeti ya udaku kuleta breaking news ya hewa? hawa ndo waandishi wetu wa habari makanjanja wanaofanya jambo kuuubwa kumbe ndiyo jamii yetu ilivyo...
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sina kisasi mzee na wala sikulenga kumkwaza mtu binafsi niliiltea kwa tafrisi inayofanana kutoka katika hiyo habari husika ambayo imetumia lugha ya Kiingereza kama ifuatavyo:

  " A pastor has been found deceiving his wife with a policeman's woman in Kenya. People of the Christian community did offer him no grace, especially because he was preaching in a crusade about adultery.

  Labda tuepuke kujitetea zaidi katika imani zetu kwani wote ni wadhambi. Hakuna aliyemsafi na hii ni kukumbushana tu wajibu wetu katika ndoa na mahusinao kama ambavyo mistari ya Bibilia na Quran tukufu inavyorejewa rejewa kila siku na haiishi kusimuliwa kama ilivyo vitabu vingine ya kujisomea..
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  sasa cha ajabu hapo ni nini...kwani huyo ni wa kwanza, hivi tukianza kuweka mmojammoja hapa kuanzia mapadri wako hapa patatosha....cha maana ongelea jamii nzima, ukiongelea pastor wa watu fulani automatically unakuwa unapunguza morali ya wale walioko kwenye imani ile, na kwa mtu mwenye akili analijua hilo hata kabla hajaandika hivyo analiepuka mapema...ngoja ukimaliza hii, mimi nitaweka yangu hapa ya kulawiti watoto kwa mapadri wanaohubiri kila siku makanisani...nikitoka hiyo naweka ya uganga wa kienyeji wa waislam, nikimaliza hapo naleta ya ushoga wa waanglikana...ukiona hivo utagundua kuwa, hatutakikwi kuelezea mtu mmoja hasa anayegusa jamii ya watu wengi kwasababu unakuwa unawaofendi wale watu sana...inabidi uongee kwenye mtazamo wa jamii nzima kuancha uovu na si chuki zako binafsi juu ya watu wa imani hiyo..unahitaji maelezo mengine kweli hapo..yaleniliyokupa haujaelewa....mwisho, hapa hatuheshimiani, tunaongea kwa point ndo maana tunajadiliana na wala hatujuani...so ondoa heshima kwangu,,,nirekebishe pale panapohitajika na mimi nitakurarua vizuri tu pale unapokosea kwa mtazamo wangu..Ok?
   
 10. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,549
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Kaka taratibu mbona una kuja juu namna hii...you have made it too personal.. matusi ya nini.. inaonekana unapenda sana ubishi wa kidini na kufanya issue kuwa za kidini... acha mkuu hapa hukumtendea haki jamaa.:angry:
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ok, yameisha lakini message sent pamoja na kwamba najua you are the same gonshwe on the other side of the coin kwa jina lingine kwa kifupi kama hauelewi....:angry:
   
 12. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jazba za Kidini mzee hazitusaidi..na sio rehema hata kidogo kuonyesha chuki hadharani dhidi ya wenzio kwa kauli mabzo hazijaelekezwa kwako binafsi. Harafu wakati huo huo unajifanya au unataka watu wakuone "UMEOKOKA/UNAMPENDA MUNGU/ U MWANA WA MUNGU NK". HAKUNA ATAKAE KUAMINI KWA HAYA MZEE LABDA KAMA NI KATIKA DINI YA MASHETANI....MKRISTO MWEMA HANA VISASI NA MAJIBIZANO YASIYO NA BUSARA.
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  vyovyote vile utakavyoelewa, cha muhimu ni kwamba,wewe ndo umekuwa mdini na umeweka hii ili kukashifu imani ya wenzio, unatakiwa uone aibu kwa hili na katu sitalivumilia...vyovyote vile unavyotaka kuamini, ukileta utumbo hapa si kwamba kwasababu mtu ameokoka ndo atakuacha tu uikashifu imani yake wakati anaangalia...kama nilivyokuambia, subiri si muda mrefu kwenye thread yako hii hii nitakuletea yale ya kina padre kimaro na wengine duniani ili tupambanishe...kama hauniamini mimi, waamini wengine...mimi nitatetea maslahi yango siku zote na wala usilete icho kama ndo kisingizio, utakuwa una upungufu wa fikra.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Nalipenda hili jukwaa; mnavaana mnapeana za uso then mnamalizana kwa kugongeana senksi! aaaaaaaaaaaah hii safi hii!
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Heshima mbele Mkuu,

  ubarikiwe kwa yote bana.
  Lakini sina muda wa kuendeleza malumbano na mtu hapa mzee..I respect your opinions! Endelea tu manake sijui kama mimi nimegusia imani yako binafsi kihivyo mpaka povu linakutoka mdomoni kutaka malumbano yaendelee baina yetu na ambayo yanaashiria kuathiri waungwana wengine humu jukwaani.

  Kila la kheri Mzee, lete tu unayoona yanafanaa ili ujinga wangu na busara zako wewe uliye mwema na mwelevu mbele za Mungu na wanadamu wengine vipimwe kwa mizani iliyosawia.

  Lakini binafsi niweke wazi kuwa kamwe zitaweza kulumbana juu ya Imani za dini za watu kama unavyodhania, kwani sijui ipi ni dini iliyobora machoni pa Mungu kati ya yako, yangu au zile za wanadamu wengine.Hiyo haitanisaidia chochote maishani mwangu..

  Mada yangu imegusa Mchungaji wa kikristu nchini Kenya na wala hajatajwa wa dhehebu gani, na pia hujajua hata mimi mwenyewe nilieleta hii mada ni wa dini au dhehebu gani, lakini unakurupuka na kuanzisha malumbano yasiyo na msingi kujaribu kutetea vitu vilivyowazi utadhani ni wewe umetajwa binafsi katika hili.


  Sipo hivyo Mzee. Jaribu tena baadae!

  Amen
   
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  angalia kekundu alafu acha unafiki bwana mkubwa..hauongelei udini wakati iko wazi umeileta hii kwania ya kukashifu dini?...unafikiri watu hawana akili..mimi mwenyewe sitaki kulumbana na wewe kwasababu naona hauelewi..

  kumbe unaongelea mchungaji wa kikristu? nilifikiri unaongelea padre wa kikristu....hapo utapata jibu mwenyewe wapi umekosea. kwaheri, tuendele na mada zingine mkubwa...ila ilikuwa muhimu kwangu kukushushua ili ubadilike....

  usiongee kama mtoto mdogo kwamba sijui mimi ndo mtu wa mungu sana, sijui ndo mwema,..iyo ni akili ya watoto wadogo...umri wako ni upi bwana ngoshwe? how old are you nisijekuwa naongea na mtoto hapa...
   
Loading...